Watanzania hawawaamini tena CCM.
Wakati
hao mamluki wanarudi kwa mabwana zao
baada ya kufukuzwa CHADEMA, watanzania kwa maelfu wanahamia Chadema.
Mifano miwili hii hapa kutokana na kazi ya Kamanda Mawazo:
na Victor Eliud, Geita
MIKUTANO ya vuguvugu la mabadiliko (M4C) inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imetikisa Jimbo la Busanda, wilayani Geita, mkoani Geita, baada ya wanachama 18,670 wakiwamo wazee na makada wa siku nyingi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutimkia CHADEMA.
Mbali na kuzoa maelfu ya wanachama, pia chama hicho kimeunda uongozi kwa kuteua wenyeviti, makatibu, na wahazini wa chama kwenye kila kata zilizokuwa hazina uongozi ngazi ya tawi.
Viongozi waliosimikwa ni wenyeviti, makatibu, wenezi na wahazini wa matawi pamoja na wale wa jumuiya mbalimbali za chama hicho hususan wazee (BAWAWACHA), Vijana (BAVICHA) na Wanawake (BAWACHA), lengo likiwa ni kukiimarisha chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake kwenye jimbo hilo juzi, Kiongozi wa M4C mkoani Geita, Alphonce Mawazo, alisema wana CCM waliojiunga na chama hicho ni kutoka kata 13 kati ya 16 za jimbo hilo.
Alisema kati yao 11,235 ni wanachama wapya na 7,435 ni waliovua gamba na kuvaa gwanda, ili kuhakikisha CHADEMA kinaibwaga CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuingia Ikulu.
Aliwataja miongoni mwa wazee na makada wa siku nyingi wa CCM waliorudisha kadi za CCM ni Thereza Lugembe (79) mkazi wa
Kijijicha Nyabulolo, Kwando Maduhu (109) mkazi wa Kijiji cha Nyarugusu na Shija Mihambo (87) mkazi wa Bugogo Bukoli ambaye alikuwa mwanachama wa CCM tangu Julai 7, mwaka 1979 kwa kadi namba C.812836.
"Kazi hii si ndogo…tunapambana na chama ambacho kina mizizi kila kona…tumezoea kuona vijana ndio wanajiunga na CHADEMA…lakini unapoona wazee nao wameanza kukimbia ujue saa ya ukombozi imekaribia," alisema Mawazo.
Chanzo: Tanzania Daima
na Lucy Ngowi, Chato
MAKADA 201 wa Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Mwenyikiti wa Kitongoji cha Buhungu, Kata ya Kigongo, wilayani Chato, Mkoa wa Geita, wamejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kujiunga CHADEMA kwa wana CCM hao kunatokana na mikutano ya vuguvugu la mabadiliko (M4C), inayofanywa na chama hicho cha upinzani katika maeneo mbalimbali likiwemo Jimbo la Chato, ambalo Waziri wa Ujenzi, John Magufuli ndiye mbunge wake.
Makada waliotimkia CHADEMA kwa nyakati tofauti ni kutoka
Kijijicha Muganza, Kasenga, Busaka na Igando, Kata ya Bwera ambapo walidai kuchoshwa na mwenendo wa siasa za CCM, hali ambayo imewasababisha waendelee kuwa na maisha magumu huku viongozi wao wakiendelea kuneemeka.
Mbali ya makada hao wengine waliojiunga na CHADEMA ni Katibu wa Umoja wa vijana wa CCM kata ya Muganza Paulo Malulu, Katibu wa Tawi la CCM Kijiji cha Mkombozi, Christopher Charles na Mwenyekiti wa kitongoji cha Buhungu Kata ya Kigongo, Razaro Busumabu.
Akizungumza muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano huo, kwenye Kata ya Muganza, Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Chato, Alex Mukama, alisema wananchi wa Jimbo la Chato wamekipokea chama hicho tofauti na awali waliogopa kujitokeza hadharani.
Kwa upande wake Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chato, Mange Ludomya, aliwataka wananchi kukipa kisogo CCM kwa kuwa kimeshindwa kuboresha maisha ya wananchi kwa miaka yote.
Chanzo: Tanzania Daima