Joram kiango vs Willy Gamba

Joram kiango vs Willy Gamba

Tutarudi na roho zetu?

Joram Kiango aliupiga mwingi. Namna alivyokua anatoroka sehemu tata ilikua poa sana. Lakini pia ukisoma kile kitabu, utaona mwandishi aliyaona mambo ya artificial intelligence miaka mingi kabla hata hayajafikiwa kiuhalisia.

I go for Joram Kiango. Mchizi alikua loyal sana kwa mademu zake!
01.jpg
 
Chase hajawahi kuwa na riwaya za state sponsored espionage kama Njama. Amnazo zilikuwa typical Musiba style.

Bora hata ungesema Musiba kamgeza Ian Fleming na James Bond.

But this is genre.

Ni sawa na kusema Justin Kalikawe kamgeza Bob Markey kuimbabreggae, wakati Justin aliimba reggae katika muktadha wa Kitanzania, akielezea mambobya Tanzania, kwa Kiswahiki, na hata Kihaya.

Unaweza kusema Musiba alikuwa inspired na Ian Fleming, au Justin Kalikawe alikuwa inspired na Bob Markey.

Lakini kuwa inspired si kugeza, na katika sanaa, inspiration inapatikana popote pale.
Sahihi kabisa.
 
Tutarudi na roho zetu?

Joram Kiango aliupiga mwingi. Namna alivyokua anatoroka sehemu tata ilikua poa sana. Lakini pia ukisoma kile kitabu, utaona mwandishi aliyaona mambo ya artificial intelligence miaka mingi kabla hata hayajafikiwa kiuhalisia.

I go for Joram Kiango. Mchizi alikua loyal sana kwa mademu zake!
Kabisa waliopata kusoma kipindi hicho nafikiri kwao hayo mambo ya AI yalikuwa ni ya kufikirika zaida
 
Benny R Mtobwa na muhusika wake Joram Kiango kwenye simulizi kitabu cha kuitwa Malaika wa Shetani
Ni simulizi bora kabisa kwangu kuisoma, na nnakitafuta saaaana hiko kitabu nlishaenda enzi zile ubungo kuuliza waaaapi, nikaenda kisutu pale nyuma ya peacock Hotel nikakikosa pia, baadae hii simulizi nikaja kuifananisha na mkasa wa JK na Lowasa

Simulizi nyingine bora kabisa kuipitia ni ya Hussein Tuwa na simulizi ya Kina Badi Gobos na wenzie
Pia ile ya Utata wa 9/12
 
Habari za Januari wakuu,

Kwa wapenzi wa riwaya za kiswahili nafikiri mtakuwa mmeshawa fahamu wahusika hapo juu mmoja anatumika na mwandishi Mtobwa B.R na Mwingine Musiba A.E.

Karibuni tuambiane yupi kati ya hao anakukosha sana hasa katika harakati zao za upelelezi

Waote waliosoma vitabu vile na kuvielewa, akili yao iko tofauti sana. Kiufupi iko juu.
Elvis Musiba alikuwa shida.
 
Aliyeandika watoto wa mama ntilie alitisha sana. Wanadai hao kina gamba et al walikuwa wana copy iriwaya za kizungu za kina chase na kuzileta kwa kiswahili japo siamini hili.
Naiomba hii Riwaya Mkuu please
 
Mkuu ni kweli kuna kucopy kwa baadhi ya riwaya. Nina riwaya moja ya joram inafanana na riwaya fulani ya hadley chase jina nmelisahau. Jamaa aliua matajairi wawili nadhani halafu waliobaki akawa anawatishia walipe pesa ili wasiuawe. Sasa hiyo riwaya ya joram ina kufanana fulani na hiyo riwaya.
Anasema fear is only thing that opens wallets of riches
 
Willy Gamba hats off.

Nakumbuka darasa la nne niliazimwa kitabu cha Njama kilikuwa kinagombewa mtaa mzima. Nikapewa sharti kumaliza kukisoma siku moja tu.

Nilijifungia ndani na kumaliza kukisoma kitabu siku moja tu.

Musiba alikuwa anahadithia Willy Gamba anakaa Upanga karibu na Palm Beach hotel. Enzi hiyo tunakaa Upanga karibu na bodyguard mmoja wa Nyerere yuko fit vibaya sana. Sasa hivi balozi. Basi mimi nikawa nasema usikute huyu ndiye Willy Gamba mwenyewe 🤣🤣🤣.
Naam Willy Gamba nilikuwa naishi hapo
 
Back
Top Bottom