Wiki ya AZAKI: Sheria ipo kwa ajili ya kuwalinda Watawala sio Wananchi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
IMG_8851.jpeg

Join JamiiForums and BBC Media Action today October 24th, 2023 from 11:00 AM to 1:00 PM on CSO Week at Arusha International Conference Center (AICC)

Topic: Tracking Information Disorder (Including Dis and Mis-Information) in the era of Technological Advancements.

Kabla ya mada hii, JamiiForums imeshiriki mjadala kuhusu Demokrasia na Teknolojia ambao ulikuwa na wazungumzaji kadhaa akiwemo Maxence Melo, wakati Baruani Mshale akiwa ni mchokoza mada.


20231024_091746.jpg

====

Screenshot 2023-10-27 181918.png

Baruani Mshale: Teknolojia haiwezi kutumika kukuza demokrasia. Kama demokrasia haipo, teknolojia itatumika kukandamiza demokrasia, kama demokrasia ipo, teknolojia itatumika kuikuza. Teknolojia haiwezi kukuza kitu ambacho hakipo.

Screenshot 2023-10-27 182332.png

Maxence Melo: Kwenye uwanda wa kidijitali watu wengi hudhani kuwa wao ni wateja lakini ninyi ni bidhaa, ndio sababu mnaona maudhui ambayo yanaendana na tabia zenu. JamiiForums kwa kushirikiana na wadau wengine tumapambania ili kuhakikisha suala hilo halitokei kwa watanzania. JamiiForums hatutumii alogarithm bias ambayo ipo kwenye mitandao mingine.


Screenshot 2023-10-27 182352.png

Tonny Alfred (The Chanzo): Ukiangalia Online Content Regulations utaona kabisa aliyeziandaa alikuwa hana ufahamu wa masuala ya internet, na suala hilo liliwaathiri sana wazalisha maudhui. Ukifananisha na nchi nyingine, Wakenya wako vizuri zaidi kuliko sisi.

Serikali inapoleta sheria inayokandamiza matumizi ya uwanda a kidijitali inaleta hasara kwa wananchi ambazo ni matrilioni ya pesa.

Big techs kwa sasa zinafanya sensorship (uzuiaji wa baadhi ya maudhui) kubwa sana. Mfano meta wanafuata sera za Marekani hivyo kuna maudhui yanazuiwa kwa sababu ya sera za Marekani. Je, ni nini kitamzuia dikteta fulani wa Afrika kuzuia maudhui huku Afrika? Kuna hamu kubwa ya watu kuzuia maudhui dunia nzima!

Kwa wenzetu Marekani mtu akiwa banned, anaweza kuongea na Seneta akaenda hata Mahakamani, lakini kwa huku kwetu ni ngumu kuwawajibisha big techs.

Screenshot 2023-10-27 182525.png

Richard Mabala: Demokrasia bila Elimu haiwezekani. Ndio maana mwanzoni niliitaja kama moja ya misingi ya Demokrasia.

Tumezungumzia masuala ya VPN na kusimamia Haki zetu za Kikatiba lakini ni watu wangapi wanaelewa haya? Ndio maana tunakuwa na uoga, tunakubali “Kuliwa na Chawa”.

Hivyo tutapigania vitu vikubwa kama Mabadiliko ya Katiba lakini bila uelewa wa Mwananchi mmoja mmoja hakuna mabadiliko tutakayofanya.

Screenshot 2023-10-27 182410.png

Joseph Ngwegwe (Mwenyekiti wa Bodi JamiiForums): Natoa wito kwa Azaki kuacha kuwa “Wahanga” na kujifanya kama hatuna cha kufanya. Tuchukue nafasi ya uongozi.

Vyombo vya dola wanaiona Teknolojia katika macho mawili, kama nyenzo ya kuwasaidia lakini pia kama adui. Ni vipi tutawasaidia kuweza kuiona kwa jicho moja kama sisi tunavyoiona?

Kuna kitu kingine ningependa tukikomeshe, nacho ni watu kujiona “Wakubwa”, kujiona wao ndio wana haki na wanaanza kuwagawia wengine, na sisi tunapaswa tuache kusubiri kupewa haki. Kila mmoja ana haki na anapaswa kuisimamia kwa nafasi yake.

Screenshot 2023-10-27 182438.png

Asha Abinallah (CEO Tech & Media Convergency): Mara zote tunapojadili masuala ya teknolojia utasikia “Tufanye nini?”

Mimi naamini sisi kama wana Azaki tuko katika nafasi ya kutoa suluhu na sio kuzisubiri kutoka nje. Kama unafanya kazi na vijana, basi fanya mabadiliko kupitia shughuli zako hizo hizo zinazogusa vijana. Mabadiliko yatafanywa na sisi wenyewe.

