Ukimuwaza na kumfikiria sana Mzee Tendwa utagundua vitu kadhaa kwake.
1. Unaweza kusema kuwa ni mnafiki na mchonganishi. Ukimfikiria hivi, unajijazia uzito wa hoja yako kwa kukumbuka kauli alizozitoa kule Arumeru kuhusu Glema wakati wa uchaguzi ulio mpa Nassari ubunge, alisema "Wazee wa kimila (washiri) wamesema hawataki kumuona Lema Arumeru na wakimuona wana wata mdhuru" ilikuwa kauli yake haikuwa kauli ya wazee, yeye msimamazi wa vyama vya siasa akachagua upande! _Unafiki.
2. Ukisema kuwa ni kibaraka anae panga mipango ovu na ccm kwa kivuli cha usajili na u- refarii wa vyama vya siasa pia huwezi kukosea! Jijazie hoja yako kwa kurejea kwenye kauli yake ya kufuta vyama vitakavyo sababisha mauwaji! Hapa alimaanisha cdm. Kumbuka maneno ya kina Nape, shigella na Nchimbi halafu kauli za polisi kuhusu mauwaji. Kama una akili timamu huhitaji kuwa na shahada ya chuo kikuu kujua kuwa kulikuwa na mpango mkubwa ulioshindwa nyuma yake! Mpango umeshindwa kwa kuwa Mungu alipanga kuwaumbua. Kusinge patikana picha za muuwaji wa Mwangosi ndio tunge ona rangi halisi za Tendwa kupitia kauli za Nape, Shigella, Nchimbi na jeshi la polisi.
3. Unaweza kusema pia kuwa mzee wetu Tendwa hajui analolifanya bali anaendeshwa kwa remote control! Kwa kuwa hakuna viongozi wa serikali wanao ikemea ccm na yeye hakemei matendo yao! Kwa kuwa wapo. Viongozi wa serikali wano ikemea cdm kwa kuwa wana ihofu na inawapa tumbo joto nae anungwana nao hata panapo kuwa na upendeleo wa wazi! Anailamu chadema kwa kuandamana anaifumbia macho ccm ikiandamana maana niya chama tawala na wao ndio wamempa ulaji.
Tendwa ni mzee wetu lakini naweza kuthubutu kusema kuwa mzee wetu anajivua heshima yake kwa kuwa kipofu mbele ya ccm na kuvaa darubini mbele ya cdm.
Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.