Jogging pembeni ya barabara zinagharimu UHAI

Kwani lazima mazoezi ya kukimbia yafanyike barabarani tu?
Mtu serious na mazoezi anahitaji nafasi kidogo tu hayo ya barabarani ni show off hakuna kingine.
Wewe sio mkimbiaji,ungekuwa mkimbiaji usinge comment hayo,unakimbia km 15,showoff hapo ni nini,unategemea kila unapokimbia kuna watu,kuna wakati mtu unaamka saa 11 alfajiri hakuna mtu barabarani show off hapo iko wapi...
 
Halafu wadangaji wameshajua huko kwenye maeneo ya michezo including Gyms ndio wakitega mingo za kuwanasa mabwana zinakubali kirahisi sana!

Ni ajabu wanaume nao hawastukii kuwa wanatafutwa kuibiwa na makahaba!

Wanaume mtafuteni Mungu , Mpeni Mungu nafasi kwenye akili na mioyo yenu ili muweze kuishinda dhambi ya uzinzi na uasherati.

Sema sasa wanawapata lakini Mwanaume mjanja akishakula mzigo kwa shilingi 20,000/- akiamza kuombwa hela za kodi, chakula, nauli n.k. Anastukia na kumblock.

Awareness ni kubwa sasa hivi.

Wanawake watafute vibarua vya kujiingizia vipato Kwa jasho Lao wenyewe.

Na Pia kuepuka tamaa.

Umalaya hauna tija.

Utafunuliwa na wanaume wangapi?!
Wake na waume za watu huko gym
Ndy sehemu za kufanya mambo yao

Watu wanabanjuana sana huko

Ova
 
Nchi za wenzetu wanazingatia sana hilo jambo la kuweka sehemu za wazi na za michezo na mazoezi.

Yani watu wa mipango miji Halmashauri hadi mtaani kwa kila mtaa kunakuwa na public places za michezo na mazoezi zinakuwa ni public gardens and free accessible.

Bongo tunakwama wapi?
Bongo maeneo ya wazi wao wanataka kujenga tu ...
Zamani biafra tumecheza sana mpira
Sahv biafra wamewaweka watu wa garage,ni kama sehemu ya uwanja wameukodisha kwa watu

Ova
 
Wanao kimbia barabarani wanafanya Show-Off wanajifanya wazungu Earphones masikioni na mbwembwe nyingine nyingi tu... Unatoka nyumban unaacha jirani yako kuna uwanja wa mpira kwanin usifanyie mazoez hapo..? Ila unataka ukakimbie barabarani dakika 10 urudi home...
ILA UKWELI NI KWAMBA UKIONA MWANAUME ANAKIMBIA KIMBIA JIONI UJUE NGUVU ZIMEPUNGUA ANAJIBUSTI NGUVU ZIRUDI
 
Nimeshaona kwenye platform nyingi, ukitokea mjadala kuhusu ajali barabarani kwa wakimbiaji/wafanya jogging/mazoezi, mara zote shutuma na pia shauri zinazotoka ni kwa wakimbiaji tu. Kwa nini watu hawaoni pia uzembe wa madereva wanasababisha hizo ajali? Kwa nini hazitolewi pia shauri kwa madereva wazembe kuwa makini, kujali watumiaji wengine wa barabara na kufuata sheria? Kwa nini shauri pia hazielekezwi kwa mamlaka husika, hasa Polisi, kuhimiza na kusimamia ufuataji wa sheria za barabarani?

Tatizo hilo haliwezi kutatuliwa na wakimbiaji/wafanya jogging/mazoezi peke yao!!:(:mad:
Jogging hazipaswi kufanyiwa barabarani. Shida sisi si watu wa kuchukuwa tahadhari. Kisha tunamsingiziya mungu.
 
Ndugu zangu wafanya mazoezi pembezoni mwa barabara. Chukueni tahadhari hususani wakati wa alfajiri na jioni/usiku.

Nimepoteza rafiki wawili (mmoja Dar mwingine Mtwara) kwa ajali wakiwa mazoezini. Wameacha familia changa mno.

Wakati mzuri wa kufanya mazoezi ya kukimbia huwa ni asubuhi au jioni, na mida hii mara nyingi kunakuwa na magari mengi sana barabarani, mfano, kuna magari unakuta ana taa moja tu, boda pia ni majanga mara nyingi katika kujihami na magari anakuja mpaka pembeni kabisa kwenye chaki,

Kuna magari yana overtake, hapa nadhani wanaokimbia watakuwa wananielewa nini huwa kinatokea, kuna boda nyingine hazina taa zenye mwanga wa kutosha, kuna wanaotembea na full light unaweza kumulikwa ukopoteza muelekeo,

Kuna boda boda zina beba mizigo mikubwa unaweza kuhisi yuko peke yake kumbe mzigo unatokeza pembeni, ni hatari sana kwakweli, kuweni makini.

Pia, Barabara nyingi sehemu za waenda kwa miguu ndio parking hizo hizo, boda boda humohumo

Vile vile Wakimbiaji wengi hawajali usalama wao barabarani wala kuchukua tahadhari. Unakuta mtu anakimbia akiwa amevaa headphones masikio yote mawili na sauti kaweka hadi mwisho, kiasi cha kushindwa kusikia honi za vyombo vya moto

Kama unaweza bora ukimbie kwenye uwanja maalumu kama wa mpira, ulio karibu na makazi yako kwa kuwa ukiachana na ajali
huo moshi unaovutwa na wanamazoezi huku wanapumulia mdomo ni janga lingine

Kama unalazimika kukimbia barabarani, Kimbia in opposite direction na uelekeo wa magari,,kaa upande wa magari yanayokuja mbele yako

NB: Lipia gym uwe salama
Vijiwe vya bodaboda machinjio mpya jijini
 
Toa constructive criticism, what should they do now?
Ni vizuri kutafita uwanja jirani
Mimi piani mkimbiaji wa pembezoni mwa barabara nimejiongeza hadi sasa navaa reflactor lakini jioni jamaa wanavyorudi toka vibaruani wanawahi home huwa wamekanyaga kweli kweli sasa barabara hizi nyingi ni nyembamba hadi nafikiria sasa ni bora kukimbia kuzunguka uwanja

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom