Joel Misesemo mwendo umeumaliza lakini...

Joel Misesemo mwendo umeumaliza lakini...

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,441
Reaction score
872,038
.. Umetuachia mijadala na sogozi kila kona!

Wengi hatukukujua kabla na hatutaweza kukujua zaidi ya haya tutakayoyasoma na tunayoyasoma mitandaoni sasa. Umeitwa chizi, umeitwa mpoteza kumbukumbu nknk.. Lakini haupo tena nasi kuweza kutusimulia zile dakika za mwisho wako zilikuwaje?

Kinachonipa shida ni hiki! Kwanini ukaamua kutumia njia hii!? Linaweza kuwa swali la kijinga lakini bado lenye kuhitaji tafakuri

Kwamba ulale kwako vizuri ama ukeshe uamke alfajiri utoke nje uwashe gari uendeshe mpaka makumbusho upande mpaka ghorofa ya 15 kisha ujirushe kwa nia ya kujimaliza? Mbona kama kulikuwa na option za kuondoka hapa duniani bila shida yote hiyo?

Sasa ulipatwa na nini ama ninini kilikupata? Ghorofa ya 15 alfajiri ya jana imebeba majibu yote! Nachelea kuamini shuhuda za mashuhuda! Daktari wa Bernard Membe familia imemkana kumjua na hajawahi kuonekana tena.

Haya ndiyo yanayosemwa sasa kukuhusu, ambayo kabla hayakuwahi kusemwa kwa wengi! Ama kwa wote[emoji1541][emoji1541][emoji1541]

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema linachunguza tukio la kifo cha Mtu aitwae Joel Misesemo Chizi anayekadiriwa kuwa miaka kati ya 35 hadi 40, Mkazi wa Mwananyamala ambaye alijirusha kutoka ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho Kijitonyama na… twitter.com/i/web/status/1…

UPDATES Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kwamba Joel Misesemo aliyejirusha ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza Makumbusho na kufariki dunia hii leo Mei 23, 2023, amejirusha kwa makusudi kupitia dirisha lililopo ghorofa ya saba.

Joel alioa miaka 9 iliyopita na hakubatika kupata Mtoto. Nyuma hapo alipooza upande mmoja wa uso na alikuwa akitumia dawa ambazo tuliambiwa zina 'side effect'ambayo ilimsababishia kupoteza kumbukumbu na kufanya matendo yasiyokuwa ya kawaida"-Reuben, Kaka wa Joel Misesemo… twitter.com/i/web/status/1…


20230524_164910.jpg
20230524_163436.jpg




A scene has a story to tell. Changamoto mpya kwenye uchunguzi, teknolojia mpya inaweza kutatua kitendawili hiki?
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema linachunguza tukio la kifo cha Mtu aitwae Joel Misesemo Chizi anayekadiriwa kuwa miaka kati ya 35 hadi 40, Mkazi wa Mwananyamala ambaye alijirusha kutoka ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho na kufariki.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Marehemu alionekana katika jengo hilo leo tarehe 23, Mei 2023 majira ya saa kumi na moja alifajiri na alimwambia Mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye Msikiti uliopo ghorofa ya 15 dani ya jengo hilo lakini muda mfupi baadaye alijirusha

Jeshi la Polisi limepata gari la Marehemu aina ya Suzuki rangi ya silver lenye namba za usajili T142 DRM lililokuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya magari katika eneo hilo na sasa limehifadhiwa Kituo cha Polisi Oysterbay.

Taarifa ya Polisi imesema camera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani na kufariki ambapo tayari mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.
 
