JK Rais Bora kuliko wote Tanzania

JK Rais Bora kuliko wote Tanzania

Ni Rais aliyepitia Misukosuko mingi
Ni Rais alikumbana na upinzani mkali
Ni rahisi aliyetoa uhuru wa kwa kila mtu asemalo
Ni Rais alietuletea misaada mingi kutoka kwa wahisani
Ni rahisi ambaye anaongoza katika kipindi kigumu
Ni Rais anayepambana na ufisadi Mf richmond,EPA,nk
Ni Rais anayepambana na wanaofuja mali ya umma
Ni Rais Msikivu na mpokea maoni ya wapinzani

Namtakia kila la heri na kazi yake

ni kweli ni bora ametuweka gizani kupita marais wote
 
Ni Rais aliyepitia Misukosuko mingi
Ni Rais alikumbana na upinzani mkali
Ni rahisi aliyetoa uhuru wa kwa kila mtu asemalo
Ni Rais alietuletea misaada mingi kutoka kwa wahisani
Ni rahisi ambaye anaongoza katika kipindi kigumu
Ni Rais anayepambana na ufisadi Mf richmond,EPA,nk
Ni Rais anayepambana na wanaofuja mali ya umma
Ni Rais Msikivu na mpokea maoni ya wapinzani

Namtakia kila la heri na kazi yake
Huyu nae ndio kaandika matope matupu, nitamjibu huyu wa chini.
Kuzidisha Barabara
Kuzidisha Shule
Kuzidisha afya
Kuzidisha Uchumi
Kuzidisha Demokrasia
Kuzidisha Maji
Kuzidisha Kazi
Kuzidisha Viwanda
Utalii
Kupigana na Rushwa
Kwa haraka haraka hayo hapo juu kafanya kuliko Rais yoyote wa kabla yake.

Naomba Premium members muwe mfano wa great thinking, I thought Premium members title hutolewa kwa watu wanaotumia bongo zao kufikiri kumbe hata wanaotumia nanihii nao wanakuwa premium members. Hayo ya kwenye red ndio aloweza JK.

Kuzidisha Barabara (nampongeza kwa kukarabati barabara alizotengeneza mkapa)
Kuzidisha Shule (zisizo na waalimu wala vifaa vya kufundishia zinazoongeza idadi wa wahitimu wa form four wasio na vyeti)
Kuzidisha afya (
za akina mama kujifungulia kwa wakunga wa jadi, kulala mzungu wa nne hospitali, vituo vya afya kutokuwa hata na panadol)
Kuzidisha Uchumi (
uchumi kwenye mifuko ya akina riz1 labda na FF kwa kuwa wananchi masikini zaidi wanaongezeka)
Kuzidisha Demokrasia (
demokrasia ya kutumia polisi kuvunja katiba kwa kuzuia haki ya watu ya kufikisha hizia zao kwa umma kwa njia ya maandamano na mikutano ya hadhara - kwa ujinga wa kusingizia alshabab)
Kuzidisha Maji (
mpaka leo ni asimilia ngapi ya wanavijiji wanapata maji salama, wangapi wanakufa kwa magonjwa ya kuhara na kuhara damu).
Kuzidisha Kazi (
za kuokota makopo barabarani)
Kuzidisha Viwanda (
du hapa mbona umeongea kinyume FF)
Utalii (
yes hapa amejitahidi mpaka kuhamisha twiga wetu kwenda kuwatangaza arabuni, utalii wa kujuha)
Kupigana na Rushwa
(hili ameweza kwani siku hizi ameacha kununuliwa suti)

 
Na tatizo la umeme hapa linatoka wapi kama hizi statistics ni real. Naomba mama yangu uache ubabaisha kwa statistics mfu zisizofanya kazi

Kumbuka, tatizo la umeme Kikwete kalikuta, kaikuta hii nchi ipo kizani, au umesahau? Hizo statistics unazoziona ni kwa muda wake tu aliokuweo hapa madarakani.

Inafaa uelewe kuwa umeme wa kwenye nchi si kama unaenda kununuwa jenereta leo, unalikuta limekaa linakungoja unalitia mafuta unaanza kutumia. Yeyote anaefikiria hivyo hayuko sawa. Umeme wa nchi ni miradi ya muda mrefu na alichofanya yeye kwa muda mfupi sana kama statistics zinavyoonyesha hapo juu, ni jambo la maajabu makubwa sana, hao wa kabla yake walikuwa wapi? wamelala?

