Mwanza: Heche achangisha Tsh. Milioni 2.3 kujenga ofisi ya CHADEMA

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, John Heche ameahidi kuchangia shilingi milioni 2.3 kusaidia ujenzi wa ofisi ya chama hicho Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Heche ametoa ahadi hiyo mjini Sengerema leo Jumatatu Novemba 14, baada ya kupokea taarifa ya Katibu wa Chadema jimbo la Sengerema, Paskazia Renatus kuhusu mpango wa kununua kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisi ya chana wilayani humo.

"Nawapa changamoto wa kujichangisha kupata zaidi ya Sh1.6 milioni za kununua kiwanja; na mkishakinunua mimi natawaunga mkono kwa kuchangia Sh2 milioni ili kuanza ujenzi," amesema na kuahidi Heche

Ahadi hiyo ya mbunge huyo wa zamani wa Tarime vijijini uliibua hamasa miongoni mwa wana Chadema waliohudhuria mkutano ambao walimuunga mkono kwa kujichangisha na kupatikana zaidi ya Sh300, 000 papo hapo.

Awali, Katibu wa CHADEMA jimbo la Sengerema, Paskazia Renatus ameueleza mkutano huo kuwa zaidi ya Sh350, 000 tayari zimechangwa kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja cha kujenga ofisi za chama.

MWANANCHI
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, John Heche ameahidi kuchangia shilingi milioni 2.3 kusaidia ujenzi wa ofisi ya chama hicho Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

MWANANCHI
Miaka Zaid ya 30 mnaZungumzia habari za viwanja wakati CCM ilishavuka na kupita habari hizo, kweli Chadema imechoka na kupoteza muelekeo kabisa, haina dira Wala muelekeo.

Kazi kutafuna Ruzuku na michango yote, Fedha za join the chain mmezitafuna yote na hapo Tena mnataka muanzishe upigaji mwingine, Hizo laki tatu mnapeleka zote mifukoni mwenu Kama kawaida yenu
 
Miaka Zaid ya 30 mnaZungumzia habari za viwanja wakati CCM ilishavuka na kupita habari hizo, kweli Chadema imechoka na kupoteza muelekeo kabisa, haina dira Wala muelekeo. Kazi kutafuna Ruzuku na michango yote, Fedha za join the chain mmezitafuna yote na hapo Tena mnataka muanzishe upigaji mwingine, Hizo laki tatu mnapeleka zote mifukoni mwenu Kama kawaida yenu

CHADEMA imeanza lini kupata ruzuku? Ruzuku wanapata kiasi gani Kwani?? Mbona nyie tangu tupate u huru mnaongoza na hadi leo mnaongelea habari za kuleta maji na uneme? Kila awamu ahadi ni hizo hizo tu
 
CCM iliondoka na mali za serikali yani imerithi mali za TANU ambazo zilipatikana enzi za chama kimoja.

Lakini mpaka leo baada ya miaka 60 CCM kila mwaka inaongelea kuchangisha wananchi kujenga madarasa na madawati, kumtua mama ndoo yaank hakuna hata 1 ililofanikisha
 
Tulipokuwa tunapata Uhuru tulikuwa millini 12 na Leo tupo million 60 ,Sasa Kama watu wanaongezeka kila mwaka unafikiri Mahitaji ya hayo uliyoyasema yatakuwa Kama miaka ya 60? Sasa nyie Ruzuku mmepokea miaka yote Lakini hata rangi tu mmeshindwa kupaka ofisini penu
 
Nchi tulizokuwa nazo sawa ambazo leo zimesonga hazina hizo excuse.

Kwani huwa hamjui kuwa population inakuwa mkapanga kabla? Au yale yale yakusubiri watu wajenge bila mipango halafu mje mbomoe kutanua barabara?

Kila kitu ni excuse tu.
 
