Joram kiango vs Willy Gamba

Joram kiango vs Willy Gamba

Hao ndo walikuwa waandishi miak hiyo.
Nimewasoma wote
J.kiango ana mahali pake na Ben Musiba ana nafasi yake.
So wote wana nyota tano kwangu.
 
Bongo movie wangekuwaga seriouz wangemtengeneza wily gamba ambaye ni real kama jason bourne na james bond wa hollywood
 
Hao ndo walikuwa waandishi miak hiyo.
Nimewasoma wote
J.kiango ana mahali pake na Ben Musiba ana nafasi yake.
So wote wana nyota tano kwangu.
Nataman sana kupata historia zao hao watu ni yupi alianza kaz ya uandishi na kama walishasoma pamoja au vipi
 
Nimesoma vitabu vya Elvis Musiba na Ben Mtobwa, wote ni mafundi sana wa kuandika riwaya tamu za kipelelezi kupitia wahusika wakuu Willy Gamba na Joram Kiango.

Kwangu Mimi Ben Mtobwa ndiye Role Model wangu Kwa namna ya uandishi wake. Jamaa alikuwa fundi wa kuchanganya maneno Kwa namna tamu inayomfanya msomaji ainjoi sana.

Kwangu Ben ni kipaji cha kuandika ambacho TZ kiliwahi kutokea. Kasome kitabu chake cha 'Dar es salaam usiku' (sio Cha kipelelezi) utaona alivyotumia mtindo wa Flashback. Utaona alivyo gwiji wa kuandika.

Au kasome 'Malaika wa Shetani' uone jamaa alivyo fundi wa kuandika. Ben Mtobwa kwangu ndiye mwandishi mwenye ladha katika maandishi yake.

Kama angepatikana katika kizazi hichi cha Sasa nadhani jamii yote ingemwadhimisha Kwa maandiko yake.
 
Gamba shughuli nyingine Joram Kiango anajitahidi kama kina Edd Ganzel,Hamie Rajabu nk
 
Nataman sana kupata historia zao hao watu ni yupi alianza kaz ya uandishi na kama walishasoma pamoja au vipi
Sidhani kama Ben Mtobwa na A. E. Musiba walisoma pamoja. Ninachokumbuka Musiba aliwahi kuajiriwa serikalini (kama sikosei alikuwa mhasibu) na huko kwenye ajira akapata kesi iliyompelekea kufungwa na mara baada ya kutoka gerezani ndipo akatoa riwaya yake ya kwanza ya KUFA NA KUPONA. Hiyo ilikuwa kwenye late 1970s.
 
Hao ndo walikuwa waandishi miak hiyo.
Nimewasoma wote
J.kiango ana mahali pake na Ben Musiba ana nafasi yake.
So wote wana nyota tano kwangu.
Ben R. Mtobwa na A. E. Musiba ndiyo walikuwa waandishi. Mtobwa akimtumia Joram Kiango kama mhusika mkuu kwenye riwaya zake na Musiba akimtumia Willy Gamba. Hakukuwa na mwandishi anaeitwa Ben Musiba.
 
Sidhani kama Ben Mtobwa na A. E. Musiba walisoma pamoja. Ninachokumbuka Musiba aliwahi kuajiriwa serikalini (kama sikosei alikuwa mhasibu) na huko kwenye ajira akapata kesi iliyompelekea kufungwa na mara baada ya kutoka gerezani ndipo akatoa riwaya yake ya kwanza ya KUFA NA KUPONA. Hiyo ilikuwa kwenye late 1970s.
Anha kumbe
 
Nimesoma vitabu vyote vya Aristablus Elvis Musiba vyenye story za Willy Gamba na pia nimesoma sehemu kubwa ya vitabu vya James Hadley Chase lakini sikumbuki kuona popote ambapo mtu unaweza kusema Musiba alikopi kutoka kitabu hiki cha James Hadley Chase. Labda staili ya uandishi.
mimi ni muandishi kwa professional. kuna kitu inaitwa advaced plagiarism...kutokana na technology ilivyo technically mtu aliesoma ABC za Uandishi anaweza akacopy kazi ya mtu yeyote kisha akaiwasilisha kwa hadhira kwa kubadili maudhui.

bila hadhira kushituka haswa ukizingatia kuwa ni kosa kubwa kufanya plagiarism {kuwasirisha kazi ya mtu mwingine ukijifanya wewe ndie mmiliki bila ridhaa ya mmiliki halali.}

hivyo waandishi nguli walikuwa wanaweza kusoma kitu na kukielewa kisha wanaunda kazi zao kupitia makosa waliyo yaona kwenye kazi walio ipenda...​
 
Back
Top Bottom