Hii dunia hii, kama kawaida mtu akishaondoka tu, maneno mlima.
Sasa wanasema kwamba alikua na matatizo ya akili....[emoji848][emoji848][emoji848]
Taarifa ya Polisi imesema camera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani na kufariki[emoji848][emoji3064][emoji2827]

CCTV kamera kumbe zina uwezo wa kuonesha nia na mawazo ya mtu? Hapa zilionesha marehemu akijirusha KWA MAKUSUDI
 
Tusema sio akili yake bali ni pepo. Ni kuomba tu hilo pepo lisikuingie. Ila linaweza kusukumizwa kwako na binadamu. Basi ujue maisha ni mchezo, ukirushiwa kipepsi ujue namna ya kukwepa.
Taarifa ya Polisi imesema camera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani na kufariki
 
Taarifa nyingine zinasema gari lake limetambuliwa kwenye Parking ya eneo la Jengo hilo , chizi anawezaje kuendesha gari na aliingiaje kwenye Jengo hilo usiku wote huo ?

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Jeshi la Polisi limepata gari la Marehemu aina ya Suzuki rangi ya silver lenye namba za usajili T142 DRM lililokuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya magari katika eneo hilo na sasa limehifadhiwa Kituo cha Polisi Oysterbay.
 
Ndio maana ninataka kuvunja hili jeshi la police na kuliunda upya.

Jeshi limejaa wazee wengi na vihiyo sasa uchunguzi wa nini wakati wana conclusion tayari, eti kajirusha kwa makusudi!

Na why utawala wa jengo uingilie ile crime scene kwa haraka kwa kusafisha pale?

Elewa mtu anayejirusha mwenyewe lazima atakua ameacha finger prints kwenye dirisha, aliyerushwa kama hakupigana kutakua hakuna finger prints
 
Taarifa ya Polisi imesema camera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani na kufariki
emoji848.png
emoji3064.png
emoji2827.png


CCTV kamera kumbe zina uwezo wa kuonesha nia na mawazo ya mtu? Hapa zilionesha marehemu akijirusha KWA MAKUSUDI
😆😆😆 Wameambiwa na watu waliokuepo kwenye maelezo nao wakasema km walivyoambiwa kwamba amefanya makusudi hajasukumwa na mtu
 
Toka kwa rafiki[emoji1541]
Da Natulia nakutana na habari yako kaka,ndugu yangu,mc kuwa umeondoka

Pole sana kwa Mama yangu Misesemo, pole kwa wanafamilia Wote Joel umeniumiza Sana yaani ulikuwa ndo umefika patamu kwenye Neema na Bland yako kupanda mjini leo umelala tena.

R.I.P Joel Misesemo[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Ukipanda gari/Basi la mkoani ukawaangalia wale jamaa wanaouza mahindi walivyo chini na wewe ulivyo juu kileleni,au tule tugari tudogo tulivyo chini unakaangalia kwa dharau,ndiyo unakuja kugundua ghorofa ya 15 ni zaidi ya kuwa juu.

Katika Hali ya kawaida huwezi kupata ujasiri wa kujirusha kutoka juu kote huko. Ipo namna asee,uchunguzi wa kina ufanyike!!
 
Ukipanda gari/Basi la mkoani ukawaangalia wale jamaa wanaouza mahindi walivyo chini na wewe ulivyo juu kileleni,au tule tugari tudogo tulivyo chini unakaangalia kwa dharau,ndiyo unakuja kugundua ghorofa ya 15 ni zaidi ya kuwa juu.

Katika Hali ya kawaida huwezi kupata ujasiri wa kujirusha kutoka juu kote huko. Ipo namna asee!!
Kwahiyo unataka kutuambia alienda kuimba mapambio msikitini wakaamua wamrushe nje kupitia dirishani?

Unataka umma uonyeshwe CCTV footage ili uamini kwa kuona kwa macho km ile ajali ya mwendokasi?
 
Taarifa ya Polisi imesema camera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka gh
Mkuu wa kilingeni
Tunza sana hizi kauli za awali za polisi.

Nina mashaka sana na haya maelezo ya haraka haraka yasiyotofautiana na yale ya aliyejitambulisha kama daktari wa Membe
 
Back
Top Bottom