JKT ni majanga kama operesheni kimbunga

JKT ni majanga kama operesheni kimbunga

Tatizo ni jku(jeshi la kujenga ubakaji),ni serikali ya mwenda wazimu ambayo inaweza kupoteza pesa kwa kutoa mafunzo ya ubakaji,ubakwaji,ukandamizaji na udharirishaji

Chuki zako na matatizo yako binafsi usiyatumie kuitukana,kuidhalilisha JKT. Usiwadhalilishe mama/dada/bint zetu waliopitia JKT kwamba wamebakwa. Kwa mtu aliye pita JKT akisoma posts zako anajua unaandika stori za kusimuliwa mitaani! JKT wanakwenda watu wazima. Waliokwenda huko wanaelewa ni mabint wa aina gani wanaishia kujirahisisha na kutembea na Maafande! Mlee mwanao vema. Asipende short cut,asipende dezo na awe fit kimwili. Hakuna atakaye mbabaisha hapa duniani!
 
Binadamu kama anampenda mkewe au anamtegemea kimaisha, ukimwambia mkeo yuko gest na kajamaa anakuchukia! Reality denial.
 
Nisaidie kunielimisha kwa hali ya matabaka yetu ya kimaisha yalivyo ni wapi vijana wetu watakutana na kujenga daraja umoja? Shuleni na vyuoni haiwezekani kwasababu elimu yetu imetengeneza madaraja kulingana na tabaka za watu. Sasa ni wapi huko utawaunganisha hawa vijana?

JKT ni usanii kama usanii mwingine! Hakuna serikali inayojali kinachoendelea kule, vikufunzi ndo vimepata nafasi ya kuwapata dada zetu na watoto wetu! Huwezi kwenda kulazimisha kufundisha uzalendo huku rushwa na ufisadi vimetamalaki serikalini na kwenye jamii yote! Uzalendo unakuja automatic ikiwa kila mtu atapata haki sawa katika kuyafaidi matunda ya nguvu zake! Huwezi kuaniambia niwe mzalendo wakati mimi nakatwa kodi mpaka almost 30% ya mapato yangu lakini maisha yangu na ndugu zangu hawafaidiki chochote kodi hiyo zaidi ya kutunisha matumbo ya mafisadi na vifisadi vidogovidogo!

Hata mimi nashindwa kuelewa kama ni kujenga uzalendo mbona hawa mafisadi wanaoisumbua nchi walipitia jkt,je uzalendo wao uko wapi?

unaonekana huna hata chembe ya ujuzi wa maswala ya kijeshi haya mengine kama ya nguo moja ni sehemu ya mafunzo tu.kama unataka ukae jeshini kama upo kwa shangazi yako hilo siyo jeshi labda ukawa.

Hayo mafunzo ya kijeshi yanauhusiano gani na nguo?pia serikali inatoa mafunzo ya kijeshi kwa watu ambao wakitoka huko wanakosa ajira,je serikali itamlaumu nani watu hawa wakitoka mafunzoni na kufanya ujambazi na kuwapora watu mali zao?

Ni serikali iliyochoka ndo inaweza kuwaza na kudhani kwamba uzalendo unajengwa kwa kuwatesa watu wake

Hongera kamanda piga vita jkt inayoleta udharirishaji na mateso kwa watu ikidhani ndiyo njia pekee ya kuleta uzalendo,kama ni jkt inajenga uzalendo leo hii tusingekuwa na mafisadi

Mtu hafundishwi kua mzalendo,uzalendo ni asili ya mtu. Pia miezi miwili au mitatu haimfundishi mtu uzalendo. JKT ni mateso,wiki 6 bila kulala,kupalilia toka asubuhi hadi jioni kwa jembe la mkono,hakuna mda wa kuoga wala kupumzika,ni kukesha unaimba,asubuhi unaamkia kulima,daily.

Mbinu za jkt hazina nafasi kwenye ulimwengu wa sasa,zimepitwa na wakati. Wewe unamlimisha mtu kwa jembe la mkono baada ya hapo itamsaidia nini wakati kilimo cha jembe la mkono kinapigwa vita hata na serikali yenyewe,hakina tija,watu wanatumia trekta wewe una mkono utatoka lini?.

Badala wafundishe watu mbinu bora za kilimo cha kisasa wao wanawafundisha kupalilia,tena kwa kuwakomoa kupalilia mchana kutwa.

Jkt mtoto wangu hawezi kwenda labda kama amenishnda kutunza.

JKT waende walioko vijiweni, chukua bodaboda, machinga, na wengine waliokaa kihasarahasara peleka JKT, tena iwe ya kudumu. Hao waliofight mbaka wakatoboa form six waachwe wajiunge JKT kwa hiari. After all philosphers wanapendekeza iron boys ndo waingie jeshini. Sasa hii ya kulazimisha hadi golden boys and girls wakapalilie kwa jembe la mkono ni kuwabrain wash yote waliojifunza shule. Nimalizie kusema, JKT waende watu sahihi siyo hao wanaolazimishwa sasa.

Wanaandaa watu watakaosema ndio kwa kila kitu hata kwa mambo ya kipuuzi.

Wamegundua kuwa hiki kizazi kinachohoji kila kitu kitawaumbua.
 
Majanga,mi nasema kwamba rushwa imeisha tawara tanzania,hii haiwez kuisha kwa maneno hapa tz,sio tu serikalin rushwa hadi oswazi ni nyingi sana,ss hapo rushwa itaisha kweli,itapungua masikion mwa watu na si kuisha,ni mtazamo wangu tu
 
Jeshini mwenye akili ni mkubwa wako. Ndo maana kila siku lazima Usome Order. Bila Order chukua kwanja subiri maelekezo.ukipewa amri yoyote huna haki ya kuhoji ni kutekeleza kama umeonewa lalamika baadae. Inafaida kwa muundo wa jeshi kwani kuna kazi za ovyoovyo zaidi. Askari akipewa fulsa ya kuhoji mnapigwa na adui. Askari ni ngao ya mafisadi wanasiasa kwani hata wakubwa ni wanasiasa pia, aidha wanatarajia fadhira ya wanasiasa, kuna nafasi za ubalozi baadaye!
 
