Joram kiango vs Willy Gamba

Joram kiango vs Willy Gamba

Mimi naipenda zaidi character ya joram kiango mzee wa totoz😃😃.Hivi Kuna mtu alisoma kitabu kinaitwa 'mkimbizi' mhusika mkuu alikua anaitwa 'Tiga Mumba', story yake ilikua nzuri Sana nilisoma nikiwa olevel, simkumbuki muandishi wake.
HUSSEIN ISSA TUWA MKIMBIZI.jpg
 
Willy Gamba kwenye kitabu cha Uchu, mule kapambana sana namna alivyoingia Rwanda, kujificha kwa kivuli cha Redcross, kuvamia kambi ya waasi na namna alivyotafuta ukweli kuhusu mauaji ya kimbali kwa kuhoji mapadre na Maofisa wa jeshi la Rwanda.

Baada ya kukamilisha mission akawawakilisha vijana wa kula kimasihara kwa yule dada chotara wa kifaransa aliyekutana nae Rwanda.
 
Tutarudi na roho zetu?

Joram Kiango aliupiga mwingi. Namna alivyokua anatoroka sehemu tata ilikua poa sana. Lakini pia ukisoma kile kitabu, utaona mwandishi aliyaona mambo ya artificial intelligence miaka mingi kabla hata hayajafikiwa kiuhalisia.

I go for Joram Kiango. Mchizi alikua loyal sana kwa mademu zake!
 
Back
Top Bottom