POLISI mkoani Arusha jana lilimhoji Mbunge waArumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari kwa zaidi ya saa saba baada yakujisalimisha katika Kituo Kikuu cha jeshi hilo.
Nassari ambaye anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Serikali katikamkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika Mei 5, mwaka huu katika Uwanja chaNMC, alishikiliwa kituoni hapo kuanzia 6:12 mchana hadi saa 12 jioni kishakuruhusiwa kuondoka na kutakiwa kuripoti kituoni hapo leo.
Alifika hapo akiwa na Wakili wake, Arbert Msando bila ya kuwakuta viongozi wajeshi hilo hivyo wakaamua kuondoka.
Lakini nusu sasa baadaye, Naibu Kamishna, Isaya Mungulu na Kaimu Kamanda waPolisi Mkoa wa Arusha, Akilimali Mpwapwa walifika na kuwataka viongozi waChadema, waliokuwa kituoni hapo kuwasiliana na Nassari ili arejee.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbless Lema aliyekuwapo aliwasiliana naNassari ambaye alirejea saa 7:20 akiwa na Wakili Msando na alichukuliwa naKamanda Mpwapwa ambaye alimwelekeza kuelekea Ofisi ya Mkuu wa
Upelelezi Mkoa (RCO) kwa mahojiano.
Baada ya kumfikisha Mbunge huyo katika ofisi za mahojiano, Kamanda Mpwapwaalisema kulingana na uzito wa shauri lake atalazimika kutafuta watu wa kumwekeadhamana mara baada ya kuhojiwa.
Hapa yupo mikononi mwa polisi, atahojiwa na baadaye atapewa dhamana, alisemaMpwapwa.
Kamishna Msaidizi wa Polisi, Salum Msangi kutoka Makao Makuu ya Idaya yaUpelelezi wa Makosa ya Jinai (CID), ndiye alikuwa akiongoza kikosi maalumukilichokuwa kikimhoji Nassari.
Msangi ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa mpya waSimiyu, alikuwa akisaidiana na Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Hamisi Wariobakutoka ofisi ya upelelezi Mkoa wa Arusha.
ASP Warioba ndiye aliyewahoji watuhumiwa wengine, John Heche na Ally Banangajuzi kwa zaidi ya saa tisa kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku,walipoachiwa kwa dhamana na kutakiwa kurejea jana asubuhi.
Awali, Nassari alieleza alikuwa hana taarifa za kuitwa polisi kwa shtaka lolotebali, mara baada ya mkutano huo wa Mei 5, alipokea ujumbe wa simu kutoka OfisaUpelelezi Mkoa wa Arusha, Faustine Mafwere kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha,Thobias Andengenye alikuwa anamtafuta ili waagane baada ya kuhamishiwa makaomakuu.
Mimi nimeshangaa leo kusoma katika vyombo vya habari kuwa nasakwa na polisi nandiyo sababu nimekuja kwani awali, nilijua rafiki yangu Andengenye anatakatuagane na nilipanga siku nyingine, alisema Nassari.
Nassari pamoja na viongozi wengine wa Chadema wanatuhumiwa kutoa kaulimbalimbali za uchochezi ikiwamo, kutishia kujitangazia uhuru wa
Arusha na kanda ya ziwa kama polisi haitawakamata waliohusika na mauaji yamwenyekiti wa chama hicho Kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo.
Pia alimtuhumu mtoto wa Rais, Ridhiwan Kikwete kushinikiza uteuzi wa baadhi yaviongozi serikalini.
Bananga ambaye pamoja na Heche pia walikuwa wakisubiri kuhojiwa zaidi janaalisema juzi aliulizwa juu ya kauli zao kwenye mkutano huo, dhidi ya RaisKikwete na mtoto wake Ridhiwan. Huku Heche akisema kwamba aliulizwa juu kauliza Nassari katika mkutano huo.