Juliana Shonza, Mtela Mwampamba wahamia CCM...

Juliana Shonza, Mtela Mwampamba wahamia CCM...

Taarifa zilizopatikana muda huu ni kwamba JUliana Shonza na Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la mbozi mashariki(MTELA ALLAM MWAMPAMBA) wamehamia CCM NA KUPOKELEWA NA MWENYEKITI WA CCM TAIFA RaisKIKWETE

Tukio la kuwapokea vijana hao limefanyika Dodoma mbele ya Rais wa nchi (MWENYEKITI WA CCM TAIFA) Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

Vijana hao ambao wameteka mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa, Wamepewa nafasi ya kutoa ushuhuda wa kile kinachofanyika ndani ya CHADEMA. Kila mmoja ametoa ushuhuda wake kadri alivyotendewa na yanayotendeka ndani ya CHADEMA.

Mapokezi yao yamekuwa makubwa sana kutokana na kuunganishwa na shughuli zingine za kichama zinazomalizika muda si mrefu.

Taarifa zaidi itakujia nikifanikiwa kupata VIDEO nitaiweka, Dr J.Kikwete awapokea rasmi muda huu,,!!



543667_10200318953750526_1713528751_n.jpg

​

Mbona alisema yeye bado Makamu Mwenyekiti wa Chadema? Piga ngumi ukutani utaumia mwenyewe, wameona wenyewe na kuamua kuhamia kwa waliowatuma. Kazi kwelikweli.

Mwampamba amekata rufaa anahama kabla rufaa yake haijasikilizwa?
 
CCM wamefanya haraka sana kuwachukua hawa kina Juliana kwakuwa Kila mtu alikuwa anajuwa wanatumika.....hata statement walizokuwa wakizitoa zilikuwa zinaratibiwa na CCM na the like of Mwigulus......this is failure of CCM political Insurgency....
Kikao kimejawapo ...hao masalia walikutana na Watu wa Prince pale Best Bites...last week.
 
Wamenyanyasika sana vijana hawa wazalendo. Waacheni waendelee kutafuta njia mbalimbali za kuitumikia nchi yao. Kama wameona wanaweza kuitumikia nchi yao vyema kupitia CCM, why not?
 
bado slaa sasa sijui wapambe wataipokeaje taarifa hiyo siku ikifika dr. slaa naye atarejea CCM
 
Wamenyanyasika sana vijana hawa wazalendo. Waacheni waendelee kutafuta njia mbalimbali za kuitumikia nchi yao. Kama wameona wanaweza kuitumikia nchi yao vyema kupitia CCM, why not?
Hapana mkuu, hawajanyanyasika. Wao ndo walitaka kuinyanyasa chadema, bahati mbaya kwao na nzuri kwa chadema walistukiwa na Intelijensia. Mungu hamfichi mnafiki.
 
Ukimaliza fungate lako na CCM,uje hapa JF utuambie katika mahojiano yako na gazeti la mtanzania kuna maneno uliyasema kuwa wewe kama kamanda huwezi kuhama CHADEMA maana kwa kufanya hivyo ni sawa na kukimbia vita,hebu tuambie kilichojili kwenye uwanja wa mapambano vipi??majeshi yako yalikuwa yanatumia silaha duni za '47 mkasambaratishwa???teh,teh teh kwi,kwi.chezea vita wewe.

kama unaelewa siasa tambua kuwa mwanasiasa kuongea maneno na akatenda tofauti si jambo la ajabu. inategemea na mazingira yaliyopo. siasa ni mchezo mchafu. kama wewe unaichukulia kama msahafu unakosea. never believe politicians!
slaa aliwahi sema kuwa siku za shibuda zinahesabika. baada ya kusoma mazingira siku hizi anasema kuwa "watu wengine dawa yao ni kuwapuuzia".

natofautiana na wana jf waliyochangia kuhusu kuhama kwa juliana. isiwe "sizitaki mbichi hizi!" juliana alikua kiongozi bavicha. alikua na msimamo wa kuwakosoa viongozi wa juu hasa slaa na mbowe. sidhani kama hili ni kosa. inapotokea mwanachama anahoji jambo asiloridhika nalo asikilizwe.

baada ya kumkosoa slaa alionekana ni mhalifu, mtovu wa nidhamu, msaliti, kibaraka wa ccm......... siasa haiendi hivyo! kwa upande wangu naona kuwa ni pigo kubwa kwa chdm juliana kujiunga na ccm. chdm ijenge utamaduni wa kuwasikiliza wanachama wote. utukufu wa slaa na mbowe uhojiwe. tukiendelea kuwaacha watukufu, chama kitakufa
 
Nadhani hao wataongezwa kwa nape wafanyekazi kama ile ya Tambwe Hiza halafu wasahaulike kabisa.

Umenikumbusha mbali sana,Tambwe Hizza,kuna siku Makamba alimtuma kwenye mdahalo wa katiba mpya... CCM bwana,laiti Nyerere angekuwepo.
 
Nashukuru mmekwenda ccm.kwasababu mmeweka rekodi vizuri kwamba kile kilichokua kinasemwa ni sahihi,asanten sana for nice confirmation.
Nadhani sasa tukienda kwa wanambozi kuwaeleza umbumbu wa vijana wao watatuelewa,
 
Hivi yule wa Mr. Politician (Nakaaya) yeye aliishia wapi ndani ya hiyo CCM? Manake sijamsikia kitambo sana.
 
Wakati tukifunikwa na fikra za vijana hawa kwenda walikokwenda mimi natafakari mchezo ulivyochezwa!!! Sidhani kama kuna wanaJF wenzangu wengi wanaotafakari huu mchezo!

Anyway swali la kizushi je mchezo umekwisha?
 
Inamchoma mwenyewe


natofautiana na wana jf waliyochangia kuhusu kuhama kwa juliana. isiwe "sizitaki mbichi hizi!" juliana alikua kiongozi bavicha. alikua na msimamo wa kuwakosoa viongozi wa juu hasa slaa na mbowe. sidhani kama hili ni kosa. inapotokea mwanachama anahoji jambo asiloridhika nalo asikilizwe.

baada ya kumkosoa slaa alionekana ni mhalifu, mtovu wa nidhamu, msaliti, kibaraka wa ccm......... siasa haiendi hivyo! kwa upande wangu naona kuwa ni pigo kubwa kwa chdm juliana kujiunga na ccm. chdm ijenge utamaduni wa kuwasikiliza wanachama wote. utukufu wa slaa na mbowe uhojiwe. tukiendelea kuwaacha watukufu, chama kitakufa
 
Kupokewa na Rahisi ....sio jambo la ajabu....tena "atapokewa" kweli Kama kina hizi tambwe na Ashilombwe ambao sasa wanakufa na njaa...
 
Lengo letu ni kujenga Tanzania moja iliyo Bora. Katika kuijenga nchi yetu hakuna haja ya kunyanyasana badi tunapaswa kupeana moyo kuwa inawezekana.
Vijana hawa wapewe moyo zaidi wa kuijenga nchi yao. Walijaribu kupitia Chadema wakakwamishwa sasa wameona mwanga mpya. Anayejua utamu wa ngoma ni yule anayeicheza...
 
natofautiana na wana jf waliyochangia kuhusu kuhama kwa juliana. isiwe "sizitaki mbichi hizi!" juliana alikua kiongozi bavicha. alikua na msimamo wa kuwakosoa viongozi wa juu hasa slaa na mbowe. sidhani kama hili ni kosa. inapotokea mwanachama anahoji jambo asiloridhika nalo asikilizwe.

baada ya kumkosoa slaa alionekana ni mhalifu, mtovu wa nidhamu, msaliti, kibaraka wa ccm......... siasa haiendi hivyo! kwa upande wangu naona kuwa ni pigo kubwa kwa chdm juliana kujiunga na ccm. chdm ijenge utamaduni wa kuwasikiliza wanachama wote. utukufu wa slaa na mbowe uhojiwe. tukiendelea kuwaacha watukufu, chama kitakufa
Unaijua katiba ya chadema vizuri?
Unajua taratibu za mwanachama kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya viongozi?

Kutumia mitandao ya kijamii ndio njia sahihi?
 
Back
Top Bottom