Ya kwanza ni Tanzania, wakati tunakubali masharti ya IMF na World Bank, hii nchi ilikuwa nyang'anyang'a, hicho ni kipindi cha Mwinyi alipokea hii nchi kutoka kwa nyerere. Hatuna fedha za kigeni, watu wote ukiwaona taabani hata kandambili hakuna madukani watu tunavaa makata mbuga. Hatuna mafuta, gari hazitembei Jumamosi na Jumapili mpaka kwa vibali, unakwenda vituo vya mafuta unakumbana na foleni, vigari vyenyewe vilikuwa kidoogo na hivyo hivyo vimechakaa kuliko Watanzania wenyewe. Hatuna chakula, kila kaya mnapewa kilo moja ya unga wa manjano kwa wiki, sukari kilo kwa wiki. Nchi imejaa rushwa na vyakula vya magendo vinavyoibiwa NMC, ukionekana umebeba mfuko tu, mgambo hao tayari wamesha kusimamisha. Hata sokoni ukienda nyanya zimesinyaa, zitatoka wapi? hakuna magari ya kuleta kutoka mashamba, mashamba hawalimi, ulime upeleke wapi mazao ukauze?
Nakumbuka hotuba ya Mwinyi alipowaita wazee wa Dar pale Diamond kuwaelezea alivyoipokea hii nchi mara tu baada ya kukabidhiwa, watu walilia machozi na nnakumbuka alipowaita tena baada ya mwaka kuwaelezea kwanini alikubali kukubaliana na IMF, hii ni hotuba inayoitwa "mikuki miwili" nayo ililiza watu, huko ndiko tulikowachiwa na Nyerere. Mengi sana, mengi sana, nikikumbuka nalia.
Leo unauliza ni nchi gani imefanikiwa kwa IMF na WB wakati mfano hai unao? au hukuwepo wakati Mwinyi anakabidhiwa hii nchi? kama hukuwepo ni bora utuulize tukueleze kiutaratibu lakini usikurupuke.
Hayo unayasema wewe, tubandikie hapa "quotations" zao kiukamilifu ili tujionee wenye walichokisema, tukuamini wewe kama nani? wakati unashindwa kuja na hata kimoja ambacho Kikwete hajakifanya unakuja na fulani kasema hivi, fulani kasema vile. Unanini? nchi inaendeshwa kwa maneno ya Warioba? nchi inaendeshwa kwa kuonesha vitendo na si porojo, hapa barabara hii, mkataba huu, na inajengwa kuanzia sehemu hii kwenda hii siyo nani kasema hiki nani kasema kile, huo ni ujinga. Mtu makini haoneshi maendeleo ya nchi kwa kusema nani kasema. Hao wote unaowataja ni vijiba vya roho kwani wao si ndiyo walikuwa viongozi wa zamani wamekiwacha nini cha kujivunia? foleni za unga wa uji na ugali?
Hayo ya mshule ndiyo usiseme kabisa, Kikwete kawachiwa hii nchi ina shule za Sekondari hazifiki 2000 na hizo ni Mkoloni, nyerere, mkapa, mwinyi wote changanya pamoja. Kwa wakati wake tu, zaidi ya shule 5000. hao waliomtangulia walikuwa wapi? leo statistics za shule zinasema 97% ya watoto wa umri wa kwenda shule wana uwezo wa kwenda shule, labda wawe na matatizo mengine, na isitoshe vyuo vikuu 11 kwa wakati wa miaka 6 tu, chuo kimoja tu cha Dodoma kinachukuwa wanafunzi zaidi ya vyuo vyote walivyoacha nyerere, mwinyi, mkapa ukichanganya pamoja, au yote hayo huyaoni?