Screenshot 2023-10-27 182459.png

Anna Kulaya (WiLDAF): Tunapopambania Katiba Mpya, inabidi tujiulize tunataka nini. Kwa sababu hata katika katiba iliyopo masuala ya Haki za Binadamu yametajwa ila tujiulize yanazingatiwa?

Katiba haiwezi kuja kubadili tabia wala mienendo yetu. Katiba Mpya sio suluhisho la kila kitu.

Ndani ya miaka 30, tumefikia asilimia 10 pekee ya uwiano katika uongozi nchini kati ya wanawake na wanaume.

Hii inamaanisha ili kufika 50/50 itatuchukua miaka 150. Wito wangu ni tutumie Teknolojia ili kuweza kufikia hili kwa haraka kwani naamini inawezekana.

======

Topic: Tracking Information Disorder (Including Dis and Mis-Information) in the era of Technological Advancements.

Maxence Melo

Awali tulipoanza kufanya Uhakiki wa Taarifa (Fact-Checking) kupitia JamiiCheck tulitumia Artificial Intelligence (AI).

Baada ya muda tuliona kwamba si kwa mara zote AI inapatia kwa sababu AI inatumia taarifa zilizopo na tunajua kwamba upatikanaji wa Taarifa Mtandaoni hapa nchini unachukua muda.

Hivyo tulilazimika kufanya Ushirikiano wa Kimkakati na Taasisi na hata watu binafsi kuweza kupata ukweli wa taarifa mbalimbali.

JamiiCheck ndio jukwaa pekee Afrika linalofanya Uhakiki wa Taarifa (Fact-Checking) iliyo shirikishi kwa Wananchi. Yaani Wananchi ndio wanaweka Taarifa ili zifanyiwe uhakiki na pia wanaweza kushiriki katika mchakato wa kuhakiki kwa kuongezea taarifa au vithibitisho na hata kupingana na kilichowekwa na wenzao.

Screenshot 2023-10-27 181327.png

Dkt. Rose Reuben
Wanawake, Wasichana na Watoto wamekuwa wahanga sana wa Taarifa zisizo za kweli. Mara nyingi wanakutana na Taarifa wasizojua undani wake na kupatwa na shauku ya kuzisambaza.

Screenshot 2023-10-27 182013.png

Nuzulack Dausen (Nukta Africa)
Sisi kama Nukta Africa, haturuhusu maudhui yaliyotengenezwa kwa msaada wa Artificial Intelligence (AI) kwenda kwa Mlaji bila kupitiwa na Binadamu, kwasababu kuna suala la muktadha, Teknolojia hii (AI) haitambui muktadha. Kwenye matumizi ya Artificial Intelligence (AI) kuna changamoto ya Faragha (Privacy).

Unaweza ukawa unafanya makala ya uchunguzi ukaenda kuiingiza kwenye “Tool” ya AI bila kujua kwamba hizi tools zinaendeshwa na Wanadamu.

AI inaweza kusababisha kuvuja kwa Taarifa kabla ya wakati au hata ambazo hutaki zijulikane kabisa.

Baruani Mshale (Twaweza)
Hatuwezi tukafikia mahali ambapo tutaondoa sintofahamu kwa 100%. Hatuwezi kusubiri katika kuandaa Sera na Sheria za kusimamia Teknolojia mpya wakati maendeleo ya Kiteknolojia hayatusubiri. Tuendelee kutengeneza na kuboresha kadri tunavyoendelea kupata taarifa

Richard Mabala:
Ni ngumu sana kuwa na Vyombo vya Habari kuwa 'Neutral', hata Marekani na Ulaya vyombo haviko 'Neutral'.

Kujua chombo kina misimamo gani inasaidia anayesoma taarifa kujua 'uongo' unaoweza kuandikwa na chombo husika.

Maxence Melo (JamiiForums)
Wananchi wanachokifanya ni kutoa taarifa. Ni kazi ya Waandishi wa Habari kuchakata taarifa za Wananchi ili kuwa habari.

Tunachangamoto ya kuelewa Sera, Sheria na Kanuni. Ndio sababu Wananchi wanatumia nguvu kubwa kudai Sheria.

Sheria ipo kwa ajili ya kuwalinda watawala sio Wananchi. Amini usiamini, Online Content Regulation iliombwa na 'bloggers' na iliwaumiza wenyewe.

Sheria hazina faida sana kama Sera. Wakati mwingine sera inaandika kuwa tuna Sheria mbovu, lakini wanatunga sheria nyingine mbovu zaidi.

JamiiForums ni sehemu ya kupaza sauti za Wananchi. Sisi sio chombo cha Habari na hatuna upande wowote zaidi ya ule wa Wananchi.

Kama Wananchi wataamua “Kutuingiza chaka” basi tutaingia chaka kwa sababu lengo letu ni kuwapa wao #Uhuru wa Kujieleza katika kuboresha demokrasia.
 
Back
Top Bottom