Huna hoja katika hili, Kikwete kafanya tena kafanya kweli kweli. Hizo statistics unazoziona ni za ufuwaji tu wa umeme, bado za usambazaji, nikikuwekea miradi ya umeme yote iliyopo sasa hivi, ukichanganya kuanzia mkoloni, nyerere, mwinyi, mkapa basi hawaipati hata robo ya miradi ya Kikwete anayoifanya kwa miaka yake 6 tu. Nyinyi kaeni na vijiba vya roho na ukweli mnauona.
 
...
Ni Rais alietuletea misaada mingi kutoka kwa wahisani
...
Ni Rais anayepambana na wanaofuja mali ya umma
Ni Rais Msikivu na mpokea maoni ya wapinzani

AMETULETEA MISAADA MINGI KUTOKA KWA WAFADHILI
Imetusadia nini? Itatusaidia kujitegemea au kuwa tegemezi zaidi? Huoni kuwa utegemezi kwa wafadhili umeongezeka. MSIKIVU ANAYEPOKEA MAONI YA WAPINZANI
Maoni kama yapi? Wabunge wake, Spika hawajadili hoja za Wapinzani badala yake wanawabeza? Au JK anaongoza Chama gani?
 
Kuzidisha Barabara
Kuzidisha Shule
Kuzidisha afya
Kuzidisha Uchumi
Kuzidisha Demokrasia
Kuzidisha Maji
Kuzidisha Kazi
Kuzidisha Viwanda
Utalii
Kupigana na Rushwa
Kwa haraka haraka hayo hapo juu kafanya kuliko Rais yoyote wa kabla yake.
Tusiifanye JF iwe kama ze comedy. Hebu tuambie JK amejenga lami mradi mpya km ngapi? Kapigana na rushwa ipi? Hakuna serikali corrupt kama ya Jk. Fuatilia taarifa za kamati za bunge. Kwa rushwa serikali hii inaongoza, inafuatiwa na Mwinyi, Mkapa kwa Mbali
 
To me he is the weakest president ever! Niambie rais gani Africa kwa sasa dhaifu kama JK? Hata ukimuuliza kesho nchi itakuwa wapi hajui. Hana malengo, hana mwelekeo wowote
 
Wewe kwishna kabisa. Ushabiki huu dio uarudisha chi yuma. Badala ya kusema ukweli maishia kujikomba. JK i miogoi mwa marais wabovu duniai chi imemshinda kabisa. Mfumuko wabei wa 18 haujawawahi kutokea, bei ya sukari 2900/= haijawahitokea, bei ya umeme ya 500/= kwa unit haijawahi kufikiwa duniani, nk.
 
Ni Rais aliyepitia Misukosuko mingi
Ni Rais alikumbana na upinzani mkali
Ni rahisi aliyetoa uhuru wa kwa kila mtu asemalo
Ni Rais alietuletea misaada mingi kutoka kwa wahisani
Ni rahisi ambaye anaongoza katika kipindi kigumu
Ni Rais anayepambana na ufisadi Mf richmond,EPA,nk
Ni Rais anayepambana na wanaofuja mali ya umma
Ni Rais Msikivu na mpokea maoni ya wapinzani

Namtakia kila la heri na kazi yake
Nchi imepokea misaada mingi,ndo raisi wake bora!hii ni kali
 
Tatizo la wabongo ni hapa mtu akifanya jambo zuri lazima apewe sifa zake tatizo letu ukisifia mazuri ya CCM basi umekuwa mwanachama,Mimi si mwanachama wa chama chochote ila kikwete is the best Presdaaaaa Utake usitake.Nchi hii tunahistoria nayo ilipotoka siyo kama ilivyo,ni selikali gani iliyopita mawazili wanashtakiwa kwa kutumia madaraka vibaya?

Nina shaka sana na ubongo wako kwenye kufikili

Watu kama nyie huwa mnatamaa sana na madaraka na hiyo inatokana na huenda mna njaa kali sana,sasa mkipewa nchi ndiyo itakuwa balaa zaid

Namshukuru sana JK kwa kuimarisha usalama kila sehemu ili kutulinda wengine ambao hatuna mawazo mgando kama yenu.

Mimi namkubali JK kwa mengi sana aliyoyafanya, namnukuu Mwl Nyerere kwa maneno yake kuwa Tatizo lenu mnaacha mema mnachukua ya kijinga

Kikweteeeeeeeeee oyeeeeeeeeeeeee!!!
Kidumu chama cha mapinduzi

......kachukue kadi aisee......lakini sijui kama utafaulu mafunzo yao.....
 
Zote hizo ni Bomu umeshawahi kusikia nchi yoyote hapa duniani ambayo ilifuata masharti ya IMF na WB kufanikiwa na sera hizo?
Ya kwanza ni Tanzania, wakati tunakubali masharti ya IMF na World Bank, hii nchi ilikuwa nyang'anyang'a, hicho ni kipindi cha Mwinyi alipokea hii nchi kutoka kwa nyerere. Hatuna fedha za kigeni, watu wote ukiwaona taabani hata kandambili hakuna madukani watu tunavaa makata mbuga. Hatuna mafuta, gari hazitembei Jumamosi na Jumapili mpaka kwa vibali, unakwenda vituo vya mafuta unakumbana na foleni, vigari vyenyewe vilikuwa kidoogo na hivyo hivyo vimechakaa kuliko Watanzania wenyewe. Hatuna chakula, kila kaya mnapewa kilo moja ya unga wa manjano kwa wiki, sukari kilo kwa wiki. Nchi imejaa rushwa na vyakula vya magendo vinavyoibiwa NMC, ukionekana umebeba mfuko tu, mgambo hao tayari wamesha kusimamisha. Hata sokoni ukienda nyanya zimesinyaa, zitatoka wapi? hakuna magari ya kuleta kutoka mashamba, mashamba hawalimi, ulime upeleke wapi mazao ukauze?

Nakumbuka hotuba ya Mwinyi alipowaita wazee wa Dar pale Diamond kuwaelezea alivyoipokea hii nchi mara tu baada ya kukabidhiwa, watu walilia machozi na nnakumbuka alipowaita tena baada ya mwaka kuwaelezea kwanini alikubali kukubaliana na IMF, hii ni hotuba inayoitwa "mikuki miwili" nayo ililiza watu, huko ndiko tulikowachiwa na Nyerere. Mengi sana, mengi sana, nikikumbuka nalia.

Leo unauliza ni nchi gani imefanikiwa kwa IMF na WB wakati mfano hai unao? au hukuwepo wakati Mwinyi anakabidhiwa hii nchi? kama hukuwepo ni bora utuulize tukueleze kiutaratibu lakini usikurupuke.
Umewasikia makada wa chama kama Warioba, SAS, Kitine na wengine jinsi wanavyosema kwamba Kikwete anaipeleka nchi pabaya? Sasa nani aaminiwe hapa hawa makada ambao wanayajua mengi ndani ya Serikali na chama chenu cha magamba au tukuamini wewe!?

Hayo unayasema wewe, tubandikie hapa "quotations" zao kiukamilifu ili tujionee wenye walichokisema, tukuamini wewe kama nani? wakati unashindwa kuja na hata kimoja ambacho Kikwete hajakifanya unakuja na fulani kasema hivi, fulani kasema vile. Unanini? nchi inaendeshwa kwa maneno ya Warioba? nchi inaendeshwa kwa kuonesha vitendo na si porojo, hapa barabara hii, mkataba huu, na inajengwa kuanzia sehemu hii kwenda hii siyo nani kasema hiki nani kasema kile, huo ni ujinga. Mtu makini haoneshi maendeleo ya nchi kwa kusema nani kasema. Hao wote unaowataja ni vijiba vya roho kwani wao si ndiyo walikuwa viongozi wa zamani wamekiwacha nini cha kujivunia? foleni za unga wa uji na ugali?
Hapa chini ni baadhi ya shule zetu na hospitali ambazo zinakatisha tamaa na kusikitisha sana na ndiyo maana watoto wa vingunge hawasomi katika shule hizi na wala wao na familia zao hawatibiwi katika hospitali zetu.

Hayo ya mshule ndiyo usiseme kabisa, Kikwete kawachiwa hii nchi ina shule za Sekondari hazifiki 2000 na hizo ni Mkoloni, nyerere, mkapa, mwinyi wote changanya pamoja. Kwa wakati wake tu, zaidi ya shule 5000. hao waliomtangulia walikuwa wapi? leo statistics za shule zinasema 97% ya watoto wa umri wa kwenda shule wana uwezo wa kwenda shule, labda wawe na matatizo mengine, na isitoshe vyuo vikuu 11 kwa wakati wa miaka 6 tu, chuo kimoja tu cha Dodoma kinachukuwa wanafunzi zaidi ya vyuo vyote walivyoacha nyerere, mwinyi, mkapa ukichanganya pamoja, au yote hayo huyaoni?

