Joto kali Dar laibua mazito

Joto kali Dar laibua mazito

Dar es Salaam. Magonjwa ya ngozi, kupungukiwa maji mwilini na maumivu ya kichwa ni kadhia zitakazowakumba baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam kutokana na joto kali linalolikumba jiji hilo.

Tayari Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza kuwa hali ya hewa katika jiji hilo hadi jana lilikuwa limefikia nyuzi joto 35.

Meneja wa Huduma za Utabiri wa TMA, Samwel Mbuya jana alisema joto la mwaka huu limevunja rekodi kwani kwa kawaida, kipindi cha Januari linatakiwa liwe nyuzi joto 32.

Mbuya alisema joto hilo pia limeongezeka hata kwa upande wa Zanzibar ambako limefikia nyuzi joto 35 ikiwa ni ongezeko la asilimia mbili.

Alisema sababu kubwa ni kuongezeka kwa joto katika ukanda wa Bahari ya Hindi ambalo pia linatishia kuwapo kwa mvua za El-nino.

Alisema kadiri mvua zinavyochelewa, ndivyo joto la bahari linavyozidi kuongezeka na kusababisha hali iliyopo.

Madhara ya joto kiafya

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani ya mwili, Meshack Shimwela alisema kwa sasa wanapokea kesi nyingi za magonjwa ya ngozi kama upele, fangasi, kupungua maji mwilini na kuumwa kichwa.

Alisema joto kali linamfanya mtu apoteze wastani wa lita tatu za maji kwa siku. “Kwa watu wasiokunywa maji katika kipindi hiki wanaweza kukaukiwa maji, kwa sababu hawanywi vimiminika vya kutosha kujazia kiwango kile kilichopotea,” alisema.

Chanzo: Mwananchi

Pamoja Na Hii TAARIFA Yako Mkuu Ila Huwezi Amini Kuna Baadhi Ya Watu Wazima Tu Kuoga Kwao Mpaka WASHIKIWE BAKORA Lasivyo Akiogoa Leo Ni Mpaka Kesho Kutwa Hiyo.
 
Sio Dar tu! Nahisi ni ukanda wote wa pwani, maana hata Lindi na Mtwara hali ni mbaya sana.
 
nasikia kuna mji huko oman kitu kinafikia 60 degree Celsius

Kuna documentary moja nilikuwa naangalia sasa hivi wanasema Qatar mwezi june na july joto linafika hadi nyuzi joto 50. Nimeogopa.
 
Kuna documentary moja nilikuwa naangalia sasa hivi wanasema Qatar mwezi june na july joto linafika hadi nyuzi joto 50. Nimeogopa.
Tofauti ya wale jamaa na sisi ni kwamba Qatar mpaka kwenye vituo vya mabasi kuna Air condition na karibia kila sehemu Ina ACs. Hapa kwetu Joto linatutesa sana hasa sisi walala hoi tusioweza gharama za Air Cons.
 
..Pia joto kali hupunguza nguvu za kiume. Je, vijana wa mjini mnalifahamu hilo???
 
Hapo ndio nazidi kupata hasira na huenda labda nisije kukunyaga jiji la dar maisha yangu yote

Haiwezekani jiji lenyewe chafu,
Folene kila sehemu
Joto na hapo bado sijakutana na vibaka
Mbona watu wa dar mnahangaika sana na maisha
Jiji lenyewe limejengwa kama mchwa

We waache waendelee kubanana hivyo hivyo..wakati huku Kanda ya ziwa(Roc city) hali ya hewa utafikiri Norway..:lol:
 
Back
Top Bottom