JKT ni majanga kama operesheni kimbunga

JKT ni majanga kama operesheni kimbunga

Solution ya changamoto zilizopo National Service sio kuifuta..Ni mambo yanayozungumzika na manageable
 
Tuko wote katika hoja hii!. Naona serikali ina nia njema ila sasa watu waliowekwa kusimamia JKT ndo wanaharibu kwa kufanya mambo yasiyo ya kiungwana. Sasa tunafundisha vijana au tunawatesa vijana?.
Mwisho wa siku mtu akitoka huKo anakuwa na machungu dhidi ya serikali, nchi na saa zingine hata wananchi wenzake badala ya kuwa na huo uzalendo wanaousema!.


Be Good!
 
JKT ni sahihi zaidi tukisema Vijana wetu wanajumuishwa pamoja wanajenga Umoja na Undugu. Uzalendo haujengwi JKT. Ni ushauri wangu kwa Vijana waende huko hakuna jambo lolote la kutisha wala kuogopesha. Ni aibu kijana wa kiume kuonyesha uwoga wako kiasi kwa kuja na hekaya za uwongo eti JKT ni mateso.

Hata baadhi ya mataifa makubwa yaliyo endelea ni lazima vijana wao waende mafunzo kama haya kwa mwaka mzima. Tufike mahali ajira zetu Serikalini na Taasisi zake kama TRA,BOT,TCRA,PPF,nk. sharti moja wapo iwe ni kupita mafunzo ya JKT!
 
Au jkt imegeuzwa na wajanja kama chanzo cha kuingiza pesa mifukoni mwao
ndugu hata ulalamike watu hela wanapiga na dada zenu wataliwa tu hamna namna mbona vyuoni hata mtaani wanaliwa sana au tatizo kuliwa na wajeda labda hilo ndio tatizo
 
Ok my dota atakuwepo intaki hii na ukweli utajianika.
 
hakika watanzania hatupaswi kukurupuka ktk hili jkt ni chombo pekee kitakachofufua uzalendo tuulize tuliotoka huku km tuna

1:element za udini tofauti na secondary schools
2:uvumilivu na ustahimilivu tofauti na zero tolerance in our society
3:ushirikiano km silaha ya mafanikio
4:discipline in all sphere of life
5:ukakamavu phisically n mentally
6:KULINDA Tanzania by any means n any cost...............etc....
hivo hapaswi mtu yeyote kudharau jitihada hz za serikali

NB:1-miundombinu iboreshwe
2:code of ethics izingatiwe na wakufunzi
3;kunahaja kuelimisha wananchi umihimu wa jkt
 
Unaonekana wewe ni mgeni hapa Tanzania toka wazazi wako hawajakuzaa JKT ilikuwepo leo hii ndiyo unakumbuka watoto watafanya ujambazi kwa kuwa ajira hakuna, hao polisi na wanajeshi wanaokamatwa kwa uhalifu hawana ajira au wana ajira kama wanazo kwa nini wanaiba ili hali wako kazini? Hoja yako ni dhaifu kuiaminisha jamii kwamba uhalifu unafanywa na vijana waliotoka JKT wasiokuwa na ajira. TUNGA SABABU NYINGINE

Acha ujima ww JKT imepitwa na wakat haina nafas tena dunia ya leo waliopita huko ndo wameua nchi yetu had leo kwa kupora mali za umma! Rais wetu msikivu tuondolee huo uchafu!
 
Acha ujima ww JKT imepitwa na wakat haina nafas tena dunia ya leo waliopita huko ndo wameua nchi yetu had leo kwa kupora mali za umma! Rais wetu msikivu tuondolee huo uchafu!

Wakati naheshimu maoni yako lakini kwangu mimi naiona JKT kama Taasisi muhimu kuwaunganisha vijana wetu wasomi wanaotoka ktk matabaka tofauti ya maisha,rangi,kabila na kanda ambao wasingekutana na kuishhi pamoja wakila,wakulala na kufanya kazi pamoja bila kuangalia hadhi ya mhusika. Na huko wanajenga urafiki na kutengeneza daraja la kuunganisha Taifa. Mapungufu yajadiliwe lakini siyo kuupuza taasisi hii muhimu ya kujenga taifa moja kwa watoto wetu,wajukuu zetu na watakao wafuata.
 
Nimeziona comment wengine wakiwalilia watt wao kuwa waliteswa sana kulimishwa nk lakini yeyote aliepitia akirudi kwanza wanahadithia yanayoendelea huko pia wapo walioipenda na hata kuamua kujiunga na JWTZ wapo na ninawajua. At least wamejua kuwa kuna maisha kama hayo ambayo watu wanaishi kama umri wao wote ni kulima na kukata kuni tu wamejifunza mengi sana
 
JKT ni sahihi zaidi tukisema Vijana wetu wanajumuishwa pamoja wanajenga Umoja na Undugu. Uzalendo haujengwi JKT. Ni ushauri wangu kwa Vijana waende huko hakuna jambo lolote la kutisha wala kuogopesha. Ni aibu kijana wa kiume kuonyesha uwoga wako kiasi kwa kuja na hekaya za uwongo eti JKT ni mateso.

Hata baadhi ya mataifa makubwa yaliyo endelea ni lazima vijana wao waende mafunzo kama haya kwa mwaka mzima. Tufike mahali ajira zetu Serikalini na Taasisi zake kama TRA,BOT,TCRA,PPF,nk. sharti moja wapo iwe ni kupita mafunzo ya JKT!
Km taifa lipi ndg?
 
Mkuu wangu,hilo la kuangaliwa nyuma ni medical examination..hususani wakiwa wanakucheck for hemorrhoids..JKT ni jeshi pia,ndio maana kuna mafunzo ya mbinu za medani,hivyo swala la kupewa nguo moja nadhani lipo kimafunzo zaidi(nadhani u can imagine hali katika uwanja wa vita inavyokuwa)..otherwise ni kweli kuna changamoto zinazotakiwa kutizamwa hususan mahusiano ya kingono kati ya maafande na makuruta na huduma za afya.
Dogo acha woga,nenda kakomae tu utamaliza tena utafurahia kama mimi nilivyofurahia.By the way umepangiwa kambi gani?
 
Dogo acha woga,nenda kakomae tu utamaliza tena utafurahia kama mimi nilivyofurahia.By the way umepangiwa kambi gani?
Daah we kijana umeona wapi nimeonesha signs za woga..all in all mimi ni afande wako maana ninakuzidi hata namba.Nasisitiza umuhimu wa JKT kwa vijana hususan katika kujenga spirit ya kupenda kazi(fatiki) na ukakamavu wa mwili
 
nimepitia jkt...nililaumu sana nlipopata taarifa za kujiunga, nlipofika kambini maisha yalikuwa magumu sanna..baadaye nlizoea na kulipenda sana jeshi mpaka leo....WENGI mnaocoment negatively hapa hawajapata nafasi hyo ya kujiunga na jeshi...imeiachia experience kubwa ktk maisha..wasichana hawabakwi na hawashurutishwi kufanya mapenzi, wengi wanajilegeza kwa maafande ili ahurumiwe nyakati ngumu...napenda sana program hii
 
Ni bora serikali itafute njia mbadala ya kuboresha elimu ambayo itawezesha vijana kuendana na mbadiliko ya dunia kupata ushindani katika nchi za wenzetu kuliko kukaa na kung'ang'ania jkt isiyo na kichwa wala miguu

ni kweli mkuu haya mambo eti ya kulimishana cjui nini wange buni kitu kina choenda na dunia ya sasa kuanzia chini mwanafunzi akiwa bado mdogo kwa kufundishwa mambo mbalimbali halafu wana chukua tu form six ambao hawafki laki na tuko zaidi ya 40m majority ya form failures wapo mtaani wangeanza na hao kufundishwa vitu mbalimbali na vjana weng walioko mtaani ingepunguza uvivu ila hi ya form six eti uzalendo siafiki the world has changed a lot JKT need to find a new way of helping our nation rather than taking only form six
 
Ok my dota atakuwepo intaki hii na ukweli utajianika.

Think 3 times kama Serikali 3: Tanganyika HURU + Zanzibar HURU = Tanzania HURU = Serikali 3 = 1+1+1=3!!!

Kilichotokea kambi 1 ya JKT last year kuna mabinti kama huyo wako wanakijutia na watakijutia maisha yao yote!!! Ilikuwa siku ya mwisho camp baada ya sherehe ya kufunga rasmi mafunzo, soda na bia kwa wingi tu. Vijana wamepewa vyeti vyao wakaingia kwenye sherehe hadi usiku mrefu!!!

Sherehe kwisha mabinti wakarudi salama bwenini, wakati huo mabasi ya kuwarudisha mjini mapema alfajiri tayari yamepaki uwanjani. Amini usiamini, saa kenda alfajiri baadhi ya maafande wakiwa wamelewa toop wakavamia bweni la mabinti kama huyo wako, walioshindwa kukimbia wakabakwa humo bwenini na waliokimbia nje ili watoe ripoti kwa wakubwa zao wakakwama coz na wao wako mtungi njwiii!!! Wakaishia kulala ndani ya basi kulipopambazuka safari yao ya kurudi mjini ikaanza. Sasa waonee huruma hao mabinti waliobakwa, utamruhusu binti yako???
 
Jkt imeshindwa kufanya jukumu lake la kujenga taifa kwa makusudi imejipa kazi ya kulibomoa taifa,jkt imekuwa ni kituo cha kuwatesa na kuwapiga watu ambapo ilipelekea vifo kwenye baadhi ya kambi,watu wakifika kambini wanavuliwa nguo na kuinamishwa uchi kwa kisingizio cha ukaguzi,huu ni ukaguzi gani unaogeuza sehemu za siri kuwa sehemu za umati wa watu?

Baadhi ya wakufunzi wanatumia nafasi zao kuwatesa mabinti na kuwalizimisha kutoka nao kimapenzi kwa kuwatishia adhabu nzito.

Serikali imeshindwa kuwajali vijana wa JKT watu wakiingia kambini wanapewa shati moja na bukta moja kiasi kwamba wakizifua wanakosa nguo za kuvaa inawabidi wavae nguo mbichi,mpaka sasa nashindwa kuelewa JKT imerudishwa kwa ajili ya kujenga au kubomoa taifa?

Bado huelewi maana ya jeshi hasa jkt
Endelea kukaa na ujinga wako
 
Hayo mafunzo ya kijeshi yanauhusiano gani na nguo?pia serikali inatoa mafunzo ya kijeshi kwa watu ambao wakitoka huko wanakosa ajira,je serikali itamlaumu nani watu hawa wakitoka mafunzoni na kufanya ujambazi na kuwapora watu mali zao?
Serikali haikupi mafunzo ili ikuajiri bali ni kukufundisha stadi mbalimbali za maisha na kukufundisha namna ya kuweza kuishi katika kila hali
Yaaani kunyumbulika.

Ila akili za wabongo zinawaza kuajiriwa tyy
 
Nani kakwambia jeshini unaenda kupiga pamba na kubadili viwalo na kuvaa supra! kwendeni zenu wavivu wakubwa nyie!

tubadili fikra jeshi la wachafu limepitwa na wakati siku hizi mtu kavaa safi anaendesha drone kama kawaida haya mambo ya uchafu, matumizi ya miguvu kama timu isiyo na kocha yamepitwa na wakati, siku hz nguvu kidogo akili nyingi
 
JKT ni sahihi zaidi tukisema Vijana wetu wanajumuishwa pamoja wanajenga Umoja na Undugu. Uzalendo haujengwi JKT. Ni ushauri wangu kwa Vijana waende huko hakuna jambo lolote la kutisha wala kuogopesha. Ni aibu kijana wa kiume kuonyesha uwoga wako kiasi kwa kuja na hekaya za uwongo eti JKT ni mateso.

Hata baadhi ya mataifa makubwa yaliyo endelea ni lazima vijana wao waende mafunzo kama haya kwa mwaka mzima. Tufike mahali ajira zetu Serikalini na Taasisi zake kama TRA,BOT,TCRA,PPF,nk. sharti moja wapo iwe ni kupita mafunzo ya JKT!

kwani ndugu hawa wazee walioko sasa kwenye hizo taasisi mbona walipitia hiyo jkt? Je hali ya ufisadi, rushwa unaionaje?
 
Back
Top Bottom