John Tendwa Live on ITV katika 'Kipima Joto' cha Masako!

John Tendwa Live on ITV katika 'Kipima Joto' cha Masako!

Jamani Tendwa amechanganyikiwa...!Maskini Baba wa watu..
 
Kinachokuja akilini mwangu kama chanzo cha mauaji ya raia na polisi ni kwamba,kamati zote za ulinzi na usalama zinamilikiwa na ccm,mfano kamati ya ulinzi ya mkoa iko chini ya mkiti ambaye ni mkuu wa mkoa kada mtiifu wa ccm halafu RPC ni mjumbe,hali kadhalika ngazi ya wilaya hata kitaifa pia,kazi yao kubwa wanahodhi majeshi na kuyatumia kulinda chama chao,na sababu askari ni watu wa kupokea amri bila hata kujiuliza mithiri ya mbwa basi wanaua--toa sababu unazojua!
 
Sungusia anamuuliza Tendwa ni lini CCM walilalamika
kunyimwa kibari na polisi katika mikutano yao? Pia
anaeleza kuwa polisi wamekuwa wakikataa mikutano
ya wapinzani eti wamegundua kuna uvunjifu wa amani,
hii ina maana kuwa ni wachache kuweza kuzuia uvunjifu
huo, na mkutano ukifanyika utashangaa kuona polisi
wengi kupita maelezo kuja kudhibiti wapinzani...
 
Masako anamtwanga tena swali tendwa kwanini c c m walipata kibali cha mkutano zanzibar na niwakati wa sensa???
 
Sungusia anamuuliza Tendwa je ni mara ngapi aliwahi kupokea taarifa juu ya chama fulani kuzuiliwa mikutano yake? lakini anauliza tena wakati mwingine inatokea polisi wanasema wakati mwingine hawana polisi wa kutosha kulinda mkutano, lakini mkiandamana tu polisiwanakuja wa kutosha je walikuwa wapi? Masako anachana live siku tukio lilipotokea iringa la Mwangosi kufa, lakini bubu ccm walifanya mkutano.. je hii imekaaje... Tendwa anasema mkutano uliofanyika bubu je ni vigezo gani vilitumika kule, anasema masako na yeye (Tendwa) hawakuwepo huko na hivyo hawezi kuwajibia polisi
 
Mungu wangu! Waambieni hawa watu wa itv wamwache mzee wa watu, huoni wanamuumbua
 
Tendwa pamoja sina imani naye lakini kajibu swali la polisi vizuri.
 
Tendwa ni Kilaza. Anachofanya ni sawa na kukonyeza huku yupo kwenye giza
 
Jana daa bank majambaz wamefanikiwa kuiba milion 300. Kwasababu jesh la polis wapo likizo wote wanasubiri mikutano ya chadema. Kwahy majambaz wakaiba kiulaini
 
Tendwa jihoji,jitathimini,jielewe,jifikirie...usijichanganye.....wewe lazima uepuke kuegemea upande wa chama tawala,vinginevyo kama kuna lolote linalosabadishwa na kutotumia hekima zako,utahukumiwa kadri ulivyopanda.
 
Kutokana na upuuuzii anaoongea huyu kada wa magamba, na kwa jinsi anavyobanywa na kuishia kuongea vepa, natumaini baada ya huu mjadala, atajifunza kukaa kimya kama afanyavyo mzee wa intelejensia, makengeza kova...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom