John Tendwa Live on ITV katika 'Kipima Joto' cha Masako!

John Tendwa Live on ITV katika 'Kipima Joto' cha Masako!

Adhabu ya kuandamana au kufanya mkutano wa hadhara bila kutoa taarifa ni shilingi elfu 50 au kifungo cha miezi 3 gerezani,hii ni kwa mujibu wa sheria
 
Ukimuwaza na kumfikiria sana Mzee Tendwa utagundua vitu kadhaa kwake.

1. Unaweza kusema kuwa ni mnafiki na mchonganishi. Ukimfikiria hivi, unajijazia uzito wa hoja yako kwa kukumbuka kauli alizozitoa kule Arumeru kuhusu Glema wakati wa uchaguzi ulio mpa Nassari ubunge, alisema "Wazee wa kimila (washiri) wamesema hawataki kumuona Lema Arumeru na wakimuona wana wata mdhuru" ilikuwa kauli yake haikuwa kauli ya wazee, yeye msimamazi wa vyama vya siasa akachagua upande! _Unafiki.

2. Ukisema kuwa ni kibaraka anae panga mipango ovu na ccm kwa kivuli cha usajili na u- refarii wa vyama vya siasa pia huwezi kukosea! Jijazie hoja yako kwa kurejea kwenye kauli yake ya kufuta vyama vitakavyo sababisha mauwaji! Hapa alimaanisha cdm. Kumbuka maneno ya kina Nape, shigella na Nchimbi halafu kauli za polisi kuhusu mauwaji. Kama una akili timamu huhitaji kuwa na shahada ya chuo kikuu kujua kuwa kulikuwa na mpango mkubwa ulioshindwa nyuma yake! Mpango umeshindwa kwa kuwa Mungu alipanga kuwaumbua. Kusinge patikana picha za muuwaji wa Mwangosi ndio tunge ona rangi halisi za Tendwa kupitia kauli za Nape, Shigella, Nchimbi na jeshi la polisi.

3. Unaweza kusema pia kuwa mzee wetu Tendwa hajui analolifanya bali anaendeshwa kwa remote control! Kwa kuwa hakuna viongozi wa serikali wanao ikemea ccm na yeye hakemei matendo yao! Kwa kuwa wapo. Viongozi wa serikali wano ikemea cdm kwa kuwa wana ihofu na inawapa tumbo joto nae anungwana nao hata panapo kuwa na upendeleo wa wazi! Anailamu chadema kwa kuandamana anaifumbia macho ccm ikiandamana maana niya chama tawala na wao ndio wamempa ulaji.

Tendwa ni mzee wetu lakini naweza kuthubutu kusema kuwa mzee wetu anajivua heshima yake kwa kuwa kipofu mbele ya ccm na kuvaa darubini mbele ya cdm.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.

Huyu mzee ni dhaifu kupita kiasi, lakini ukisoma saikolojia unajua wazee ni watu ambao hujiamini sana na huwa hawana cha kupoteza coz wanajua wakati wao umeisha so huwa wanaongea tu na kufanya lolote liwe (LIWALO NA LIWE)
 
Adhabu ya kukaidi amri ya katazo la kufanya maadamano au mikutano ne faini elfu 50, au kifungo cha miezi mitatu au vyote kwa pamoja wala sio kuua raia anayekaidi katazo hilo- Kipimajoto-ITV leo.
 
Isije ikawa anaomba suluhu katika kipindi hiki cha matangazo,
au msishangae mkiona amesepa maana hali ni mbaya...
 
Kumbe mabadiliko yanawezekana wajamen????

Haya ndio majibu ya Ritz kweli??

Usiogope mkuu, mabadiliko huja taratibu sana.. umeshamuona rejao huku tena , au Faiza fox .....siku moja tutaongea nao lugha moja
 
Hivi huyu mtangazaji wa ITV si aligombea ubunge kupitia CCM.
 
Tenda anazidi kujichanganya.Alisema juzi kuwa ataifuta CDM huku akifahamu kuwa ni haki ya raia kuandamana.Anazeeka vibaya.Fuatilia ITV-Live hivi sasa.
Leo kakwepesha yale aliyosema juzi
 
Hivi Tendwa kwa kweli uwa simuelewa kwanza anajifanya kiswahili kinampa shida halafu ana tabia za kibabe ambazo zinamfanya awe anropoka hovyo.

Ongea na mshua am-delete kwenye hiyo post...
 
Adhabu ya kuandamana au kufanya mkutano wa hadhara bila kutoa taarifa ni shilingi elfu 50 au kifungo cha miezi 3 gerezani,hii ni kwa mujibu wa sheria

sasa mbona anazidi kuwadharirisha wenzie?
 
Tendwa leo kazi ipo,
masako amemvalisha viatu ambavyo vinampwaya.
Hao wajomba ni noma,they talk with data
 
Hafai hata kidogo Huyu Tendwa kuleta vyama vya Siasa, anabubujika maneno tu! Bado Ana mategemeo ya pesa za wafadhili eti kuwezesha political dialogue Kati ya vyama vya Siasa, polisi na wanaharakati. Uzuri wachangiaji wanampasha kiuwazi kabisa tena kwa kuelezea maana halisi ya demokrasia.
 
Huenda Tendwa akakimbia leo studio, maana kakamatwa pabaya!!
 
Mhhh. Hivyo CDM wakilipa Shs 50,000 x2, Policcm wanaweza kuwarudisha waliowaua Moro na Kilolo?
 
SUNGUSIA: Mfumo wa chama kimoja ni chanzo cha migogoro: mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa usalama wa mkoa na RPC anakuwa chini yake!; Wilaya DC ni mwenyekiti OCD yuko chini yake. Na wote hao wawili (RC na DC) ni makada wa chama kilichopo madarakani. Hivyo kinachofanywa na polisi ni maagizo ya chama tawala. Kikao cha Tendwa kijacho kihusishe vyama vya siasa si polisi ili CCM wasitumie vibaya uhuru walionao.
 
Hashindw kwn masako nae c gamba cialiangukia pua morogoro kwenye kura za maoni za kufuata posho ndefu bungeni

Kwani watu hawabadiliki? Kakumbana na mizengwe
ndo maana kageuka, na sasa anawachambua...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom