Barabara ya Dar Moro “jam ya kufa mtu” inahitaji uangalizi mahsusi

Twin Tower

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
2,133
2,987
Hii barabara kwa sasa haikupi msafiri uhakika wa kufika kwa wakati. Inakubidi walau ujipe hata siku 2 za kuwa barabarani vinginevyo utapanda boda boda.

Jumapili tarehe 12, Nov kulikuwa na ajali ilileta jam iliyozuia magari kwa takriban masaa 6. Hivyo kufanya watumiaji wa kipande hiko wengine kukesha.

Leo ndo, foleni tokea moro hadi dar, sababu kubwa ni ajali na wingi wa malori. Kuna kila dalili ya watumiaji barabara hiyo kutumia masaa 12 kati Dar Moro.

Mapendekezo;
1. Project ya SGR kwa kipande hiko kianze kazi, tusilete danadana hadi miundombinu ianze kuchakaa kabla ya kutumia.

2. Upanuzi wa barabara kwa sasa hauzuiliki, serikali ifanye hivyo hata kwa kiwango cha barabara ya vumbi/changarawe ili iwe inatumika kwa dharura.

3. Matumizi ya reli ya Tazara kwa ajili ya mizigo izingatiwe. Hatuwezi kuwa na maelfu ya malori barabarani huku tukiwa na malori. Malori yatumike kuanzia mpakani huko kama itabidi, pia kwa mizigo ya ndani ya mkoa.

Najua hiyo ni miradi ya watu kuwa na malori, ila binadamu tumeumbwa kujibalilisha kuendena na mazingira.

4. Askari polisi wa barabarani, panapotokea Jam wachukue hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kuzuia malori popote yalipo kuruhusu magar ya abiria na gari ndogo kuendelea na safari wakati ugatuzi ukiendelea.

5. Tanroads wanawajibika kuwa na vifaa vya kuondolea magari yanayopata ajali barabara kwa haraka. Haiwezekani 6hrs mikese tu pakose namna ya kusafisha barabara.

6. Zimamoto wapewe Helkopta za uokoaji kipindi cha ajali ambapo ambulance haiwezi kufika. Hawa wakiambatana na madaktari na wataalamu wa uokoaji watasaidia kuokoa maisha ya watu.

Kama nchi tunachangamoto nyingi, lakini kujali muda na maisha ya watu kutasaidia kuwa na taifa lenye tija zaidi.
 
Mkuu idara hii iondolewe kuwa chini ya police, municipalities ziwe na vikosi vyake vya uokoaji, Lori linaungua chimala kisa hakuna fire engine, ila DC ana V8 ya 500M

Tumejaa ubinafsi. Inahitaji kujitoa kwanza kuboresha maisha ya watu wetu katika kila nyanza ndiyo tuanze kula bata kama hizo.

Ila sasa tunafanya kinyume chake. Bata zinaliwa kwa ahadi ya kuboresha maisha.
 
Back
Top Bottom