Joto kali Dar laibua mazito

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Dar es Salaam. Magonjwa ya ngozi, kupungukiwa maji mwilini na maumivu ya kichwa ni kadhia zitakazowakumba baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam kutokana na joto kali linalolikumba jiji hilo.

Tayari Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza kuwa hali ya hewa katika jiji hilo hadi jana lilikuwa limefikia nyuzi joto 35.

Meneja wa Huduma za Utabiri wa TMA, Samwel Mbuya jana alisema joto la mwaka huu limevunja rekodi kwani kwa kawaida, kipindi cha Januari linatakiwa liwe nyuzi joto 32.

Mbuya alisema joto hilo pia limeongezeka hata kwa upande wa Zanzibar ambako limefikia nyuzi joto 35 ikiwa ni ongezeko la asilimia mbili.

Alisema sababu kubwa ni kuongezeka kwa joto katika ukanda wa Bahari ya Hindi ambalo pia linatishia kuwapo kwa mvua za El-nino.

Alisema kadiri mvua zinavyochelewa, ndivyo joto la bahari linavyozidi kuongezeka na kusababisha hali iliyopo.

Madhara ya joto kiafya

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani ya mwili, Meshack Shimwela alisema kwa sasa wanapokea kesi nyingi za magonjwa ya ngozi kama upele, fangasi, kupungua maji mwilini na kuumwa kichwa.

Alisema joto kali linamfanya mtu apoteze wastani wa lita tatu za maji kwa siku. “Kwa watu wasiokunywa maji katika kipindi hiki wanaweza kukaukiwa maji, kwa sababu hawanywi vimiminika vya kutosha kujazia kiwango kile kilichopotea,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Nyuzi joto 35?? Duh!
Si ajabu nimejikuta nakunywa maji zaidi ya lita moja na nusu kwa siku!
 
Badala yake wanakata miti.
u!!

Tuanze kwa kutafuta nishati mbadala wa matumizi ya mkaa na kuni. Gesi ya kupikia ipunguzwe bei kwa kiasi kikubwa, umeme usambazwe vijijini, matumizi ya solar na biogas yahimizwe, small scale wind farms za kutengeneza umeme inawezekana kwa kila familia au mtaa...

Kila familia, mtaa, kijiji, kata, tarafa, wilaya na taifa tupeane targets za kupanda miti kila mwaka.

Mwanzo utakuwa mgumu ila mbeleni tutazoea na itakuwa tabia yetu..

Ni kwa faida yetu sote
 
Nimetokwa vipele kama mtoto mdogo. Naulizwa umepaka nini!! Au maji ya chumvi? Walaa... Kumbe joto....
Inyeshege tu hio mvua kha!
 
Hapo ndio nazidi kupata hasira na huenda labda nisije kukunyaga jiji la dar maisha yangu yote

Haiwezekani jiji lenyewe chafu,
Folene kila sehemu
Joto na hapo bado sijakutana na vibaka
Mbona watu wa dar mnahangaika sana na maisha
Jiji lenyewe limejengwa kama mchwa
 
Kama walivyoonya wataalam, hii huenda ikapika mvua ya hatari itakayoleta maafa. Sasa sijui tunajiandaaje kukabiliana na hiyo hali ki miundombinu na kupunguza athari.
 
Yani Kama ulikuwa umekaa ndani kwenye kipupwe ukitoka tu unalisikia wimbi la joto.... Daladala zilivyojazana hata likimbieje husikii Upepo... Sijui huko Khartoum wanaishije
 
Poleni sana kweli naona kiwango cha juu cha Joto ni nyuzi joto 32 kwa Dar. Ila cha ajabu sisi mwanza toka asubuhi ni mvua mpaka sasa.... Kama Picha zinavyoonesha hapo chini.
ImageUploadedByJamiiForums1452776955.974328.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1452776993.123258.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom