Tuacheni mizaha katika mambo nyeti kama haya. Yanayojalisha mstakabali wa taifa letu. Lema anahaki zote ya kuwazilisha hisia zake zote kwa namna yeyote ile ppopote pale anapopata nafasi hivyo. Tafadhali msimkejili, msifedhei, msimtweze, msimpige vijembe, msimkatishe tamaa, msimtukane, msimsulubishe, msiwaunge maadui zake mkono, msiache kumwombea muumba wake amjaaliye afya njema na fanaka tele n.k. Mambo yote hayo hapo juu tafadhali tuyaache yafanywe na vibaraka wa wawekezaji wa nchi za ughaibuni pamoja na mafisadi. Waungwana tuungane tuweke itikadi za kisias kando tulijenge taifa letu lililobomolewa na mafisadi, madhalani umeme shida, maji shida, madawa hospitalini shida, madaktari shida, elimu shida, waalimu shida,mfumko wa bei za bidhaa nyeti shida, misharahara ya wafanyakazi wa umma shida, ugumu wa maisha shida. Tunategemea nini katika hali kama hiyo waungwana, itabidi tuanze kufikiria kwa kichwa na wala si kwa tumbo, waungwana wenzangu!!! Mungu uibariki Tanganyika, Mungu uibariki Zanzibar. Inshala!!!