JK kumpooza Masha na cheo gani?

Salimia dawa ya misuli....anza upya, umesema nini? Hujatoa mchango wako zaidi ya kutoka povu.
 
Salimia dawa ya misuli....anza upya, umesema nini? Hujatoa mchango wako zaidi ya kutoka povu.

Nimekutoa povu??........ Utatukana sana ndugu yangu na kuita majina yooote unayoyajua,, mwisho wake utamaliza vituko. Ukweli unabaki pale pale. You need to grow up na kutoa meaningful ideas na siyo ku crash eti huyu katumwa huyu mwenzetu,,Hiyo mipasho si mngechapisha kanga mukaandika humo? mnabwabwaja kweli kweli,, wanaume tumeumbwa na koromeo la kumeza maneno mengine,,, sasa ninyi mnaongea kila linakuja hata kama halina tija. This is what we call Baloney!
 
Matusi mbona siyo tija? Hivi hamna hoja mpaka muanze matusi na kushambuliana? Halafu mimi nataka kujua kama kuingia leo au jana kama huyo chipukizi aliyeshambuliwa ni dhambi au la msingi ni kutoa hoja zenye mashiko. Kuna watu humu wana maelfu ya thread lakini michango yao ni pumba! Mnalilia uhuru wa kutoa mawazo lakini mnageuka madikteta kwa nini?
 
Kweli JK sikio la kufa....habari hii ni ya uhakika LAU MASHA yuko kwenye list ya wakuu wa mikoa wapya wanaotarajiwa kutangazwa kesho na kapewa Mkoa mpya wa shimiu...

Msibishe wala msinishushue kesho mtaona..

Hakuna neno cause hizi ni nafasi za kisiasa zaidi kuliko kiutendaji, nadhani huko mbeleni ni za kufutilia mbali.
 
Jamani thread kama hizi ni nzuri kwa JF kama zina ukweli. Kwa maana hiyo naomba muendelee kiustaarabu nisi lazimike kumpa ban mtu na kashindwa kuchangia huu mjadala.
 
sasa mbona umefuta hoja yangu wakati haina tusi?
si bora ungefuta hiyo "quote" ukaacha hoja yangu
ambayo nayo ilikuwa inatahadhalisha utumiaji wa lugha
"chafu".

kwa jinsi ulivyo-delete mchango wangu msomaji anawezadhani
nami nilitoa tusi.

Jamani thread kama hizi ni nzuri kwa JF kama zina ukweli. Kwa maana hiyo naomba muendelee kiustaarabu nisi lazimike kumpa ban mtu na kashindwa kuchangia huu mjadala.
 
Ni rafiki yake wa muda mrefu,sishangai.....watang'ooka wote...
 
Kama Lau akiwa ama mkuu wa Mkoa au Wilaya, naanza kuandaa kolomeo langu kwa "zomea zomea"
Maana sipati picha?

Nani anapicha ya kale ka mlembo ka Mweshimiwa ka Manyoni? Kawekeni hapa jamvini mazee!
 
Kama huyo katumwa kwa kuwa kajiunga na jina hilo juzi,, mbona nawe huna miezi 3 humu kwa "Chezo"? Na wewe umetumwa?? Mtu ameuliza swali zuri tu, mlitaka amchague nani mridhike? wewe unadandia treni kwa mbele ati umetumwa?? Nataka nikujulishe tu kwa faida yako na wenzako wa fikra za majitaka kama hizo kwamba, watu humu wamo long time kwa names tofauti. Wengine tangu enzi za Nyenzi.com (sina hakika hata kama unaijua) baadaye wakahamia humu. Na wala wewe si kwako humu, kwa hiyo huwezi kubagua watu,, huyu mwenzetu,, huyu katumwa. Wewe leta hoja na sera acha umbeya.

Embu mtetee kwa ID nyingine tuone ukongwe wako
 
sasa mbona umefuta hoja yangu wakina haina tusi?
si bora ungefuta hiyo "quote" ukaacha hoja yangu
ambayo nayo ilikuwa inatahadhalisha utumiaji wa lugha
"chafu".

kwa jinsi ulivyo-delete mchango wangu msomaji anawezadhani
nami nilitoa tusi.

Cool down wana JF no need for bickering her
 
Bwana Lau si kwamba hafai kwa uongozi...tatizo ni madaraka aliyokua with ref to uwezo wake...perhaps angeanzia chini angekua kiongozi bora siku za usoni...labda ameanzia juu kushuka chini kwa kua kwa maisha ya sasa si lazima kuanza chini kukwea juu unaweza anzia juu kushuka as well
 
Chezo mbona unajihami usishushuliwe aisee, kama kweli ni kweli kama uongo ndo utashushuka bila kushushuliwa.:decision:
 
Kweli JK sikio la kufa....habari hii ni ya uhakika LAU MASHA yuko kwenye list ya wakuu wa mikoa wapya wanaotarajiwa kutangazwa kesho na kapewa Mkoa mpya wa shimiu...

Msibishe wala msinishushue kesho mtaona..

Japo sijakubaliana na ukweli wa jambo lenyewe kwa sababu limekaa kijuujuu lakini hata kama itakuwa hivyo sitashangaa kwa sababu imekuwa ni kawaida ya ccm (si jk pekee) ya kuwa mtu anakataliwa na wananchi kwa kishindo kupitia sanduku la kura halafu bado anarudishwa kwa njia nyingine kuwatumikia wananchi wale wale walioona mtu huyo hawafai. Mamlaka ya rais yanatumika vibaya (kibinafsi zaidi na si kwa manufaa ya umma). Ndio maana tunasema KATIBA MPYA NI LAZIMA.
 
Kama ni hivyo poa tu kaanza na uwaziri then mkuu wa mkoa then atakuja kuwa mkuu wa wilaya next katibu kata ndiyo mwanzo wa kumsahau.
 
Hakuna cha kushangaa, hao ndiyo ana ona wanafaa kwenye orodha yake. Isitoshe lazima afanye hivyo ili aiwekee CCM mazingira ya ushindi kila Mkoa.
Ni miaka minne tu baada ya Katiba mpya mambo yote yataenda sawia.
That is why we need new constitution.
 
Back
Top Bottom