Juliana Shonza, Mtela Mwampamba wahamia CCM...

Juliana Shonza, Mtela Mwampamba wahamia CCM...

Sasa imetimia kauli na maono ya walio wengi wenye busara na hekima ya kutazama mambo kwa weledi mkuu. Kwa yaliyokuwa yanaendelea Chadema yakiratibiwa na kupigiwa chapuo na BABU wa Chama hiko na watu wa kundi lake, sasa yamedhihiri kuwa yanakimaliza na kukizika moja kwa moja Chama hiko.

Ni jambo la hatari kwa chama ambacho viongozi wake wana uwezo wa kukandamiza, kubaguza wenzao kwa namna wanavyojisikia bila kuzingatia mchango wao, hadhi yao na muruwa wao., wanaweza kufanya lolote kwa yeyote ndani ya Chama kwa kadri wanavyojisikia wao.

Ni hatari kuwepo watu miongoni mwa jamii ambao Ubaguzi kwao ni Sera ya kujinadi kwa watu, ni hatari sana...!

Shonza na Mwampamba wameiona hatari hiyo na vijana na wanachama wengine wa CHADEMA waione hatari hii ya kuongozwa na watu ambao hawajui nini maana ya kuwa kiongozi, hawajiheshimu wenyewe na hawaheshimu wengine, ni watu ambao maslahi binafis yanatangulia maslahi ya wengi, hawana uzalendo na wamekosa hata chembe ya Utaifa.

Watu wanaohubiri chuki na kuhamasisha Utengano, watu ambao wamekosa mapenzi na Taifa lao kiasi cha kuwa tayari kufanya lolote ili kuhakikisha kuwa nchi hii haitabiriki na kuandika ripoti za uongo na uchochezi kwa mataifa makubwa na jumuiya za kimataifa kuwa TANZANIA si sehemu salama ya kuishi wala kuwekeza, ni wazandiki wasiolitakia mema Taifa hili.

Chadema kuna Viongozi ambao hawatendi haki baina yao kama viongozi lakini pia hawatendi haki kwa wanaowaongoza, wanaipinga na kuikataa kweli hata ikidhihiri mbele ya macho yao.

Ni watu ambao hawaheshimu, hawasimamii na wanapuuza Katiba waliyojitungia wenyewe, hawako balanced katika maamuzi wala katika hukumu.

Natoa ANGALIZO Kwa vijana ambao wanajitoa kuijenga na kuitetea CHADEMA umefika wakati sasa wa ninyi kuiona hatari hii ndani ya Chama hicho mnachokiamini na kutafuta Chama kingine ambacho hayo yanayowakuta chadema hayatowakuta., Karibuni CHAMA CHA MAPINDUZI.,Chama kinachodumisha mapinduzi na mageuzi ya kweli katika jamii.,Chama kinachotoa fursa kwa wanachama wake kusikilizwa na kuthaminiwa kwa michango yao na huduma yao kwa Chama.

Napenda kuchukua fursa hii kumtaka Zitto Kabwe kuiona hatari hii lakini pia kumkaribisha CCM, ambako michango yake itathaminiwa na wala hatobaguliwa na kunyanyaswa bali atathaminiwa na kuheshimika.

Nawapongeza JULIANA SHONZA na MTELA MWAMPAMBA kwa kuiona hatari iliyoko chadema na kuchukua uamuzi wa kujiunga CCM, naamini wataleta michango bora na mawazo yenye kujenga.

Kwa wale wafuata upepo na mashabiki wa siasa, hii ni fursa kwao kujikumbusha fasihi ya TOPAN kwenye MFALME JUHA aliposimuulia kisa cha BAKARI na WALII walipofika nchi ya kichaa ambayo mfalme wake alitoa tangazo la kila kitu ratili moja kwa pesa moja na WALII kumtaka BAKARI wahame nchi hiyo ila BAKARI aling’ang’ania kubaki na yaliyomkuta mnayajua…!

