Judge Mapigano is no more. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Judge Mapigano is no more.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by mayenga, Jan 17, 2011.

 1. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Aliyewahi kuwa Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania,na wakati mwingine akitumika kama Jaji wa mahakama ya rufaa Tanzania(Acting Justice of Appeal)Dan Petro Mapigano amefariki dunia tarehe 15 Jan.2011,Aga Khan Hospital.Mwili wa marehemu utaagwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana.Jaji Mapigano mpaka mauti yanamkuta alikuwa ni mmoja wa Mawakili katika Kampuni maarufu ya Uwakili ya FK Law Chambers iliyopo Sea View Dar es Salaam.

  Bwana alileta na Ametwaa!
   
 2. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  RIP Hon. Judge Map.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  RIP Hon. Judge Mapigano!
   
 4. T

  Taso JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  what legacy did he leave on the bench, if any
   
 5. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Innalillah, wayna illahy rajuun
   
 6. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Rip judge mapigano.
   
 7. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ukiona hivyo ujue nasi siku zetu zinakaribia. kama unmuaminimungu jitayarishe au namna gani vipi leave your life to the fullest

  RIP
   
 8. O

  Ogah JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Poleni sana wafiwa..........RIP Jaji Mapigano
   
 9. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Kujenga nyumba mpaka kwenye hifadhi ya barabara.
   
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,813
  Trophy Points: 280
  RIP Judge Mapigano
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  'Hukumu za Jaji Mapigano hazikuwa tata'


  Na Peter Mwenda

  JAJI Mstaafu Dan Mapigano (72) aliyefariki Jumamosi katika Hospitali ya Aga Khan alizikwa jana katika makaburi ya Kinondoni, Dar es salaam, huku akisifiwa kuwa kutoa hukumu zisizo na utata maisha yake yote.Umati wa
  waombelezaji waliofurika kuaga mwili wa marehemu katika Wiwanja vya Mnazi Mmoja wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Bw. Ali Hassan Mwinyi ilielezwa kuwa marehemu Jaji Mapigano wakati wa uhai wake hakuwahi kutoa hukumu yenye utata, jambo linalothibitisha uadilifu wake.

  Akitoa salamu za Chama cha Majaji Wastaafu, Mwenyekiti wa chama hicho, Jaji Thomas Mihayo alimweleza Jaji Mapigano kuwa hakuwa mwenye majivuno na kila mara alitoa ushauri kwa majaji wenzake na kuwaasa watende haki kabla ya kutoa hukumu.

  "Jaji Mapigano alikuwa safi lakini hakuingilika, alipostaafu hakuacha viporo vya hukumu na hukumu zake aliziandika kwa Kiingereza fasaha," alisema Jaji Mihayo.Alisema Jaji Mapigano hakuona ufahari wa cheo chake na alifarijika kukaa pamoja na wenzake lakini hakuwa tayari kuchangia hoja kabla ya kujua jambo linalozingumziwa.

  Alisema Jaji Mapigano hakuwahi kukisaliti kiapo chake alichokula cha kutenda haki katika kazi yake mpaka anakufa, hivyo atakumbukwa na wanasheria wengine nchini.

  Chama cha Wanasheria Tanzania Bara nacho kilisema Jaji Mapigano hakuwahi kutoa hukumu yenye utata na katika kipindi chote akiwa Jaji ni hukumu mbili tu zilizowahi kukatiwa rufaa.

  Hukumu hizo mbili zilizokatiwa rufani zilitolewa na jopo la majaji watatu akiwemo yeye, lakini hata hivyo hazikushinda.

  Katika salamu hizo, Profesa Florance Luoga wa F.K Chambers ambako marehemu alikuwa akifanya kazi ya Uanasheria baada ya kustaafu, qlimtaja kuwa alikuwa mdhibiti mkuu wa sheria katika kampuni hiyo.

  "Alipenda kesi zote zinazofika mbele yake, mhusika apate haki halali aliyopaswa kuipata na pengo hilo halitazibika mara moja.

  Katika kuaga mwili wa marehemu mawaziri Wakuu wastaafu, Jaji Joseph Warioba na Frederick Sumaye pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Bi. Celine Kombani walihudhuria. Pia walikuwapo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta na Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja.Majaji, wanasheria, mawakili na waombelezaji mengi waliaga mwili wa marehemu kabla ya kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni.

  Marehemu Jaji Mapigano alizaliwa mwaka 1939 katika kijiji cha Murangi, katika Wilaya ya Musoma na kusoma Shule ya Msingi Ikizu kabla ya kuchaguliwa kwenda Shule ya Sekondari Bwiru Boys mkoani Mwanza alipomaliza 1956.

  Alijiunga na kidato cha tano Tabora Boys alipohitimu mwaka 1959 na kujiunga Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda na kuhitimu shahada wa kwanza ya biashara kabla ya kuhamia masomo ya shahada ya sheria.Mwaka 1966 aliajiriwa na idara ya Mahakama kuwa Hakimu Mkazi na Mwaka 1974 aliapishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

  Marehemu alistaafu mwaka 1999 na kuanza kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari mwaka 2000 na Jumapili ya Januari 2, alipatwa na kiharusi na kukimbizwa hopitali ya Aga Khan ambako alilazwa chumba cha wagonjwa mahututi na kufariki Januari 15. Mungu ilaze roho ya marehemu mahali pema Pepon. Amen.

  [​IMG]
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  IT could have been more rewarding if these encomiums were made when he was still alive.......................but posthumous dirge sounds hypocritical
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  R.I.P. Mzee Mapigano.

  Steve Dii
   
Loading...