CHADEMA imeanza lini kupata ruzuku? Ruzuku wanapata kiasi gani Kwani?? Mbona nyie tangu tupate u huru mnaongoza na hadi leo mnaongelea habari za kuleta maji na uneme? Kila awamu ahadi ni hizo hizo tu
Sabodo aliwachangia wee mpaka akachoka mkaishia kunywea mapombe tu, mkawa mnawachangisha wabunge wenu lakini bado mkazitafuna zote kwa anasa, pesa za Ruzuku zote mnapeleka matumboni mwenu, Sasa nyie mlitaka muwe na shilingi ngapi? Ndio maana Watanzania wamewapuuza Sana nyie
 
Wacha tujenge ofisi zetu kwa nguvu ya wananchama wetu, vyama vingine hadi vipige uchawa vipewe pesa ya umma - sisi tunaamini kwenye nguvu ya umma & nguvu ya wanachama wetu ndiyo msingi wa CDM ulipo.

Ofisi zote cha Chama zitajengwa kwa nguvu ya wanachama wenyewe !!
 
Miaka Zaid ya 30 mnaZungumzia habari za viwanja wakati CCM ilishavuka na kupita habari hizo, kweli Chadema imechoka na kupoteza muelekeo kabisa, haina dira Wala muelekeo. Kazi kutafuna Ruzuku na michango yote, Fedha za join the chain mmezitafuna yote na hapo Tena mnataka muanzishe upigaji mwingine, Hizo laki tatu mnapeleka zote mifukoni mwenu Kama kawaida yenu
Wewe endelea kutokea macho pesa za join the chain hizo tuna kazi nazo nayo Bado haijafika endeleeni kujichanganya na wizi wenu,mmevuka Kwa kuiba Mali za Umma na kuzifanya kuwa za chama

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Miaka Zaid ya 30 mnaZungumzia habari za viwanja wakati CCM ilishavuka na kupita habari hizo, kweli Chadema imechoka na kupoteza muelekeo kabisa, haina dira Wala muelekeo. Kazi kutafuna Ruzuku na michango yote, Fedha za join the chain mmezitafuna yote na hapo Tena mnataka muanzishe upigaji mwingine, Hizo laki tatu mnapeleka zote mifukoni mwenu Kama kawaida yenu
CCM ina ofisi wewe? hizo zote zimejengwa kwa fedha za umma - CCM ina tuhuma nyingi tu ya uporaji wa mali za umma na kufanya za chama chao.

Mafaili yapo ni suala la muda tu, msifikiri watanzania wamesahau.
 
Miaka Zaid ya 30 mnaZungumzia habari za viwanja wakati CCM ilishavuka na kupita habari hizo, kweli Chadema imechoka na kupoteza muelekeo kabisa, haina dira Wala muelekeo. Kazi kutafuna Ruzuku na michango yote, Fedha za join the chain mmezitafuna yote na hapo Tena mnataka muanzishe upigaji mwingine, Hizo laki tatu mnapeleka zote mifukoni mwenu Kama kawaida yenu
Je CCM ilijenga ofisi zake au ilitaifisha mali za serikali?
 
Ilijenga yenyewe, Kwa hiyo nyie mnataka mjengewe ofisi na nani
Nakujua wewe ni chawa promax wa serkali ya Samia! Ila kwenye kuwaambia ukweli hawa CHADEMA lazima waambiwe tu!

Kwanza chama kilikuwa kinapokea Ruzuku ya mabilioni miaka zaidi ya kumi lakini Hata kujenga ofisi nzuri tu Hata kwa milioni 400 ilishindikana huku Makengeza Mbowe akila hela yote na wapambe wake!

Leo wanapinga kila kitu kinachofanyika na CCM mbaya zaidi Heche akiwa Sengerema anaongea blahblah juu ya Magufuli huku kasahauhata hospital ya Rufaa mkoani kwake ilikwama ujenzi tokea wakati ya Nyerere kaingia Magufuli akafufua ujenzi mpaka sasa Samia kamalizia!

