Jukwaa hili mbona Kimya, kunani?

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,188
3,360
Nmekuwa member since 2012 ,nlikiwa mdau mkubwa wa hili jukwaa la tech pamoja na wakuu wengine, jukwaa kwa sasa naona linazidi kukosa post hata wachangiaji.

kadri muda unavyozidi kusonga teknolojia inazidi kuexpand lakini hapa jukwaani kadri muda unavyoenda jukwaa la tech linashrink,kuna tatizo lipi???

Naona hapa tz teknolojia hata haupewi heshima inayostahili, technology ndo kila kitu ulimwengu huu..
 
Tech imerahisishwa mno siku hizi mtu ana Google tu na kupata kila kitu
 
Ni sawa lakini mimi nimejibu kutokana na ninachokiona
Ni kweli ila google ni search engine tu kila hapa forum ndo inafaa zaidi kubadilishana mawazo na kupeana taarifa hata huko nyumba 2012 jf tech ipo on fire google ilikuwa unapiga mambo fresh
 
Ni kweli ila google ni search engine tu kila hapa forum ndo inafaa zaidi kubadilishana mawazo na kupeana taarifa hata huko nyumba 2012 jf tech ipo on fire google ilikuwa unapiga mambo fresh
Hakuna shida ngoja tuwasubirie au pengine siku hizi watu ni wajuaji zaidi kwenye tech
 
Hili ni moja ya jukwaa lililonipa manufaa sana hapa JamiiForums,hasa ktk jamii inayonizunguka..yaani wananikubali kweli kitaa naonekana mjanja mimi kwenye programs hasa ktk simu ila ujanja wote JF,watu kama Chief Mkwawa ndo wanalifanya jukwaa liwe active vinginevyo tungekuwa tunaongea mengine hapa.
 
Kuna tatizo moja nimeligundua. Watu wanaamini kwamba ukishakuwa mtaalamu wa kitu fulani , basi hakuna la kujifunza kutoka kwa yule asiye mtaalamu. HII NI FIKRA POTOFU. Mtu anaona kwakuwa yeye ni mkali wa hiki, basi akiwa na swali au shida au changamoto anaona hawezi kuileta humu jf kwa sababu anaamini kama yeye imemshinda basi humu hakuna msaada.
MFUPA ALIOUSHINDWA FISI, MBWA HATAUWEZA.

HII NI FIKRA POTOFU PIA.

Anyone can be a hero, anyone can be a star and anyone can be a professional.

Sasa basi. Tusife na matatizo yetu! Tuyalete huku.

Na pia wale mnaoangalia post mnazipita kisa hazihusiani na simu- android,ios,bb,wp. Sasa mbadilike . TECHNOLOGY SIO SIMU PEKEE, hata blender lako la nyumbani ni tech.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom