NADHARIA Joseph Kabila siyo mtoto halisi wa Hayati Laurent Desire Kabila, na ana asili ya Rwanda

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Rais Mstaafu Joseph Kabila inasemekana hakuwa mtoto halisi(Biological Son) wa Rais Mstaafu Joseph Desire Kabila. Inasemekana jina halisi la Joseph Kabila ni Hypolite Kanambe Kazemberembe akiwa na asili ya Kitusi kutoka nchi ya Rwanda.

kabila_adresse_18_003_jpg_711_473_1.jpeg
Pamoja na machapisho mengi kumtambua Joseph Kabila kama mtoto halisi (Biological son) wa Hayati Joseph Desire Kabila, baadhi ya machapisho yamehabarisha kuwa baba mzazi wa Joseph Kabila Kabange anajulikana kama Christopher Kanambe Kazemberembe na mama yake akiitwa Marcellina Mukambukuje.

Maswali ambayo wakongo wengi wanajiuliza, ilikuwaje wakatawaliwa na Rais aliyezaliwa Rwanda na mwenye asili ya Kitusi kutoka Rwanda huku Moise Katumbi aliyezaliwa Congo DR na Mama Mkongo na Baba Mgiriki akiwekewa vikwazo na mamlaka kugombea urais!

Kabila.png

Rais Laurent Kabila akisalimiana na Joseph Kabila aliyevaa nguo za kijeshi

Kanambe.jpg

 
Tunachokijua
Kiongozi wa kisiasa wa Kongo (Kinshasa) anayejulikana pia kama Joseph Kabila Kabange, alizaliwa Juni 4, 1971, mtoto wa mwanamapinduzi na Rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC; Zaire ya zamani), Laurent-Désiré Kabila.

Alizaliwa katika kijiji cha Hewa Bora II katika eneo la mbali la Fizi nchini DRC, ambapo baba yake aliongoza vuguvugu dogo la waasi dhidi ya udikteta wa Mobutu Sese Seko.

Kwa kuwa baba yake alitengwa sana mwanzoni mwa miaka ya 1970, vyanzo vichache vilikuwepo kuhusu utoto wa Kabila, ikizingatiwa kwamba alikuwa mtoto wa Laurent Kabila na kwamba alikuwa na familia kubwa. Ndugu zake Kabila ni pamoja na Josephine, Cecile, Zoe, Fifi, Selemani, Jaynet, Anina, na Tetia.

Elimu na Madaraka
Alipata elimu yake ya awali kwenye shule za umma huko Fizi, Kivu Kusini. Alimaliza shule ya msingi Dar es Salaam, Tanzania, na shule ya sekondari Mbeya, pia Tanzania.

Alikuwa akijua vizuri Kiswahili kuliko Kilingala ambayo ni lugha inayozungumzwa katika mji mkuu wa Kongo. Akiwa shuleni pia alisoma Kifaransa. Baada ya shule alipata mafunzo ya kijeshi nchini Rwanda kwa miaka mitatu kabla ya kuendelea na masomo.

Alianza masomo katika Chuo Kikuu cha Makerere mwaka 1995. Ilipofika mwaka 1996, baba yake Kabila, mkuu wa kikosi cha msituni kilichopinga Serikali wakati huo, alimwomba ajiunge naye katika vita vya kumpindua Rais wa wakati huo Mobutu Sese Seko.

Alipelekwa China kuendeleza mafunzo yake ya kijeshi, na miezi sita baadae waliongoza uasi uliopindua serikali ya Kongo na kumweka Laurent Kabila kwenye ofisi ya Rais. Aliteuliwa kwenye nafasi ya meja jenerali na akawekwa kuwa msimamizi wa jeshi.

Mwaka 1998, akiwa bado anaongoza majeshi, Kabila aliongoza vita dhidi ya Rwanda na Uganda, ambazo zote ziliivamia Kongo na kuwa na udhibiti wa sehemu zake. Operesheni hiyo ilikuwa bado inaendelea wakati Kabila aliporejea nyumbani. Kwa wakati huu Kabila aliishi katika kitengo cha makazi ya kijeshi na mpenzi wake Olive, na binti yao, Josephine, lakini maisha haya hayakudumu.

Baba yake Kabila aliuawa na mmoja wa walinzi wake, Rashisi Kasereka, mwaka wa 2001. Kasereka aliuawa kwa kupigwa risasi papo hapo baada ya mauaji hayo.

Baada ya baba yake Kabila kufariki, mama Kabila aliendelea kuishi kwenye jumba hilo, mbali na macho ya watu. Na Kabila mwenyewe akawa Rais wa Kongo akiwa na umri mdogo wa miaka 29.

Aliachia urais Januari 24, 2019, na kukabidhi madaraka kwa Félix Tshisekedi, mabadiliko ya kwanza ya amani ya mamlaka nchini Kongo tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1960.

Asili ya Joseph Kabila
Mama yake Joseph Kabila alikuwa Sifa Mahayana, ambaye baadhi ya watu wamedai alikuwa na asili ya Rwanda badala ya Kongo, na jina lake halisi lilikuwa Marcellina Mukambukuje. Pia, inadaiwa kuwa alipokuwa Tanzania kimasomo, Joseph Kabila alitumia jina la Hippolyte Kanambe Kazemberembe kwa sababu za kiusalama.

Aidha, baba yake hakuwa Laurent-Désiré Kabila, bali alifahamika kwa jina la Christopher Kanambe. Kazemberembe

Tovuti ya Karisimbi Trumpeters linaweka mkazo kwenye madai haya kwa kufafanua kiundani asili ya Joseph Kabila. Sehemu ya madai hayo ni;

"Joseph Kabila, ambaye jina lake halisi ni Hyppolite Kanambe Kazemberembe, alizaliwa Juni 4, 1971, na baba wa Rwanda aitwaye Christopher Kanambe na mama wa Rwanda Marcelline Mukambukuje. Baba yake alikuwa mpinzani wa Rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana. Alikutana na Laurent Désiré Kabila, mpinzani wa Rais wa zamani wa Zaire Mobutu, katika vuguvugu la upinzani lililoko milimani kwenye mpaka wa Rwanda-Zaire, ambapo walipigana dhidi ya maadui wao wa kawaida: Mobotu na Habyarimana."

kanambe-jpg.2692803

Joseph Kabila au Hyppolite Kanambe Kazemberembe (Kushoto) akiwa na baba yae anayedaiwa kuwa na jina la Christopher Kanambe (Kulia)

Madai haya yaliwahi pia kuchapishwa hapa JamiiForums, Machi 26, 2012 yakiwa na kichwa cha habari “Ijue Familia ya Kabila Katika Picha” ambapo pamoja na mambo mengine mwandishi alitoa dokezo la asili na majina halisi ya Joseph Kabila kama yalivyobainishwa awali.

Tovuti ya Congovox katika nyakati tofauti limewahi pia kuchapisha makala inayofafanua asili ya Joseph Kabila kuwa ni Rwanda.

Tovuti hii imeenda mbele zaidi kwa kibainisha kuwa Laurent Kabila alimuua rafiki yake Christopher Kanambe, baba mzazi wa baba yake Hyppolite kutokana na kusalitiana kwenye masuala ya kivita kisha kumuoa mjane wa Marehemu ambaye tayari alikuwa na watoto, akiwemo Hyppolite.

Huo ndio ukawa mwanzo wa kubadilika kwa majina kutoka kuitwa Hyppolite Christopher Kanambe hadi kuitwa Joseph Kabila.

Taarifa hizi kwa ujumla wake hazipatikani kwenye vyanzo vya kuaminika.

Taarifa rasmi zinamtambua kama Joseph Kabila Kabange, mzaliwa wa kijiji cha Hewa Bora II katika eneo la mbali la Fizi nchini DRC pia mtoto wa mwanamapinduzi na Rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC; Zaire ya zamani), Laurent-Désiré Kabila.

Aidha, hii haiondoi uvumi unaotilia mashaka asili yake, ni mjadala wa wazi ambao JamiiForums inauchukulia kama nadharia.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom