John Heche: CHADEMA ina wanachama milioni nane

Mbunge wa zamani wa Chadema jimbo la Tarime amesema hivi sasa chama hicho kimepata mafanikio makubwa kutokana na kampeni ya Chadema digito inayoendelea. Amesema hayo leo tarehe 4 Disemba 2021 kupitia kipindi cha Medani ya Siasa cha Star TV kinachoendeshwa na Odemba. Amesema kupitia kampeni hiyo chama hicho kimesajili wanachama milioni nane.

Aidha amesema kutokana na kuwa na wanachama hao milioni nane ambao wanachangia Shs. 500/= kwa mwezi kila mmoja, Chama kinapata Shs. Bilioni nne kwa mwezi.

Fedha hizo zitakiwezesha Chadema kuendesha shughuli za kiofisi na kujenga ofisi mpya katika majimbo mbalimbali.
Hongereni kwa ubunifu tofauti na yale majangili yanatumia mali za umma kama za chama
 
Back
Top Bottom