John Shibuda: Mbowe ni dikteta

John Shibuda: Mbowe ni dikteta

Shibuda huwa simuelewi ni kama vile ana sura mbili za chadema na ccm
 
Mbowe anajulikana ni DJ wa muziki sio kiongozi wa siasa, sasa ulitegemea aache kuwapendelea watu wa kanda ya kaskazini akupe wewe Shibuda ?. Ni afadhali umetoa jina lako , na hiyo ni rasha rasha tu, mvua ya udikteta wa mbowe yaja
 
shibuda,
naona umeanza rasmi kufanya kazi yako ULIYOTUMWA!

TUNAJUA KILA KITU
TUNAJUA MICHEZO YOTE MICHAFU YA CHAMA TAWALA
 
CDM hawaoni makosa ya baba yao Mbowe, they will try to justify his every move....the guy is a crook. The party now needs a strong visionary leader not this thug....


wabunge wote wako shwari isipokuwa wawili tuuu....guess who??shibuda na zitto....wamepokea hela za mafisadi kuvuruga chama lakini wamestukiwa mapema...chadema majasusi wewe...nafikiri sugu ameupdate ANTIVIRUS YAKE...kama alivyosema slaa..hakuna aliye juu ya chama..chadema is here to stay..my conscious is telling me that they are here for the right course..iam down with them to the very end
 
Kipindi kingine CDM wawachunguze hawa watu wanohamahama vyama kabla ya kupewa dhamana kubwa..
Ni heri kuwa na wabunge wawili wenye msimamo na kuheshimu mamlaka kuliko mia wasioeleweka..
 
Kuna taarifa kwamba Shibuda kufukuzwa Chadema, aonekana ni mamluki kutoka ccm.na nafasi ya zito kuchukuliwa na Luwakatare.source: Uhuru gazeti makini
source ya ms: baada ya kumsikiliza dk slaa Jana kupitia Tv mlimani aliposema kwamba Shibuda unamchunguza kwa kauli zake.napata picha kwamba Shibuda anaonekana ni mamluki ndani ya Chadema


Kwakweli kuanzia leo mtu atakaekuwa anamchukia malaria sugu basi huyo mtu atakuwa ana tafuta ugomvi na mimi, i like this guy, hii ni propaganda mashine ambayo hata kama umenuna saa nyingine waweza kucheka, kama mtakumbuka vizuri wakati wa utawala wa Saddam Hussein waziri wake wa habari alikuwa i Al Sahaf, na George W Bush alimpenda sana wakati ule wa vita kutokana na kuwa a good propaganda machine, na ikafikia Bush kumuondoa Al sahaf kwenye orodha ya maofisa wa serikali ya Saddam Hussein waliopaswa kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.
sasa kwa mimi Malaria sugu kwangu ni kama Al Sahaf, anaburudisha, kumbuka buruani sio lazima imvutie kila mtu.
dokezo: burudani zangu kwa malaria sugu huanzia pale unapoona thread yake ameiedit lakini bado mafyongo matupu spell check ndio sifuri kabisa, na kama huamini hili angalia signature yake sasa hivi nadhani na wewe utaanza kuwa a fans of MS.
 
When was the last time dictatorship was regarded as a good brand?

Dictatorship is relative...only depends on which angle you are looking out from.

Saddam Hussein was branded as one.....

George W Bush (then prez of arguably the biggest democracy on the planet) ignored all democratic calls across the globe and went on ahead to kill innocent people in Iraq in his evil pursuit of toppling Saddam. Bush was never branded a dictator, was he?

I hear there's similar name-calling for Kagame.....a man who is about to turn his tiny nation into a regional economical superpower!

The list goes on...
 
Mkuu ningependa unielimishe ukiacha nafasi ya ubunge, je SHIBUDAana cheo gani ndani yaCHADEMA? au ni mjumbe wa kikao kipi na alichaguliwa lini?
2. si ndio huyu huyu UDSHIBA mwenye uchu wa nyama aliyekwenda kwenye mnuso wa uzinduzi wa bunge wakati wenzake walimwacha mkwere akae na wasanii wenzake wachekecheke vizuri? sasa mtu mwenye uchu wa nyama unategemea nini kutoka kwake? labda tumshauri MBOWE awe anchinja mbuzi kila wiki kuwafurahisha wenye uchu wa nyama.
soma hayo maandishi niliyoyakuza....nahisi harufu ya chuki ya udini na ukabila katika post yako.
ningekuwa MOD,,, nadhani wapumbavu mnaotumia makalio kufikiria kama wewe msingepata nafasi jukwaani. ila kwa sababu ya uhuru wa kujieleza alioupromot MKWERE! hatuna budi kuusoma ujinga wenu
 
Mkuu ningependa unielimishe ukiacha nafasi ya ubunge, je SHIBUDA ana cheo gani ndani ya CHADEMA? au ni mjumbe wa kikao kipi na alichaguliwa lini?
2. si ndio huyu huyu SHIBUDA mwenye uchu wa nyama aliyekwenda kwenye mnuso wa uzinduzi wa bunge wakati wenzake walimwacha mkwere akae na wasanii wenzake wachekecheke vizuri? sasa mtu mwenye uchu wa nyama unategemea nini kutoka kwake? labda tumshauri MBOWE awe anchinja mbuzi kila wiki kuwafurahisha wenye uchu wa nyama.



Kweli devide & rule inaonekana kufanikiwa. Yaani watu wamepandikiziwa chuki wenyewe kwa wenyewe na wakakubali?
 
Tatizo wana chadema ukweli hamtaki.
Huu ndio ukweli Mbowe ni fisadi wa uongozi na Slaa wake.
Ukabira umejaa humo chadema.
 
Sijui nini hakijaeleweka kwa wana-JF, Shibuda ni mmoja ya mapandikizi ya sisiem, huyu ni kibaraka alitumwa rasmi kuja kuvuruga cdm baada ya CCM kuona joto linalowakabili. Wana CHADEMA Siyo mwenzetu huyu aogopwe kama ukoma.
 
Je hayo uliyoyaorodhesha yametokea kipindi ambacho Bob Makani ndie Mwenyekiti wa Chama au Aikaeli?


Sasa kama yametokea wakati yeye ndie mwenyekiti wa chama basi anastahili pongezi.


Ngoja nikupe Mfano:
Anza tangu enzi ya Marehemu Kolimba, pitia mpk kwa Mangula kisha njoo kwa Baba January.
Je ni kipindi cha nani kama katibu mkuu ambacho chama kimeporomoka?


Au anzia kwa Mchonga, Mzee Ruksa, Uncle Ben au kwa huyu wa sasa je ni uongozi wa nani ambao chama kimeonekana kuporomoka?


Sasa ukipata jibu ndo utakuwa umefahamu kwa nini Mbowe anaheshimika na yeye binafsi yuko imara kuhakikisha hakuna ushuzi yeyote ambaye ni pandikizi atapata nafasi ya kutema sumu.


Endelea Mbowe, hao wanaopiga kelele ni madebe matupu tu

Bado hujajibu hoja yangu ni vipi Mbowe amekisaidia Chadema kukua? Usizungumze upupu kaka au dada?
 
Gazeti la Mtanzania 13 December 2010 limemnukuu Shibuda akilalamika kuwa mbowe ni Dikteta na anawaburuza na anajenga makundi badala ya umoja ndani ya chama

"hali ilikwishachafuka, Mbowe anaendesha vikao kwa ubabe, kuhujumiana, kubomoana na kujenga makundi... ule ulikuwa mkutano wa uchaguzi wa wajumbe watano wa kamati kuu, lakini ukatanguliwa na hicho kikao cha kuvunjiana heshima, ilibidi nitoe jina langu" alisema Shibuda.

Shibuda kama ulikuwa hujui huyo ndio Mbowe.
Mhe. Shibuda arejee sisiem , huko alishataka kuwa Rais wa Tz
 
kwa sasa marando bado ni shujaa ila akikutana na ubabe wa mbowe na kumtolea uvivu atapewa jina baya

ukitaka kumuuwa paka mpe jina baya
 
Mbowe, Ze Dictator!!
kiongozi CHADEMA ni Slaa pekee!!
Uchaguzi ujao Slaa achukue uenyekiti, na ukatibu vyote. utaona chama kitakavyo plogless.
ha ha ha ha ha ha
 
Bado hujajibu hoja yangu ni vipi Mbowe amekisaidia Chadema kukua? Usizungumze upupu kaka au dada?

hoja yako ni uharo.
Sina haja ya kukuorodheshea aliyoyafanya Mbowe ila kama unakifuatilia chama cha Chadema kilivyokuwa kabla ya Mbowe na sasa wakati mwenyekiti ni Mbowe utagundua ni yepi ambayo Mbowe amesaidia.
Ukishindwa kuelewa hapo tena basi
 
Back
Top Bottom