Joto kali Dar laibua mazito

Joto kali Dar laibua mazito


Huyo Umwonae Ktk AVATAR Hapo Juu Ndiyo GENTAMYCINE Mwenyewe Mkuu Ila Hayo Mambo Yako Ya Rwanda Na Mauaji Ya Kimbari Unayajua Wewe Uliyeshiriki.
Duh! mkuu mbona sura haieleweki kama wewe ni kijana au mzee? Una undugu na Humphrey Polepole? wana ccm bana mna sura zenu zimekaa ki dazaini dizaini tu aisee, duh! sijui kwa sababu ya ufisadi wenu uliotukuka hadi mnakuwa na sura zenu special.
 
I
Duh! mkuu mbona sura haieleweki kama wewe ni kijana au mzee? Una undugu na Humphrey Polepole? wana ccm bana mna sura zenu zimekaa ki dazaini dizaini tu aisee, duh! sijui kwa sababu ya ufisadi wenu uliotukuka hadi mnakuwa na sura zenu special.
Umemaliza Kila kitu boss wangu, viva UKAWA
 
Hayo ni magonjwa ya haraka haraka lakini kubwa zaidi naona watu wanatwanga soda kiwango kisicho na idadi kujaribu kutuliza kiu, hapo naona tunatengeneza majanga mengine siku za usoni.
yani hilo ni moja ya janga kubwa zaidi litakalotokea mbeleni
 
H
Dar es Salaam. Magonjwa ya ngozi, kupungukiwa maji mwilini na maumivu ya kichwa ni kadhia zitakazowakumba baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam kutokana na joto kali linalolikumba jiji hilo.

Tayari Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza kuwa hali ya hewa katika jiji hilo hadi jana lilikuwa limefikia nyuzi joto 35.

Meneja wa Huduma za Utabiri wa TMA, Samwel Mbuya jana alisema joto la mwaka huu limevunja rekodi kwani kwa kawaida, kipindi cha Januari linatakiwa liwe nyuzi joto 32.

Mbuya alisema joto hilo pia limeongezeka hata kwa upande wa Zanzibar ambako limefikia nyuzi joto 35 ikiwa ni ongezeko la asilimia mbili.

Alisema sababu kubwa ni kuongezeka kwa joto katika ukanda wa Bahari ya Hindi ambalo pia linatishia kuwapo kwa mvua za El-nino.

Alisema kadiri mvua zinavyochelewa, ndivyo joto la bahari linavyozidi kuongezeka na kusababisha hali iliyopo.

Madhara ya joto kiafya

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani ya mwili, Meshack Shimwela alisema kwa sasa wanapokea kesi nyingi za magonjwa ya ngozi kama upele, fangasi, kupungua maji mwilini na kuumwa kichwa.

Alisema joto kali linamfanya mtu apoteze wastani wa lita tatu za maji kwa siku. “Kwa watu wasiokunywa maji katika kipindi hiki wanaweza kukaukiwa maji, kwa sababu hawanywi vimiminika vya kutosha kujazia kiwango kile kilichopotea,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
Hali ya hewa wamechelewa kusema kuwa kuna heatwave
 
Kati ya Jua na Mvua Bora Nini?

Kati ya baridi na Joto Bora nini?
 
Back
Top Bottom