Joram kiango vs Willy Gamba

Joram kiango vs Willy Gamba

Nafikiri wanalinganisha maudhui ya kiupelelezi ndo mana wanasema hivyo ila kiuhalisia sioni kufanana kwa kazi zao labda waseme ni riwaya gani wamecopy kutokea huko tulinganishe
Mkuu ni kweli kuna kucopy kwa baadhi ya riwaya. Nina riwaya moja ya joram inafanana na riwaya fulani ya hadley chase jina nmelisahau. Jamaa aliua matajairi wawili nadhani halafu waliobaki akawa anawatishia walipe pesa ili wasiuawe. Sasa hiyo riwaya ya joram ina kufanana fulani na hiyo riwaya.
 
Ni members wanajidai much know
Nimesoma vitabu vyote vya Aristablus Elvis Musiba vyenye story za Willy Gamba na pia nimesoma sehemu kubwa ya vitabu vya James Hadley Chase lakini sikumbuki kuona popote ambapo mtu unaweza kusema Musiba alikopi kutoka kitabu hiki cha James Hadley Chase. Labda staili ya uandishi.
 
Joram Kiango yumo kwenye Dar es salaam Usiku,Salamu kutoka kuzimu,Tutarudi na Roho zetu,Zawadi ya Usindi,Pesa zako zinanuka,najisikia kuua tena,Nyuma ya mapazia ,Mikononi mwa Nunda na vingine. Willy Gamba kwenye Njama,Kikosi cha kisasi,Hofu,Kikomo,Kufa na Kupona na Hujuma. Watunzi wote ben Mtobwa na Elvis Musiba wapo vizuri.Nimesoma vitabu vyao wote kila mmoja ana ladha yake .Musiba alimtumia muhusika wake mkuu Willy Gamba kama mtu wa Usalama wa Taifa wakati ben mtobwa alimtumia Joram kiango kama mpelelezi huru
 
Screenshot_20240111-221907_Chrome.jpg
 
Mkuu ni kweli kuna kucopy kwabaadhi ya riwaya. Nikariwaya moja ya joram inafanana na riwaya fulani ya hadley chase jinanmelisahau. Jamaa aliua matajairi wawili nadhani halafu waliobaki akawa anawatishia walipe pesa ili wasiuawe. Sasa hiyo riwaya ya joram ina kufanana fulani na hiyo riwaya.
Jaribu kukumbuka ukipata jina la hiyo riwaya ilite mana najaribu kukumbuka kisa cha namna hiyo lakini hakiji
 
Kuna riwaya inaitwa BADO MMOJA mtunzi ni D. Sangija ambapo mhusika mkuu alikuwa ni Mercus Nicholas (Kuzenza Sayuki) nimekitafuta miaka nenda rudi bila mafanikio. Nayo ilikuwa moto wa kuotea mbali. Mtunzi huyo alitunga riwaya nyingine iitwayo PENDO LA KIFO na KUKOPA HARUSI KULIPA MATANGA.
 
Back
Top Bottom