Jogging pembeni ya barabara zinagharimu UHAI

Nimeshaona kwenye platform nyingi, ukitokea mjadala kuhusu ajali barabarani kwa wakimbiaji/wafanya jogging/mazoezi, mara zote shutuma na pia shauri zinazotoka ni kwa wakimbiaji tu. Kwa nini watu hawaoni pia uzembe wa madereva wanasababisha hizo ajali? Kwa nini hazitolewi pia shauri kwa madereva wazembe kuwa makini, kujali watumiaji wengine wa barabara na kufuata sheria? Kwa nini shauri pia hazielekezwi kwa mamlaka husika, hasa Polisi, kuhimiza na kusimamia ufuataji wa sheria za barabarani?

Tatizo hilo haliwezi kutatuliwa na wakimbiaji/wafanya jogging/mazoezi peke yao!!:(:mad:
Mkuu,

Kuongezea ushauri uende pia kwa mamlaka za barabara ili kuwe na njia tofauti za waenda kwa miguu.
 
Kwa wenzetu Wana pedestrian road(barabara za watembea kwa miguu),na most of them ziko mbali kabisa na barabara kuu,na nyingi zimewekea uzio wa chuma,nothing can cross over,hii ni safe hata kuvaa kwa kua unamkwepa/au mnakwepana na binadam wenzako au pet's si magari.
Kingine asubuhi na jioni ni rush hours kila mtu anawahi either sehemu ya kazi au nyumbani,zaidi kwenye miji mikubwa kwa hiyo si salama kufanya mazoezi sehemu hizi.
Ushauri,ukiweza kwenda kwenye kiwanja Cha mpira/basketball/netball au kama una nafasi kwako fanyia mazoezi humo ukiwa na kwa kujiachia kabisa,au barabara za mitaa.
Na kikubwa kabisa ni Kumuomba Mungu Atulinde katika kila tufanyalo.
 
Tena Maulidi Kitenge, jeshi la polisi na wenzie waonywe.
Viwanja vya mipira ni vingi sna. Sehemu za wazi ni nyingi sna na mapori Tz ni mengi sna ya kufanyia mazoezi. Pia madaktari hushauri watu kufanyia mazoezi chumbani au sebuleni.

Wana leta Jams ktk barabara kisa kupata Sifa tu.
 
Leo wakati natoka kwenye kibarua changu asubuhi nikiwa na rafiki yangu kituo cha vetenary nyuma kulikuwa na kundi la wanajeshi wamevaa nguo za kimichezo truck suit wakikimbia jogging nais ni wa jkt mgulani walitoka upande wa Tazara wakielekea sokota mim na mwenzangu tukavuka upande kutoka kulia kuelekea kushoto yaani kituoni kabisa na kusimama yule mwanajeshi kijana alikuwa kashika bendera nyekundu akiongoza kile kikundi alisimama ghafla na kutuambia rudi mara moja upande tuliotoka akituonesha kwa bendera "rudi haraka kabla sijakasirika atukubisha tukatoka upande wa kituoni na kurudi upande mwingine maana pembeni nliona kulikuwa na madimbwi ya maji lile kundi likapita baadae nikamuhuliza yule jamaa nliyekuwa nae kosa letu nin akasema akuna kosa uo ni ubabe wa kijeshi na tungebisha wangetutia aibu mbele ya abilia waliokuwa wamekaa kituoni
Hii story haihusiki na mada iliyo mezani
 
Wanao kimbia barabarani wanafanya Show-Off wanajifanya wazungu Earphones masikioni na mbwembwe nyingine nyingi tu... Unatoka nyumban unaacha jirani yako kuna uwanja wa mpira kwanin usifanyie mazoez hapo..? Ila unataka ukakimbie barabarani dakika 10 urudi home...
😎 ILA UKWELI NI KWAMBA UKIONA MWANAUME ANAKIMBIA KIMBIA JIONI UJUE NGUVU ZIMEPUNGUA ANAJIBUSTI NGUVU ZIRUDI😂
Mimi siamini kama wote wanaokimbia Barabarani wana show off, pia siamini mtu kwenda barabarani kulimbia 10 min.
Mtu mwenye lengo la dhati la kufanya mazoezi hawezi kufanya hayo unayoyasema.

Kuhusu kukimbia uwanjani pia sikatai lkn kukimbia ni maisha ya kila siku kwa kina sie, je kila siku tutakimbia uwanjani? Jibu ni hapana kwa sababu kukimbia katika mazingira ya aina moja yanachosha. Kuna watu wanakimbia 3hrs- 12hrs, how can u manage kukimbia masaa hayo kwenye eneo moja!

Explore kbl ya kuongea bro!!
 
Mtu akikimbia barabarani aache wosia nyumbani kuepusha ndugu kugombania sabufa na TV nk.
Na aandike anazikwa mjini au anaenda kuzikwa kwao shamba na aache pesa ya mazishi yake?!?
Na kama ana mke aseme kabisa mkewe aolewe na nani?
 
Kama unaweza bora ukimbie kwenye uwanja maalumu kama wa mpira, ulio karibu na makazi yako...ukiachana na ajali
huo moshi unaovutwa na wanamazoezi huku wanapumulia mdomo ni janga lingine
Open space zote tulishaziuza michezo sio kipaumbele chetu,
 
Mimi siamini kama wote wanaokimbia Barabarani wana show off, pia siamini mtu kwenda barabarani kulimbia 10 min.
Mtu mwenye lengo la dhati la kufanya mazoezi hawezi kufanya hayo unayoyasema.

Kuhusu kukimbia uwanjani pia sikatai lkn kukimbia ni maisha ya kila siku kwa kina sie, je kila siku tutakimbia uwanjani? Jibu ni hapana kwa sababu kukimbia katika mazingira ya aina moja yanachosha. Kuna watu wanakimbia 3hrs- 12hrs, how can u manage kukimbia masaa hayo kwenye eneo moja!

Explore kbl ya kuongea bro!!
inaonekana una uelewa mdogo sana wa kufikiri, ngoja nikuache binti yangu
 
Ndugu zangu wafanya mazoezi pembezoni mwa barabara. Chukueni tahadhari hususani wakati wa alfajiri na jioni/usiku.

Nimepoteza rafiki wawili (mmoja Dar mwingine Mtwara) kwa ajali wakiwa mazoezini. Wameacha familia changa mno.

RIP

NB: Lipia gym uwe salama

View attachment 2297135
pole.Hakika si nzur kiafya tunafanyaga tu ila hatari ni nyingi hata moshi wa magari .
 
Acha tupunguepungue tumekuwa wengi mno hadi ukisikia kuna interview ya kazi unaogopa kwenda, nafasi moja ya kz waombaji 1000
 
Back
Top Bottom