pmwasyoke
JF-Expert Member
- May 27, 2010
- 4,611
- 3,010
Mkuu,Nimeshaona kwenye platform nyingi, ukitokea mjadala kuhusu ajali barabarani kwa wakimbiaji/wafanya jogging/mazoezi, mara zote shutuma na pia shauri zinazotoka ni kwa wakimbiaji tu. Kwa nini watu hawaoni pia uzembe wa madereva wanasababisha hizo ajali? Kwa nini hazitolewi pia shauri kwa madereva wazembe kuwa makini, kujali watumiaji wengine wa barabara na kufuata sheria? Kwa nini shauri pia hazielekezwi kwa mamlaka husika, hasa Polisi, kuhimiza na kusimamia ufuataji wa sheria za barabarani?
Tatizo hilo haliwezi kutatuliwa na wakimbiaji/wafanya jogging/mazoezi peke yao!!
Kuongezea ushauri uende pia kwa mamlaka za barabara ili kuwe na njia tofauti za waenda kwa miguu.