Ambae dada yake kabakwa atoe ushuuda hatutaki uongo wa kipuuzi..nendeni jkt.. wasichana kutoa ngono ni kawaida ata vyuoni ipo..
 
YES she will go;
Na ndo itajulikana mbivu na mbichi.

Think 3 times kama Serikali 3: Tanganyika HURU + Zanzibar HURU = Tanzania HURU = Serikali 3 = 1+1+1=3!!!

Kilichotokea kambi 1 ya JKT last year kuna mabinti kama huyo wako wanakijutia na watakijutia maisha yao yote!!! Ilikuwa siku ya mwisho camp baada ya sherehe ya kufunga rasmi mafunzo, soda na bia kwa wingi tu. Vijana wamepewa vyeti vyao wakaingia kwenye sherehe hadi usiku mrefu!!!

Sherehe kwisha mabinti wakarudi salama bwenini, wakati huo mabasi ya kuwarudisha mjini mapema alfajiri tayari yamepaki uwanjani. Amini usiamini, saa kenda alfajiri baadhi ya maafande wakiwa wamelewa toop wakavamia bweni la mabinti kama huyo wako, walioshindwa kukimbia wakabakwa humo bwenini na waliokimbia nje ili watoe ripoti kwa wakubwa zao wakakwama coz na wao wako mtungi njwiii!!! Wakaishia kulala ndani ya basi kulipopambazuka safari yao ya kurudi mjini ikaanza. Sasa waonee huruma hao mabinti waliobakwa, utamruhusu binti yako???
 
Nisaidie kunielimisha kwa hali ya matabaka yetu ya kimaisha yalivyo ni wapi vijana wetu watakutana na kujenga daraja umoja? Shuleni na vyuoni haiwezekani kwasababu elimu yetu imetengeneza madaraja kulingana na tabaka za watu. Sasa ni wapi huko utawaunganisha hawa vijana?

Wazazi wetu walisha changanywa na vizazi vyetu ni Hybrid tayari,tuangalie what next,kuliko kuwa mawazo mgando katika kipindi hiki tunakakabiliwa na halingmu ya uchumi."is jkt a priority!"
 
. .hile sio private school . .na sio sehemu yakufanya ubishoo. .pale ni kazi tu . .ukitaka kubadilisha nguo . .haina haja yakwenda . .!!
 
Chuki zako na matatizo yako binafsi usiyatumie kuitukana,kuidhalilisha JKT. Usiwadhalilishe mama/dada/bint zetu waliopitia JKT kwamba wamebakwa. Kwa mtu aliye pita JKT akisoma posts zako anajua unaandika stori za kusimuliwa mitaani! JKT wanakwenda watu wazima. Waliokwenda huko wanaelewa ni mabint wa aina gani wanaishia kujirahisisha na kutembea na Maafande! Mlee mwanao vema. Asipende short cut,asipende dezo na awe fit kimwili. Hakuna atakaye mbabaisha hapa duniani!

Mkuu nashukuru kwa ufafanuzi maaana wengi wetu humu tunajadili hisia binafsi zinazotokana na hofu ya hearsay. Binafsi nilikuwa na bias na JKT baada ya kuambiwa habari za mabinti kulazimishwa ngono, jambo ambalo baada ya utafiti nimegundua si kweli ingawa ngono kwa makubaliano binafsi ipo kama ilivyo kwenye taasisi nyingine kama vyuo vikuu. Naamini mafunzo kama yale hasa kwa mujibu wa sheria yanasimamiwa na taasisi mbalimbali hasa usalama wa Taifa hivyo mambo ya ovyo kama ubakaji kutokea ni ngumu japo hatuwezi kusema hakuna wakufunzi wenye utovu wa nidhamu maana hata kwenye majeshi makubwa duniani kama la Marekani wapo askari wanaoshughulikiwa na Court Marshals on gender related issues. JKT ni muhimu kama si lazima.
 
Kama huamini jaribu utazame
 
hii ni kwenda kuanzisha kambi ya ngono tu isiyo na sababu! nadhan watu wa tasaf wapige washike bango ni kuongeza maambukiz yasiyo na ulazima maana uko maporini hata condom nadhan ni adimu kupatikana!!!
 
Mkuu nashukuru kwa ufafanuzi maaana wengi wetu humu tunajadili hisia binafsi zinazotokana na hofu ya hearsay. Binafsi nilikuwa na bias na JKT baada ya kuambiwa habari za mabinti kulazimishwa ngono, jambo ambalo baada ya utafiti nimegundua si kweli ingawa ngono kwa makubaliano binafsi ipo kama ilivyo kwenye taasisi nyingine kama vyuo vikuu. Naamini mafunzo kama yale hasa kwa mujibu wa sheria yanasimamiwa na taasisi mbalimbali hasa usalama wa Taifa hivyo mambo ya ovyo kama ubakaji kutokea ni ngumu japo hatuwezi kusema hakuna wakufunzi wenye utovu wa nidhamu maana hata kwenye majeshi makubwa duniani kama la Marekani wapo askari wanaoshughulikiwa na Court Marshals on gender related issues. JKT ni muhimu kama si lazima.

Tupe sababu za kutufanya tuaminia au ni hawa wala rushwa waliojaa serekalini wanaoitwa ni ma graduate wa jkt pole sana.
 
Back
Top Bottom