Joram kiango vs Willy Gamba

Joram kiango vs Willy Gamba

Joram Kiango yumo kwenye Dar es salaam Usiku,Salamu kutoka kuzimu,Tutarudi na Roho zetu,Zawadi ya Usindi,Pesa zako zinanuka,najisikia kuua tena,Nyuma ya mapazia ,Mikononi mwa Nunda na vingine. Willy Gamba kwenye Njama,Kikosi cha kisasi,Hofu,Kikomo,Kufa na Kupona na Hujuma. Watunzi wote ben Mtobwa na Elvis Musiba wapo vizuri.Nimesoma vitabu vyao wote kila mmoja ana ladha yake .Musiba alimtumia muhusika wake mkuu Willy Gamba kama mtu wa Usalama wa Taifa wakati ben mtobwa alimtumia Joram kiango kama mpelelezi huru
Hakika unawajua vyema kongole sana
 
Ni baadhi tuu, kuna vingine vingi havipo kama kufa na kupona nk.
Screenshot_20240111-222840_Chrome.jpg
 
Mimi Nina ushahidi wa riwaya moja ya Shaaban Robert alicopy Kila kitu kutoka riwaya nyingine. Nilisikitika sana vile napenda riwaya zake. Siku moja nitashusha Uzi wenye jina :
MFANANO USIO WA KAWAIDA KATI YA RIWAYA YA ......YA SHAABAN ROBERT NA HADIDHI ZA.....ZA....
Kusadikika...kufikirika au ni ipi
 
Kuna riwaya inaitwa BADO MMOJA mtunzi ni D. Sangija ambapo mhusikz mkuu alikuwa ni Mercus Nicholas (Kuzenza Sayuki) nimekitafuta miaka nenda rudi bila mafanikio. Nayo ilikuwa moto wa kuotea mbali. Mtunzi huyo alitunga riwaya nyingine iitwayo PENDO LA KIFO na KUKOPA HARUSI KULIPA MATANGA.
Riwaya nyingi za zamani utazipata maktaba za mkoa, ukipata nafasi jaribu kubahatisha unaeza ukakuta kipo katika mkoa wako
 
Mpk unatamani wewe msomaji ndio uwe Willy Gamba , binafsi naona zilikua zinajenga uzalendo
Sana. Hasa ile issue ya almasi za mwadui ni noma sana. Watu walizipenda mno ndio maana Nyerere akaona hawa jamaa watajifunza haya mambo iwe shida, akazipiga marufuku eti zinafundisha ujambazi kumbe hata yeye alikuwa anazisoma
 
Back
Top Bottom