John Heche: CHADEMA ina wanachama milioni nane

Kwani CAG hakagui? Hata PCCB walikagua hawakuona ubadhirifu ila ww layman wa JF ndio una doubt??

CHADEMA ilisimamisha wagombea 95% ya mitaa, vijiji na vitongoji alafu unadhani hakijasambaa kama CCM!!?
Na hii ndiyo ilimtisha sana dikteta uchwara akaamua kuuvuruga uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Sukuma gang naona unajipa faraja baada ya jini lenu kufa na Sasa linabagazwa na mama kwamba lilikuwa fisadi
Yaani unawatukana Bure sukumagang yaani sio ccm Wala Chadema yeyote anaweza kuwachukua ninyi Chadema hamjitambui tyuu hawa Sasa sukumagang wananing'ia Kama mtakuwa na ushawishi mtaweza kuwachukua, kazi kenyuu sasa
 
Mbunge wa zamani wa Chadema jimbo la Tarime amesema hivi sasa chama hicho kimepata mafanikio makubwa kutokana na kampeni ya Chadema digito inayoendelea. Amesema hayo leo tarehe 4 Disemba 2021 kupitia kipindi cha Medani ya Siasa cha Star TV kinachoendeshwa na Odemba. Amesema kupitia kampeni hiyo chama hicho kimesajili wanachama milioni nane.

Aidha amesema kutokana na kuwa na wanachama hao milioni nane ambao wanachangia Shs. 500/= kwa mwezi kila mmoja, Chama kinapata Shs. Bilioni nne kwa mwezi.

Fedha hizo zitakiwezesha Chadema kuendesha shughuli za kiofisi na kujenga ofisi mpya katika majimbo mbalimbali.
Huo ndio mtaji wa chama; na mkiweza kuutumia vyema mtaji huo hakuna litakaloshindikana mbele yenu.

Hakuna anayeweza kuchezea kura za watu milioni nane, hata awe na jeshi kubwa kiasi gani. Kazi mliyobaki kuifanya nyinyi viongozi ni jinsi ya kuwaongoza hao wanachama wenu kukataa kudhurumiwa haki zao.
 
waoneshe mfano kwa kuweka wazi hesabu za makusanyo na matumizi ya chama ikiwezekana kila mwezi...

wanachama 8mil iwe ni halisi na wawe wanapiga kura....kama CDM ina wanachama hai 8mil..CCM itakuwa na wanachama wangapi? maana wanufaika wa CCM ni wengi kuliko tunavyofikiri kuanzia huko mashinani mpaka mikoani kwa viongozi na familia zao...kumbuka CCM imefika kila mahala kuanzia kigonsela, nanyamba mpaka kibirizi na mwandiga kwa ZZK...
CCM imebaki kwenye vitabu vya historia tu. Inategemea vyombo vya dola tu
 
waoneshe mfano kwa kuweka wazi hesabu za makusanyo na matumizi ya chama ikiwezekana kila mwezi...

wanachama 8mil iwe ni halisi na wawe wanapiga kura....kama CDM ina wanachama hai 8mil..CCM itakuwa na wanachama wangapi? maana wanufaika wa CCM ni wengi kuliko tunavyofikiri kuanzia huko mashinani mpaka mikoani kwa viongozi na familia zao...kumbuka CCM imefika kila mahala kuanzia kigonsela, nanyamba mpaka kibirizi na mwandiga kwa ZZK...
Rudi kwenye uchanguzi wa 2015 angalia idara ya wapiga kura

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Mbunge wa zamani wa Chadema jimbo la Tarime amesema hivi sasa chama hicho kimepata mafanikio makubwa kutokana na kampeni ya Chadema digito inayoendelea. Amesema hayo leo tarehe 4 Disemba 2021 kupitia kipindi cha Medani ya Siasa cha Star TV kinachoendeshwa na Odemba. Amesema kupitia kampeni hiyo chama hicho kimesajili wanachama milioni nane.

Aidha amesema kutokana na kuwa na wanachama hao milioni nane ambao wanachangia Shs. 500/= kwa mwezi kila mmoja, Chama kinapata Shs. Bilioni nne kwa mwezi.

Fedha hizo zitakiwezesha Chadema kuendesha shughuli za kiofisi na kujenga ofisi mpya katika majimbo mbalimbali.
Kwanza wajenge makao makuu ya chama.

Back
Top Bottom