Hao unaosema watoto wa vingunge, si wakati huu toka mkoloni mpaka leo, kila mzazi aliye na uwezo alipeleka mwanawe shule aipendayo, sema kabla ya mwinyi watu walibanwa na umasikini alioujaza Nyerere, watu wakawa hawana uwezo, baada ya Mwinyi tu tukaanza kuona mashule yaliyotaifishwa mengine yanarudishwa, watu kujenga mashule mapya "ruksa", watu kusomesha watoto zao nje "ruksa", sasa wangoje nini? na Nyerere aliwacha shule nyang'anyag'a hazitamaniki, hata zilizokuwa za mkoloni nzuri na za kupendeza yeye akaziuwa hakuna yenye afadhali, na watu wameshafunguliwa kwa "ruksa" na Al Haj Ali Hassan Mwinyi, wafanye nini> wenye uwezo wakapeleka watoto zao, Ulaya, wengine India, wengine Malaysia, wengine Kenya, wengine USA, wengine Canada, wengine Uganda, almuradi kila mmoja yuko huru, na hao unaowaona wewe walalahoi, huo ndiyo urithi wa Nyerere, alifanya nini miaka zaidi ya 20 aliyotawala kawawacha watu hohehahe.
Hebu sema kweli kuhusu hili, ATC Kikwete kaikuta hoi bin taabani, TRC kaikuta hoi bina taabani tunaona yeye ndiye anaejitahidi kuzifufuwa sasa hivi, hao walioziacha hoi wakina nani, jiulize? si ndio haohao kina Warioba? haohao waliyoiuwa hii nchi, haohao ndiyo waliyoziuwa hizo. Leo wakati wa Kikwete tunaona Mataka anapandishwa kizimbani, wako wapi wa kabla ya Mataka? ni nani aliyeonesha hata kukemea? kwa hili huna na bado utayaona mengi ya haya madudu yanafichuliwa na Kikwete, kuanzia kina mramba, yona, mahalu na sasa kina mataka na bado anaendelea hajamaliza. Tartiibu, lakini "action speaks louder than words".
Umeshajiuliza kwanini hali ikafikia hivyo? au waalimu wanaota juu ya miti? hao wa kabla ya Kikwete walifanya nini kuhusu hilo? hawakufanya kitu ndiyi maana unauona huo uozo, leo tunana Kikwete anajenga vyuo vya walimu kila Mkoa na kwa muda huu mfupi tu wa Kikwete anatowa Waalimu zaidi ya 20,000 ya aliyetowa yeyote wa kabla yake kwa mwaka, haya ni mafanikio makubwa sana, Jee walikuwa wapi wa kabla yake?
Hao unaosema wewe wachache tuambie kabla ya Kikwete walikuwa wengi zaidi au walikuwa wachache zaidi? nnakuhakikishia wakati huu mfupi wa Kikwete anatowa wanafunzi wengi wa chuo Kikuu kuliko wakati mwengine wowote ule, na bado vyuo vinajengwa, hebu kuwa mkweli japo kidogo. Kuhusu ajira na fursa za kujiwezesha zilizopo leo Tanzania huna haja hata ya kusema, tunaona watu wa nchi mbali mali wakizikimbilia hizo fursa, sasa mtu unataka uwezeshwe vipi zaidi ya hivyo, mpaka wageni wanaziona fursa ziliopo, hao waliopo humu ndani hawazioni? Au unataka mtu akae na mfuko wa fedha anawajaza mifukoni ndiyo ujuwe kuna fursa? hilo sahau, hakuna nchi duniani inafanya hivyo, jitume na jitume kwa kasi zaidi. nguvu zaidi na ari zaidi.
Hizo kauli zako tu hapo juu zinaonesha ni chuki binafsi, alikufanyia usanii upi? Kikwete ni kiongozi tena mzuri sana na kila utapogusa katika uongozi wake utakuta kafanya zaidi ya yoyote wa kabla yake. kwa kuwa huna la kuonesha kuwa hajafanya vyema ndiyo kwa chuki zako tu binafsi unaanza kumuita majina asiyokuwa nayo, mimi nataka unioneshe kimoja tu, ambacho hajakifanya vyema zaidi ya Rais yeyote usinletee hadithi fulani kasema fulani kasema vile.
Leta hoja hapa usilete chuki zako binafsi, Nnakuhakikishia huna.