GE2025 John Heche: Waliokatwa CCM wananipigia Simu, wanalalamikia mwenendo wa Chama na kuonesha matumaini kwa CHADEMA

GE2025 John Heche: Waliokatwa CCM wananipigia Simu, wanalalamikia mwenendo wa Chama na kuonesha matumaini kwa CHADEMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amesema baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokatwa kwenye mchakato wa uteuzi wamekuwa wakimpigia simu wakilalamikia mwenendo wa chama hicho na kueleza matumaini yao kwa CHADEMA.

Akizungumza nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2025 mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Tundu Lissu, Heche amesema:

“Tupiganie haki kwa sababu hakuna aliye salama. Jana kuna watu wa CCM wamenipigia wanasema, ‘kwanini hampeleki chama kwenye uchaguzi, sisi tungekimbia kuja huku’. Hawa walikuwa kwenye utawala, lakini sasa wameonja maumivu, ndiyo wanajua kwamba CHADEMA ndiyo chombo cha kuwasaidia.”

Heche amesisitiza kuwa chama chao kitaendelea kupigania haki na kusimama na Tundu Lissu, akibainisha kuwa licha ya Lissu kuwa na haki ya kuwa huru, bado kuna mazingira yanayozuia maamuzi huru kufanyika mahakamani.

Video: Jambo TV
Heche ana akili sana.
Maneno yake yana maana kuwa CHADEMA ndio tegemeo la wengi hata waliomo CCM, na kwamba Reforms zikifanyika, wanufaika ni Watanzania wote bila kujali uchama.
 
Back
Top Bottom