Joto kali Dar laibua mazito

Joto kali Dar laibua mazito

Kama walivyoonya wataalam, hii huenda ikapika mvua ya hatari itakayoleta maafa. Sasa sijui tunajiandaaje kukabiliana na hiyo hali ki miundombinu na kupunguza athari.
Na hivi na nyumba mnabomolewa aiseee Mungu awape wepesi jamani.
 
Mkuu ciprofloxacin, gentrisone ina steroid, itamchubua, tena na joto hili kali.. Itakuwa balaa. Ni bora atafute Zincast babby cream®. Huondoa vipele vya joto mwilini.It is special formulated kwa watoto, but hata mtu mzima anaweza tumia na ikamsaidia.
 
Dar es Salaam. Magonjwa ya ngozi, kupungukiwa maji mwilini na maumivu ya kichwa ni kadhia zitakazowakumba baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam kutokana na joto kali linalolikumba jiji hilo.

Tayari Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza kuwa hali ya hewa katika jiji hilo hadi jana lilikuwa limefikia nyuzi joto 35.

Meneja wa Huduma za Utabiri wa TMA, Samwel Mbuya jana alisema joto la mwaka huu limevunja rekodi kwani kwa kawaida, kipindi cha Januari linatakiwa liwe nyuzi joto 32.

Mbuya alisema joto hilo pia limeongezeka hata kwa upande wa Zanzibar ambako limefikia nyuzi joto 35 ikiwa ni ongezeko la asilimia mbili.

Alisema sababu kubwa ni kuongezeka kwa joto katika ukanda wa Bahari ya Hindi ambalo pia linatishia kuwapo kwa mvua za El-nino.

Alisema kadiri mvua zinavyochelewa, ndivyo joto la bahari linavyozidi kuongezeka na kusababisha hali iliyopo.

Madhara ya joto kiafya

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani ya mwili, Meshack Shimwela alisema kwa sasa wanapokea kesi nyingi za magonjwa ya ngozi kama upele, fangasi, kupungua maji mwilini na kuumwa kichwa.

Alisema joto kali linamfanya mtu apoteze wastani wa lita tatu za maji kwa siku. “Kwa watu wasiokunywa maji katika kipindi hiki wanaweza kukaukiwa maji, kwa sababu hawanywi vimiminika vya kutosha kujazia kiwango kile kilichopotea,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
Mkuu Figganigga,
Nimejaribu kutafuta hayo mazito yaliyoibuliwa na joto kwenye habari yako sijayaona. Au haya mazito ya kutulaza uchi watu wazima nyakati za usiku!!?? Maana haya ni mazito haswaaa!
 
Binadamu tulipewa akili ya kutawala mazingira wenzetu wazungu wameweza ila sisi Waafrika bado, tuna njia ndefu mno
 
Kila kitu kinapozidi kwa sisi Binaadam kwa kweli ni mtihani
 
Pamoja Na Hii TAARIFA Yako Mkuu Ila Huwezi Amini Kuna Baadhi Ya Watu Wazima Tu Kuoga Kwao Mpaka WASHIKIWE BAKORA Lasivyo Akiogoa Leo Ni Mpaka Kesho Kutwa Hiyo.
Hiyo avatar yako ni wewe mwenyewe au baba yako? maana imefanana sana na muuaji mmoja wa Rwanda aliyehusika na mauaji ya kimbari.
 
Kweli joto limezidi. Daaa chini ya manyonyo kumechubuka, mapajani kumechubuka hali ni hovyo.
Poooole mndenyi! inabidi sasa jiachie nor kuvaa skin tight neither brazier kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi
 
Dar es Salaam. Magonjwa ya ngozi, kupungukiwa maji mwilini na maumivu ya kichwa ni kadhia zitakazowakumba baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam kutokana na joto kali linalolikumba jiji hilo.

Tayari Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza kuwa hali ya hewa katika jiji hilo hadi jana lilikuwa limefikia nyuzi joto 35.

Meneja wa Huduma za Utabiri wa TMA, Samwel Mbuya jana alisema joto la mwaka huu limevunja rekodi kwani kwa kawaida, kipindi cha Januari linatakiwa liwe nyuzi joto 32.

Mbuya alisema joto hilo pia limeongezeka hata kwa upande wa Zanzibar ambako limefikia nyuzi joto 35 ikiwa ni ongezeko la asilimia mbili.

Alisema sababu kubwa ni kuongezeka kwa joto katika ukanda wa Bahari ya Hindi ambalo pia linatishia kuwapo kwa mvua za El-nino.

Alisema kadiri mvua zinavyochelewa, ndivyo joto la bahari linavyozidi kuongezeka na kusababisha hali iliyopo.

Madhara ya joto kiafya

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani ya mwili, Meshack Shimwela alisema kwa sasa wanapokea kesi nyingi za magonjwa ya ngozi kama upele, fangasi, kupungua maji mwilini na kuumwa kichwa.

Alisema joto kali linamfanya mtu apoteze wastani wa lita tatu za maji kwa siku. “Kwa watu wasiokunywa maji katika kipindi hiki wanaweza kukaukiwa maji, kwa sababu hawanywi vimiminika vya kutosha kujazia kiwango kile kilichopotea,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
Joto limeongezeka kiasi kwamba kwenye daladala duuh nishida!! Watu wanajazana harufu kali dah sijui kama itaongezeka hali itaendelea kuwaje
 
Kupungua kwa maji mwilini kwa joto na kutokwa jasho pia huambatana na kupungua kwa Chumvi mwilini,ni vizuri kunywa vinywaji kama Pocari sweat au kuzidisha chumvi kiasi katika chakula, mwenye kujua zaidi hili la kupungukiwa chumvi atujuze zaidi
 
Joto limeongezeka kiasi kwamba kwenye daladala duuh nishida!! Watu wanajazana harufu kali dah sijui kama itaongezeka hali itaendelea kuwaje
Usiku kwa Dar feni inapuliza upepo wenye joto, ni shida tupu!
 
Hiyo avatar yako ni wewe mwenyewe au baba yako? maana imefanana sana na muuaji mmoja wa Rwanda aliyehusika na mauaji ya kimbari.

Huyo Umwonae Ktk AVATAR Hapo Juu Ndiyo GENTAMYCINE Mwenyewe Mkuu Ila Hayo Mambo Yako Ya Rwanda Na Mauaji Ya Kimbari Unayajua Wewe Uliyeshiriki.
 
Back
Top Bottom