Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,302
- 33,754
Uongozi si akili au uwezo wa kuzungumza mtu, kuna vitu vingi vinavyoweza kumpamba au kumbomoa kiongozi.
Vitu hivyo ndivyo vyenye nguvu ya ushawishi. Moja ya kitu hicho ni 'Charisma'- compelling attractiveness or charm that
can inspire devotion in others' ikimaanisha mvuto wenye ushawishi kwa wengine.
Mh Nasari kwa umri wake na CV yake kuwa katika hadhi aliyo nayo ni wazi ana Charisma ya aina fulani.
Charisma hiyo ndiyo inampatia wafuasi waliojitoa(devotion) kwa ajili yake. Hawa watamsikiliza kwa kila jambo na baadhi yao wataziweka fikra zao rehani ili mradi tu kumsikiliza na kumtii kiongozi wao kwa heri au kwa shari.
Hoja ya udogo wa umri na akili haina mantiki hasa tukijua uwezo wake wa kushawishi wana Arumeru kumchagua, pamoja hadhi anaopewa bungeni kama alivyo mzee Samuel Sitta n.k.
Nasari si mbunge mtoto au kijana ni mbunge na kwa taratibu za nchi yetu ni kiongozi wa umma katika hadhi ile ile ya mbunge mwingine. Ni ujuha kudhani kuwa hoja zake zinatapewa hadhi ya utoto.
Tuache ushabiki na tuangalie ukweli. Kauli aliyotoa inamtia yeye mwenyewe doa, CDM na wanananchi anaowawakilisha.
Leo hii akitokea kiongozi kupopolewa mawe au kudhurika kwa namna yoyote kule Arumeru Nasari hatakwepa tuhuma.
Huu ni ukweli hata kama watu hawaukubali. Ni kauli aliyoitoa ima kwa kutojua au kwa bahati mbaya lakini ina madhara
Ukiachilia mbali kauli yake, Nasari anakijengea chama taswira ile ile inayopigwa vita au kushadidiwa na watu kuhusu Ukanda. Ndiyo maana mwenyekiti Mbowe hakusubiri kuikana.
Busara zinasema kuwa, na nimewahi kuandika, ilibidi Nasari aitishe mkutano wa vyombo vya habari na kusema samahani.
Mwendelezo wa malumbano haukitendei chama chake haki na unazidi kutia shaka juu yake na uwakilishi wake.
CDM walipaswa kumshinikiza aombe radhi kama sehemu ya kumlea. Nashangaa anaendelea kutoa kauli tata, hili linammaliza kisiasa na kukiumiza chama chake.
Jambo la kushangaza ni kuwa yapo mengi ya kuongelea katika mikutano, kauli zenye utata ni uchanga wa kisiasa au ukosefu wa malezi ya kisiasa.
Nasari wewe ni kiongozi wa taifa na siku zote fikra na kauli zako zilenge kuleta utangamano kitaifa.
Wewe ni kiongozi kauli zako ni tofauti na kauli za Nasari wa mwaka 2010.
Tumia ushawishi wako, karama na haiba yako katika kufikiria namna ya kuwakomboa Watanzania kutoka katika lindi lenye kina kirefu la umasikini.
Nasari, wewe bado ni mchanga kisiasa, jitokeze na useme neno moja 'Samahani'. Samahani si neno la udhaifu ni dalili ya kukua kifikra, busara na utimilifu wa hekima.
Hiki ni kidonda utakachoishi nacho, dawa si kukifunika ni kukitafutia dawa.
Mdogo wangu dawa ni moja tu na unayo, ulimi wako na kinywa chako