MC Joel Misesemo aliyejirusha ghorofani azikwa Kinondoni tarehe 26/05/2023

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
1685188049035.png

Joel Misesemo enzi za uhai wake

Mwili wa MC Joel Misesemo Mkazi wa Mwananyamala ambaye alijirusha kutoka ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho Kijitonyama na kufariki, umezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Polisi Dar es salaam, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Marehemu alionekana katika jengo hilo tarehe 23, Mei 2023 majira ya saa kumi na moja alifajiri na alimwambia Mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye Msikiti uliopo ghorofa ya 15 ndani ya jengo hilo lakini muda mfupi baadaye alijirusha.

Taarifa ya Polisi imesema camera za jengo hilo zilimuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani na kufariki ambapo tayari mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.

Jeshi la Polisi limesema limepata gari la Marehemu aina ya Suzuki rangi ya silver lenye namba za usajili T142 DRM lililokuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya magari katika eneo hilo na sasa limehifadhiwa Kituo cha Polisi Oysterbay.

Soma
- TANZIA - Joel Misesemo afariki dunia kwa kujirusha kutoka ghorofani jengo la Derm eneo la Makumbusho, Dar
 
Back
Top Bottom