Hao unaosema watoto wa vingunge, si wakati huu toka mkoloni mpaka leo, kila mzazi aliye na uwezo alipeleka mwanawe shule aipendayo, sema kabla ya mwinyi watu walibanwa na umasikini alioujaza Nyerere, watu wakawa hawana uwezo, baada ya Mwinyi tu tukaanza kuona mashule yaliyotaifishwa mengine yanarudishwa, watu kujenga mashule mapya "ruksa", watu kusomesha watoto zao nje "ruksa", sasa wangoje nini? na Nyerere aliwacha shule nyang'anyag'a hazitamaniki, hata zilizokuwa za mkoloni nzuri na za kupendeza yeye akaziuwa hakuna yenye afadhali, na watu wameshafunguliwa kwa "ruksa" na Al Haj Ali Hassan Mwinyi, wafanye nini> wenye uwezo wakapeleka watoto zao, Ulaya, wengine India, wengine Malaysia, wengine Kenya, wengine USA, wengine Canada, wengine Uganda, almuradi kila mmoja yuko huru, na hao unaowaona wewe walalahoi, huo ndiyo urithi wa Nyerere, alifanya nini miaka zaidi ya 20 aliyotawala kawawacha watu hohehahe.
Usafiri angalia TRC, ATC na hata usafiri wa meli ulivyochoka kutokana na sera mbovu za Kikwete.

Hebu sema kweli kuhusu hili, ATC Kikwete kaikuta hoi bin taabani, TRC kaikuta hoi bina taabani tunaona yeye ndiye anaejitahidi kuzifufuwa sasa hivi, hao walioziacha hoi wakina nani, jiulize? si ndio haohao kina Warioba? haohao waliyoiuwa hii nchi, haohao ndiyo waliyoziuwa hizo. Leo wakati wa Kikwete tunaona Mataka anapandishwa kizimbani, wako wapi wa kabla ya Mataka? ni nani aliyeonesha hata kukemea? kwa hili huna na bado utayaona mengi ya haya madudu yanafichuliwa na Kikwete, kuanzia kina mramba, yona, mahalu na sasa kina mataka na bado anaendelea hajamaliza. Tartiibu, lakini "action speaks louder than words".
Hiyo Elimu shule hazina Walimu au unakuta shule ina Mwalimu mmoja kuanzi la kwanza hadi la saba au sekondari kuanzi form 1 hadi 4 haina Walimu matokeo yake wanaomalia hata kuandika majina yao hawajui,
Umeshajiuliza kwanini hali ikafikia hivyo? au waalimu wanaota juu ya miti? hao wa kabla ya Kikwete walifanya nini kuhusu hilo? hawakufanya kitu ndiyi maana unauona huo uozo, leo tunana Kikwete anajenga vyuo vya walimu kila Mkoa na kwa muda huu mfupi tu wa Kikwete anatowa Waalimu zaidi ya 20,000 ya aliyetowa yeyote wa kabla yake kwa mwaka, haya ni mafanikio makubwa sana, Jee walikuwa wapi wa kabla yake?
hao wachache waliobahatika kumaliza vyuoni hakuna ajira halafu wanaambiwa mjiajiri!!!! Utajiajiri vipi unatoka katika familia ya kimaskini huna hata kianzio cha biashara

Hao unaosema wewe wachache tuambie kabla ya Kikwete walikuwa wengi zaidi au walikuwa wachache zaidi? nnakuhakikishia wakati huu mfupi wa Kikwete anatowa wanafunzi wengi wa chuo Kikuu kuliko wakati mwengine wowote ule, na bado vyuo vinajengwa, hebu kuwa mkweli japo kidogo. Kuhusu ajira na fursa za kujiwezesha zilizopo leo Tanzania huna haja hata ya kusema, tunaona watu wa nchi mbali mali wakizikimbilia hizo fursa, sasa mtu unataka uwezeshwe vipi zaidi ya hivyo, mpaka wageni wanaziona fursa ziliopo, hao waliopo humu ndani hawazioni? Au unataka mtu akae na mfuko wa fedha anawajaza mifukoni ndiyo ujuwe kuna fursa? hilo sahau, hakuna nchi duniani inafanya hivyo, jitume na jitume kwa kasi zaidi. nguvu zaidi na ari zaidi.
Acha hizo banaaa. Hakuna Mtanzania ambaye ana chuki binafsi na msanii Kikwete lakini ikija kwenye utendaji wake lazima ukweli tuuseme kwamba kazi ya kuongoza nchi imemshinda vibaya sana, angekuwa na mapenzi ya kweli na nchi yetu basi angejiuzulu na kuwapisha wenye uwezo wa kuongoza nchi wafanye hivyo.

