Haya ni maneno ya Mstaafu SAS na si maneno ya BAK na huyu sidhani kama ana chuki binafsi na Kikwete hata baada ya Kikwete na kundi lake la mtandao kumchafua katika kampeni za 2005:
ANAONYA BILA MARIDHIANO NCHI ITAELEKEA KUBAYA, KITINE ADAI SERIKALI 'INATUPELEKA PABAYA'
Boniface Meena
Mwananchi
MJADALA wa Muswada wa Katiba Mpya umechukua sura mpya baada ya viongozi waandamizi wa Serikali wakiwamo wastaafu, kutaka upatikane mwafaka wa kitaifa kuhusu suala hilo vinginevyo taifa litaelekea kubaya.Onyo la viongozi hao akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa , Dk Hassy Kitine, linakuja ikiwa ni siku chache baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kutaka mwafaka huo wa kitaifa.
Jana, viongozi wakichangia maoni yao katika mdahalo uliondaliwa na Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF), kuhusu nafasi na umuhimu wa katiba katika maisha ya Watanzania, kwa sehemu kubwa walipaza sauti kutaka mwafaka huo ili kunusuru taifa.
Kauli ya Dk Salim
Dk Salim ambaye ni mwenyekiti wa MNH, alisema ni muhimu kuwe na makubaliano na maafikiano katika suala la Katiba Mpya kwa CCM na Chadema.
Alisema, Chama tawala na chama kikuu cha upinzani vijue tunaangalia mustakhabali wa taifa letu, lazima uelewano uwepo.
Dk Salim alisema kwamba malumbano si mazuri japokuwa ni sehemu ya siasa, lakini akaonya kwamba yasiruhusiwe yakasababisha nchi ikafika pabaya.
Ninachoomba chama tawala na Chadema wafikirie mwafaka na kuangalia mustakhabali wa taifa, kama hakuna maafikiano si jambo zuri kwa taifa,alisema Dk Salim ambaye ana uzoefu na utatuzi wa migogoro ya kimataifa.