Karibuni CCM.,Umoja wetu ndio ushindi wetu...

Magari na Nyumba Mtapatiwa... AJIRA PIA


[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Juliana Shonza akijitambulisha kwa wana CCM leo tarehe 12/2/2013, katika Makao Makuu ya CCM,mjini Dodoma[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mtela Mwampamba akijitambulisha kwa wana CCM,wakati wa sherehe za utambulisho wa wajumbe wa kamati kuu ya CCM.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Ni umburula kudhani vyama vya siasa ni wazazi,shonza na mwampamba wanahaki ya kwenda kokote watakako,ili mradi nafsi iamini tu kwamba huko aendako atapata akitakacho,kukejeli au kutukana hakuna tija.nawapa hongera sana kwa maamuzi yao,wametii haja ya nafsi zao.
Kama suala ni kuamini tu basi na uamini kunywa sumu ya panya na usife,CCM NI SAWA NA SUMU YA PANYA AU SUMU NYINGINE ILIYO HATARI,KUMBUKA SUMU HAIONJWI,HUWEZI KUNIAMBIA WAMEAMINI CCM NI CHAMA CHA KULIKOMBOA TAIFA HILI,HATA KIPOFU ANASIKIA UFISADI UNAOTENDWA NA MACCM NA MATOKEO YA UFISADI HUO NI VIFO VINAVYOTOKANA NA KUKOSA HUDUMA ZA AFYA,AJALI ZINAZOZUILIKA,VIFO VYA NJAA NK
 
Hata akina Shitambala,Warid Kaburu,Tambwe Hiza na wengine wengi walienda kwa mbwembwe wako wapi sasa?
 
oil chafu imekuwaje tena? Hawa mbwa wa magamba wanakatisha tamaa ya kufanya siasa hapa tanzania!

pisto lerohakufanya lolote baya linalostahili, kukufanya wewe umuite mwana jukwa mwezako mbwa, hii lugha yako ndugu inamaanishe wewe ni mhuni, usiyejua siasa au namna ya kuweza kumjibu mtu katika mazungumzo ya aina yoyote ile. Hapa tulipo umedhahirisha kuwa wewe ni mwana cdm, na ni haki yako ya kidemokrasia, jee ungependa kuitwa jina kama hilo?????????
 
Duh, sasa hawa mambulula walikuwa wanabisha nini kuwa walitumwa na mkoloni mweusi (CCM) kuichafua Chadema? Maskini Umma ushajua mchezo wao mchafu hilo ni doa ambalo halitatoka kamwe, kwa kifupi siasa zishawashinda, watutumiwa kutukana Chadema kipindi fulani majukwaani halafu mwishowe watapotea kabisa. Ndugu zangu hatutawasikia tena, R.I.P J Shonza and Mwampamba
 
JAMAN ACHEN KUWAJADILI CHADEMA WAHUNI nani asiyejua kuwa aslimia 70 ya watu wa CHADEMA NI WAHUNI lile ni genge la wahuni nshasema na ntaendelea kusema yaan haiwezekan tukawavumilia wahuni ndani ya nchi uko wapi kova wavue magwanda hao
 
Kabaki zitto kabwe naye inabidi ahame pale wale watu chama wanakipeleka kikabila zaidi upuuz na wizi mtupu
 
Ndugu zangu tusiwalaum Shonza na mwenzake mimi nawaunga mkono isipokuwa bora wangeenda NCCR kuliko huko kwa MAGAMBA.Dk slaa ni mbinafsi sn na wasipoangalia wengi watatimka.Nahisi babu uzee unamsumbua,otherwize vijana wako sahihi.
 
Ritz wakaskazini maana yake nini?? teh teh teh sasa hv kibao cha kuchoma misikiti kitawageukia
 
Last edited by a moderator:
Kifupi ni kwamba kazi waliyotumwa ndani ya CHADEMA imewashinda, bora warudi makao makuu wakajipange upya, VIVA CHADEMA
 
Kutokana na akili zao kuwa fupi watakuja kusema wao bado wanachama wa CHADEMA subirini.
 