Hizo kauli zako tu hapo juu zinaonesha ni chuki binafsi, alikufanyia usanii upi? Kikwete ni kiongozi tena mzuri sana na kila utapogusa katika uongozi wake utakuta kafanya zaidi ya yoyote wa kabla yake. kwa kuwa huna la kuonesha kuwa hajafanya vyema ndiyo kwa chuki zako tu binafsi unaanza kumuita majina asiyokuwa nayo, mimi nataka unioneshe kimoja tu, ambacho hajakifanya vyema zaidi ya Rais yeyote usinletee hadithi fulani kasema fulani kasema vile.

Leta hoja hapa usilete chuki zako binafsi, Nnakuhakikishia huna.
 
Haya ni maneno ya Mstaafu SAS na si maneno ya BAK na huyu sidhani kama ana chuki binafsi na Kikwete hata baada ya Kikwete na kundi lake la mtandao kumchafua katika kampeni za 2005:


ANAONYA BILA MARIDHIANO NCHI ITAELEKEA KUBAYA, KITINE ADAI SERIKALI 'INATUPELEKA PABAYA'
Boniface Meena
Mwananchi

MJADALA wa Muswada wa Katiba Mpya umechukua sura mpya baada ya viongozi waandamizi wa Serikali wakiwamo wastaafu, kutaka upatikane mwafaka wa kitaifa kuhusu suala hilo vinginevyo taifa litaelekea kubaya.Onyo la viongozi hao akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa , Dk Hassy Kitine, linakuja ikiwa ni siku chache baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kutaka mwafaka huo wa kitaifa.

Jana, viongozi wakichangia maoni yao katika mdahalo uliondaliwa na Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF), kuhusu nafasi na umuhimu wa katiba katika maisha ya Watanzania, kwa sehemu kubwa walipaza sauti kutaka mwafaka huo ili kunusuru taifa.

Kauli ya Dk Salim
Dk Salim ambaye ni mwenyekiti wa MNH, alisema ni muhimu kuwe na makubaliano na maafikiano katika suala la Katiba Mpya kwa CCM na Chadema.

Alisema, "Chama tawala na chama kikuu cha upinzani vijue tunaangalia mustakhabali wa taifa letu, lazima uelewano uwepo".
Dk Salim alisema kwamba malumbano si mazuri japokuwa ni sehemu ya siasa, lakini akaonya kwamba yasiruhusiwe yakasababisha nchi ikafika pabaya.
"Ninachoomba chama tawala na Chadema wafikirie mwafaka na kuangalia mustakhabali wa taifa, kama hakuna maafikiano si jambo zuri kwa taifa,"alisema Dk Salim ambaye ana uzoefu na utatuzi wa migogoro ya kimataifa.

Sasa hilo gazeti ulilobandika ndiyo unataka kuekeza nini, maana hapo sioni hata kimjoa kinachoelezeam kuwa Kikwete hajajenga barabara zaidim hajajenga mashule zaidi, sijaona. naona ni wazee wanaongea siasa na hao wote walikuwepo kabla ya Kikwete walifanya nini?

Huyo SAS si aligimbea kinyang'anyiro cha Urais na Kikwete? au umesahau ni nani akaibuka mshindi? hao wote si waliwahi kuwa mawaziri wakuu wa hii nchi ni kipi kimoja tu walichokifanya wakati wao ambacho Kikwete hajakifanya zaidi.

Usilete porojo zisizokuwa na mpango kufanya hila za kuharibu mada, kaa kwenye mada, kama unataka kuanzihsa mada mpya fanya hivyo, sisi tupo tutakuja kuchangia.
 
