John Tendwa Live on ITV katika 'Kipima Joto' cha Masako!

commited

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,626
870
Wadau mlio karibu na tv, angalieni kipima joto ITV.

Mada mezani, ni "Je, kuongezeka kwa mauaji ya raia katika mikutano ya vyama vya kisiasa ni kukua kwa demokrasia?"

Wageni waalika ni John Tendwa, bwana Harord Sungusia, huyu mwingine sijampata vizuri, polisi walialikwa pia lakini wamegoma kuja.

Tendwa ameanza kubwabwaja..... Masako anambana vilivyo
 
Wana jf

Msajili wa vyama vya siasa na gamba tiifu John Tendwa yuko live itv anabwabwaja karibuni.
 
Tenda anazidi kujichanganya.Alisema juzi kuwa ataifuta CDM huku akifahamu kuwa ni haki ya raia kuandamana.Anazeeka vibaya.Fuatilia ITV-Live hivi sasa.
 
Safi sana masako kauliza,,,,,,,,inakuwaje Chama kingine kilikuwwa kinafanya kitu hicho hicho lakini hawakuguswa.....bali wakafuatwa CDM........kajibu ati Polisi ilitakiwa watekeleze sheria
 
Msajili wa vyama vya siasa anaelezea juu ya utaratibu wa Chama cha siasa kuomba kufanya maandamano au hotuba.Maelezo yake sasa yanaeleza jinsi sheria inavyosema bila vitisho kama alivyotoa mwanzo.
 
Sina hakika kama huwa anakuwa objective huyo mzee, he is most of the time emotional and sentimental!!!
 
Sungusia anasema kazi ya polisi si kuuwa bali ni kulinda usalama wa taifa
 
Safi sana masako kauliza,,,,,,,,inakuwaje Chama kingine kilikuwwa kinafanya kitu hicho hicho lakini hawakuguswa.....bali wakafuatwa CDM........kajibu ati Polisi ilitakiwa watekeleze sheria

anazidi kujichanganya inamaana ana kubali polisi kuionea cdm!
 
Tutakujulisha Tendwa atakachosema, kwa kuanzia alianza kwa kusoma sheria ya usajili wa vyama.
 
Tv yangu chenga chenga, mpigeni picha tendwa anatamani ardhi ifunguke imfunike.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom