GE2025 John Heche: Waliokatwa CCM wananipigia Simu, wanalalamikia mwenendo wa Chama na kuonesha matumaini kwa CHADEMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amesema baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokatwa kwenye mchakato wa uteuzi wamekuwa wakimpigia simu wakilalamikia mwenendo wa chama hicho na kueleza matumaini yao kwa CHADEMA.

Akizungumza nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2025 mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Tundu Lissu, Heche amesema:

“Tupiganie haki kwa sababu hakuna aliye salama. Jana kuna watu wa CCM wamenipigia wanasema, ‘kwanini hampeleki chama kwenye uchaguzi, sisi tungekimbia kuja huku’. Hawa walikuwa kwenye utawala, lakini sasa wameonja maumivu, ndiyo wanajua kwamba CHADEMA ndiyo chombo cha kuwasaidia.”

Heche amesisitiza kuwa chama chao kitaendelea kupigania haki na kusimama na Tundu Lissu, akibainisha kuwa licha ya Lissu kuwa na haki ya kuwa huru, bado kuna mazingira yanayozuia maamuzi huru kufanyika mahakamani.

Video: Jambo TV
 
Hao jamaa waliokatwa na kuanza kusumbua chadwma ni njaa tu, hawana nia ya kweli ya mageuzi…

This is a killer ya chadema, makapi na mamluki

Chakandumuz jizaeni upya by texturing youths wasiopenda matusi na vurugu - na wawe wanajiandaa kuwa viongozi kifikra, vitendo na falsafa

10 years down the road watachukua dola
 
Hao jamaa ni njaa tu, hawana nia ya kweli ya mageuzi…

Hii ndio comment nilikuwa naitafuta. Chadema wanatakiwa kujenga vijana wazalendo wanaojua sheria na sio shari.

Vijana wenye mtazamo wa utulivu lakini ambao ni wabishi na wafanya maamuzi sampuli za akina Martin Luther king Jr.

Vijana wanatakiwa wasome sheria za inchi na kujieleza kwa kwa kuzijua lakini pia wajue madhaifu ya hizo sheria. Na ndani ya Chadema kuwa na shuffling ya uongozi kusiwe na sura zile zile kwenye uongozi miaka yote.

Wajitahidi pia hawa vijana wasiwe ni wahuni wawe wachapa kazi na wanaojua kujituma.
 
Heche anawaamini hao watu? Yaani kama Heche awaamini waliokatwa atakuwa ni mjinga namba moja
 
Hao jamaa ni njaa tu, hawana nia ya kweli ya mageuzi…

This is a killer ya chadema, makapi na mamluki

Chakandumuz jizaeni upya by texturing youths wasiopenda matusi na vurugu - na wawe wanajiandaa kuwa viongozi kifikra, vitendo na falsafa

10 years down the road watachukua dola
Matusi gani CHADEMA Huwa wanatukana?
Na Kwa akili hii unaamini ni haki yako kutotukanwa.
 
Hii ndio comment nilikuwa naitafuta. Chadema wanatakiwa kujenga vijana wazalendo wanaojua sheria na sio shari.

Vijana wenye mtazamo wa utulivu lakini ambao ni wabishi na wafanya maamuzi sampuli za akina Martin Luther king Jr.

Vijana wanatakiwa wasome sheria za inchi na kujieleza kwa kwa kuzijua lakini pia wajue madhaifu ya hizo sheria. Na ndani ya Chadema kuwa na shuffling ya uongozi kusiwe na sura zile zile kwenye uongozi miaka yote.

Wajitahidi pia hawa vijana wasiwe ni wahuni wawe wachapa kazi na wanaojua kujituma.
Hao vijana wapo nchi gani au mnataka wakawatoe Kenya.
Ndiyo maana watu Huwa wanawatukana Kwa sababu mnatetea upumbavu Kwa hoja dhaifu na za kijinga.
CHADEMA ni chama Cha watanzania na kipoe Tanzania,hao aina ya vijana unaowasema CCM mnao au ACT wanao?
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amesema baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokatwa kwenye mchakato wa uteuzi wamekuwa wakimpigia simu wakilalamikia mwenendo wa chama hicho na kueleza matumaini yao kwa CHADEMA.

Akizungumza nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2025 mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Tundu Lissu, Heche amesema:

“Tupiganie haki kwa sababu hakuna aliye salama. Jana kuna watu wa CCM wamenipigia wanasema, ‘kwanini hampeleki chama kwenye uchaguzi, sisi tungekimbia kuja huku’. Hawa walikuwa kwenye utawala, lakini sasa wameonja maumivu, ndiyo wanajua kwamba CHADEMA ndiyo chombo cha kuwasaidia.”

Heche amesisitiza kuwa chama chao kitaendelea kupigania haki na kusimama na Tundu Lissu, akibainisha kuwa licha ya Lissu kuwa na haki ya kuwa huru, bado kuna mazingira yanayozuia maamuzi huru kufanyika mahakamani.

Video: Jambo TV
Wanaogopa tu mpama muda huu wangekuwa wameshahamia NRNE.

Huu mwaka hawatoboi
 
Kama ni kweli, hao sio wapenda maendeleo ya taifa, ila ni walafi, wazee wa fursa,
Ina maana ubaya wameanza kuuona baada ya kutemwa ubunge wangepitishwaz wangeona ni sawa tu.

Hao ni wa kunyonga, hapo wa kuongea hivyo ni MPINA pekee mwenye haki hiyo, alianza mapambano toka akiwa CCM
 
Back
Top Bottom