Nasema hivi, mtuwekee takwimu na sababu zenu za kudai kwamba Kikwete "kafanya zaidi" kulingana na dhana na vigezo vya "Mfumo Islamu" ukilinganisha na vile vya "Mfumo Kristo". Kwa kifupi, tunaomba "darsa" kwa nini Kikwete ni bora zaidi ya Nyerere na pengine hata Mkapa kulingana na mtazamo mliyo nao wa "Mfumo Islamu"

Hayo ya mfumokristo kwenye huu mjadala hayamo kama unataka yafungulie nyuzi yake hujakatazwa, hapa upo "wrong number".

 
Nahisi mtoa haja....sorry I mean mtoa hoja na waungaji wake, I hope they are typing under the gun point(an order they cant refuse).
But anyway it depends on how others see things e.g either a glass is half full or half empty thats just a set up o mind.
 
Kuna dada mmoja aliwahi kunambia wapo watu huwa hawaridhiki na wanachopata akatoa mfano kuwa ktk mapenzi mtu hata apewe masaburi na mke wake atatoka tu nje ya ndoa au hatatosheka.sasa hawa wanaobeza nao nadhani ni walewale wasiotosheka na jitihada zilizofanywa na govt ya awamu ya 4.
 
Kuna dada mmoja aliwahi kunambia wapo watu huwa hawaridhiki na wanachopata akatoa mfano kuwa ktk mapenzi mtu hata apewe masaburi na mke wake atatoka tu nje ya ndoa au hatatosheka.sasa hawa wanaobeza nao nadhani ni walewale wasiotosheka na jitihada zilizofanywa na govt ya awamu ya 4.na nina wasiwasi na uaminifu wao ktk ndoa zao.
 
Ni Rais aliyepitia Misukosuko mingi
Ni Rais alikumbana na upinzani mkali
Ni rahisi aliyetoa uhuru wa kwa kila mtu asemalo
Ni Rais alietuletea misaada mingi kutoka kwa wahisani
Ni rahisi ambaye anaongoza katika kipindi kigumu
Ni Rais anayepambana na ufisadi Mf richmond,EPA,nk
Ni Rais anayepambana na wanaofuja mali ya umma
Ni Rais Msikivu na mpokea maoni ya wapinzani

Namtakia kila la heri na kazi yake

.................................................................................
crap.gif
 
Nategemea uje na vigezo mbadala vinavyoendana na "Uislamu" na matakwa ya "Allah", na siyo dhana za "economic statistics" na "comparative statistics" zinazotakana na "intellectual traditions" za "Mfumo Kristo". Kwa kifupi, nategemea ungekuja na vigezo na dhana za "Mfumo Islam" kupima mafanikio na mapungufu ya Alhaji Rais wako "JK."

Watakukuruka sana lakini hii post yako ni ya moto hawawezi kukujibu kwa hoja za maana katika hili mkuu
 
Ongeza na sifa hizi:
Ni Rais wa kwanza tokea tupate Uhuru kutumia muda wake kuzurura ulimwenguni kwa safari zaidi ya 360 ndani ya miaka sita tu ya utawala wake ambazo ni sawa na jumla ya safari walizofanya wenzake woote!
Naona mpaka leo wewe bado unaishi karne zilizopita, hivi unafikiri haya madege yanayovumbuliwa kazi zake ni nini? kama hujuwi, basi kazi zake ni kusafiri pale unapohitaji, leo upo New York kikao cha umoja wa Mataifa kesho upo Dodoma unahidhuria kika cha CCM, jioni yake uko Nairobi unawaoatanisha kina Kibaki na Odinga.Hapo ndipo panakufaa kuelewa kauli mbiu ya Ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Wewe bado una fikra za kijinga kuwa kwenda nje ya Tanzania ni starehe, ondoka kwenye huo ujinga, dunia leo ni kijiji, unakwenda Karikaoo kutafuta nguo zako za kutokea kwenye "kipa imara" ukiona hazifai una vunja jet unaingi Dubai, kesho unarudi jioni upo kwenye "kipa imara" hiyo ndiyo dunia ya leo. Wewe bado upo kule ambapo ikitoka Marangu kuja Dar, kijiji kizima unakiaga na ufanyiwe matambiko na upewe buriani, wapiiiiii? kwisha wakati huo kijana. Ishi katika dunia ya leo, ondoka huko ulikokwama.
Ni Rais wa kwanza 'kuingizwa mjini' kwa kudanganywa na kusaini nyaraka kadhaa nyeti ambazo baadae aligundua kuchomekewa na kuzifuta!
Hayo ni yako tena yanaonyesha upunguwani wako, toto la mujini Kikwete uliinginze mujini? ustake ncheke. Hapo huna kijana, tafuta lingine.
Ni Rais wa kwanza kuchaguliwa kwa kishindo kikubwa katika uchaguzi uliohusisha upinzani lakini ambaye kwa kipindi kimoja tu cha miaka mitano alichokwa karibu na kila mtu hadi ilimbidi kuchakachua ili kubaki madarakani!
Na wale wasimamizi wa ndani na nje ya nchi wooote hawakuona huu uchakachuwaji na magwanda wenzako walishindwa kutuonesha palipochakachuliwa na walishindwa kwenda mahakamani, za Tanzania au nje ya Tanzania. Muone hata haya huna kwa kusema uongo.