Watu wanaona Matunda ya JPM anaropoka tu ili aonekame anakosoa yaani watu wanashuhudia Busisi ikijenga na Samia naikiwa imeanzishwa ujenzi na JPM wewe unaleta blahblah za kupinga wakati hata ofisi huna! Huyu mkurya Stupid kabisa!
 
Miaka Zaid ya 30 mnaZungumzia habari za viwanja wakati CCM ilishavuka na kupita habari hizo, kweli Chadema imechoka na kupoteza muelekeo kabisa, haina dira Wala muelekeo.

Kazi kutafuna Ruzuku na michango yote, Fedha za join the chain mmezitafuna yote na hapo Tena mnataka muanzishe upigaji mwingine, Hizo laki tatu mnapeleka zote mifukoni mwenu Kama kawaida yenu
kukujibu wewe muhitimu wa chuo kikuu cha mwalimu nyerere pale kivukoni ni kupoteza muda tyuu. huwezi kujibu maswali muhimu. upo kama busha mbele haupo nyuma haupo, NI KASUKU unaitika kila wimbo? ulishawahi fanya utafiti popote pale duniani? unajua chanzo cha kinachoitwa mali za ccm? zilitoka wapi lini na nani walijenga? unalinganishaje mtu mwenye umri wa miaka 40 plus na yule wa miaka 20? kwenye mambo gani, lengo likiwa nini?
chawa ni chawa tu.
 
Nakujua wewe ni chawa promax wa serkali ya Samia! Ila kwenye kuwaambia ukweli hawa CHADEMA lazima waambiwe tu!

Kwanza chama kilikuwa kinapokea Ruzuku ya mabilioni miaka zaidi ya kumi lakini Hata kujenga ofisi nzuri tu Hata kwa milioni 400 ilishindikana huku Makengeza Mbowe akila hela yote na wapambe wake!

Leo wanapinga kila kitu kinachofanyika na CCM mbaya zaidi Heche akiwa Sengerema anaongea blahblah juu ya Magufuli huku kasahauhata hospital ya Rufaa mkoani kwake ilikwama ujenzi tokea wakati ya Nyerere kaingia Magufuli akafufua ujenzi mpaka sasa Samia kamalizia!

Watu wanaona Matunda ya JPM anaropoka tu ili aonekame anakosoa yaani watu wanashuhudia Busisi ikijenga na Samia naikiwa imeanzishwa ujenzi na JPM wewe unaleta blahblah za kupinga wakati hata ofisi huna! Huyu mkurya Stupid kabisa!
Sukuma gang pole.
 
Miaka Zaid ya 30 mnaZungumzia habari za viwanja wakati CCM ilishavuka na kupita habari hizo, kweli Chadema imechoka na kupoteza muelekeo kabisa, haina dira Wala muelekeo.

Kazi kutafuna Ruzuku na michango yote, Fedha za join the chain mmezitafuna yote na hapo Tena mnataka muanzishe upigaji mwingine, Hizo laki tatu mnapeleka zote mifukoni mwenu Kama kawaida yenu
Ccm chama changu ukweli ni kwamba viwanja na majengo nchi zima TULIKwAPUA nahuo ndo uzoefu WETU
 
Miaka Zaid ya 30 mnaZungumzia habari za viwanja wakati CCM ilishavuka na kupita habari hizo, kweli Chadema imechoka na kupoteza muelekeo kabisa, haina dira Wala muelekeo.

Kazi kutafuna Ruzuku na michango yote, Fedha za join the chain mmezitafuna yote na hapo Tena mnataka muanzishe upigaji mwingine, Hizo laki tatu mnapeleka zote mifukoni mwenu Kama kawaida yenu
Mkuu unaifahamu namba yao ya Akaunti naomba uiweke hapa , nataka kuchangia kidogo milioni 3
 
Back
Top Bottom