Nani kati ya hawa njuka alikuwa machachari kuliko MASUMBUKO LAMWAI? muulize LAMWAI baada ya kurudi CCM mambo imekuwaje? jibu ni simple, hakuwahi kutamba tena kwenye huu ulingo wa siasa! Sembuse JULIANA, sembuse MWAMPAMBA!
wasifurahie kukumbatiwa na DHAIFU hapo wakadhani watakaa waonane naye tena kabla ya 2015. Kwaherini vijana kwenye siaza za Tanzania ndio tumewazika hivyo!
 
Naona my milk za bi dada zimestand mpaka shati haifungi.
 
Taarifa zilizopatikana muda huu ni kwamba JUliana Shonza na Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la mbozi mashariki(MTELA ALLAM MWAMPAMBA) wamehamia CCM NA KUPOKELEWA NA MWENYEKITI WA CCM TAIFA RaisKIKWETE Tukio la kuwapokea vijana hao limefanyika Dodoma mbele ya Rais wa nchi (MWENYEKITI WA CCM TAIFA) Mh. Jakaya Mrisho Kikwete. Vijana hao ambao wameteka mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa, Wamepewa nafasi ya kutoa ushuhuda wa kile kinachofanyika ndani ya CHADEMA. Kila mmoja ametoa ushuhuda wake kadri alivyotendewa na yanayotendeka ndani ya CHADEMA. Mapokezi yao yamekuwa makubwa sana kutokana na kuunganishwa na shughuli zingine za kichama zinazomalizika muda si mrefu. Taarifa zaidi itakujia nikifanikiwa kupata VIDEO nitaiweka, Dr J.Kikwete awapokea rasmi muda huu,,!!
919665090.jpg
Juliana Shonza akijitambulisha kwa wana CCM leo tarehe 12/2/2013, katika Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma​
119763348.jpg
Mtela Mwampamba akijitambulisha kwa wana CCM, wakati wa sherehe za utambulisho wa wajumbe wa kamati kuu ya CCM.​
700794081.jpg
Mwenyekiti wa CCM-Taifa, Rais Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wapya wa CCM, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba, kushoto kwenye picha ni Makamu Mwenyekiti CCM-Bara ,Ndugu Philip Mangula na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahaman Kinana.​
katika hili kuna aina mbili za mambo ya kujifunza kwanza kwa chadema yenyewe itambue namna ya kufanya hata michujo ya wagombea mbalimbali na watambue si kila aliyevaa gwanda na kusema peopless ni mwenzao na ana nia njema 2 ccm unaonesha na kudhihirisha jinsi ilivyo desperate kama alivyotamka ndugu heche kuwa wamefikia sehemu mtu yeyote akijitokeza kuwwa ni chadema inaandaliwa sherehe na kupokelewa na mwkt wa taifa aibuuu hawa makanjanja wanapokelewa watu wote hao mnaacha kujadili mambo ya msingi ya kitaifa mnajadili wajinga mliowapa rushwa kwa muda mrefu eti wamejitokeza hadharani?
 
SIO ahamia CCM bali arejea ofisini kwake ccm, huyu mdada ni Ccm hajawahi kuwa upinzani, ni shushushu mbona tokea Mlimani anafahamika... Enewei kaishia pabaya

CHADEMA kimemjenga hata akawa Juliana. CHADEMA ni taasisi kubwa ambayo magamba wanaiogopa, na wanaotoka huko (oili chafu) CCM wanaiona LULU. Ila wakiingia humo (CCM wanapotea kabisa. Hawana hela za kuwafanya wang'are kule!
 
RIP (politically) nyie ndio mmemaliza..ccm ina wenyewe ha ha ha..kumbe kweli cdm wakisema huyu wala sio uongo!!
 
Back
Top Bottom