Ni Rais wa kwanza kufunga safari kwenda kuomba vyandaruwa na kurejea akijitapa kwamba safari yake imezaa matunda - (Ya kupewa vyandaruwa?)

Tena sana sana, ni nani alifanya hivyo kabla yake? ikazaa vyandaruwa na Tanzania ikawa nchi ya kwanza katika Afrika kumpokea na kuwa mgeni wa Rais wa USA kwa siku nne mfululizo, haijwahi kutokea katika Sfrika ni mara ya kwanza na ndiyo ikapelekea Kikwete pia kuwa Rais wa kwanza wa Afrika kualikwa na Rais mpya wa USA Barack Obama, naona hayo uliyasahau yalikuwa pia ni matunda yaliyoambatana na vyandaruwa million saba, na bush tuliona akienda Arusha kuzinduwa utengenezwaji wake. Hapo nipo na wewe ila nilikukumbusha uliyoyasahau.
Ni Rais wa kwanza kutumia mabavu kuwanyamazisha wanaompinga kwa kutumia Jeshi linaloongozwa na shemeji yake kuwauwa wananchi wengi kwa risasi zaidi ya Rais yeyote aliyemtangulia.
Nadhani umesahau kuwa wakati wa Nyerere alipingwa na jeshi lake na mpka likaja jeshi la Muingereza kumsaidi, kama hujui uliza tarehe 20 wakati wa Nyerere ilikuwa ni nini?Kikwete hatujaona anaempinga tunaona watu wanajitafutia umaarufu wa kisiasa kwa kuandamana kijinga, wakisikia mgeni anakuja wao ndiyo wanajida kundamana mbona wakati hawasikii wageni hawaandamani? watu kama hao ni mkon'oto tu kwa nguvu zaidi mpaka wajifiche chini ya vipaza sauti, unawatowa hukohuko, na wakijidai kuwapeleka mbele mahawara zao kama ndiyo ngao, na wao unawalamba makofi tu. Ndiyo lugha wanayoijuwa.
Ni Rais wa kwanza kushindwa kuchukua hatua dhidi ya vibaka uchumi na mafisadi na ambao yeye mwenyewe pia ni mtuhumiwa.
Kwani hao mafisadi walianzia wakati upi na wakati uoi ndiyi tunaona wakipelekwa mahakamani? au huyaoni? hayo ya ufisadi wa Kikwete mtasema sana lakini hata moja hamna, si mliona fedha za rada? zilikuwa wakati upi na nani akzirudisha? si umeona mramba? alinunuwa ndege wakati upi na nani kamsweka ndani, wengi sana na bado, tena nasikia hivi karibuni kesi ya mwenyekiti wa chama fulani ya kuchota fedha NSSF kabla ya Dau. Dau kaistukia na anaipeleka TAKUKURU ikachunguzwe upya na kuna uwezekano badala ya kuwa kesi ya madai tu kuna kaufisadi kalitendeka ngoja tuone sakata hilo linaishia wapi.

Ni Rais wa kwanza kuiongoza nci kisanii sanii na kwamba analolisema si analolidhamiria.

Huna hoja hapo. Wasanii ni kina Sugu na wale wanaofadhili wasanii pale Katikati ya jiji panaitwaje ile kilabu ya usiku?

Ni Rais mwasisi wa udini, ukabila na umakundi makundi katika chama chake na nchi.

Ndiyo aliyepelekea waumini wakfukuzwa kanisa la Sumbawanaga au umesahau?
Na wengine ongezeni niliyoyasahau, maana ametenda meengi.

Uliyoyasahu, ni mabarabara, mashule, vyuo vikuu, makliniki, uchumi, utalii, demokrasia. Niendelee?
 
Back
Top Bottom