Kuna habari nimeipata kutoka kwa mzee mmoja CCM damu damu na anajua haya mambo vizuri, anasema sheria hairuhusu kumweka mtu aliyeshindwa kwenye jimbo viti Maalumu, halafu Batilda hawezi kuchaguliwa tena coz ameshakaa bungeni miaka kumi na ndo maana alirudi jimboni. Labda apate RC au UBALOZI.
Ukweli nusu, na sehemu kidogo si sahihi.
Viti Maalumu vya upendeleo kupitia akina Mama, Vijana, Wafanyakazi, Vyuo na kadhalika majina yao yamekwishapelekwa kwenye Tume Ya Uchaguzi, mwisho ilikuwa Sept 30. Kwa hiyo, kwa wale ambao majina yao hayamo katika hizo orodha kupitia vyama vyao, basi ki-sheria hawawezi kuvipata hivyo Viti Maalum. (Huku ndiyo yako makorokoro mengi, wake na vimada wa vigogo, watoto wa vigogo, makuwadi, n.k).
Tume ya Uchaguzi inagawa nafasi hizo kufuata uwiano wa wingi wa Wabunge wa kuchaguliwa majimboni. Tume haichagui ni nani apewe na nani asipewe. Kila Chama kiliweka orodha yake kwa mpangilio wa yupi apewe mwanzo, na kuendelea hadi wa mwisho. Kwa maana hiyo ni kuwa Chama kinavyozidi kupata wabunge wengi wa majimbo, basi pia kinazidi kupata wabunge wengi wa viti maalumu, na kinyume chake pia.
Nafasi 10 za uteuzi wa Rais, hizi hazina sheria yo yote isipokuwa utashi wa Rais mwenyewe. Rais anaweza kumpa ye yote apendaye katika hizi nafasi 10. Ila katiba haimpi Rais nafasi ya kumteua mtu kuwa mbunge kwa nafasi 10, na pia kumteua huyo mtu kuwa Waziri au Naibu Waziri. Mawaziri au manaibu wanatokana na wabunge wa majimbo au viti maalumu.
Ugumu kwa Kikwete si kuwa ni nani apewe katika hizo nafasi 10, ila ugumu ni kwa nini fulani apewe na si fulani. Kikwete ana watu lukuki ambao wanasarandia hizo nafasi 10, pamoja na 25 za Ukuu wa Mikoa, na si ajabu kuna ambao wame-ahidiwa tayari baada ya kura za maoni. Kikwete atataka kutumia hizi nafasi 10 (na Ukuu wa Mikoa) si kufurahisha marafiki tu, bali kujaribu kuziba ufa na kutengeneza mustakabari ambao utampa nafasi ya kupumua akiachia madaraka 2015.
Ikumbukwe kuwa Uchaguzi Mkuu wa CCM ni 2012 ambao utatoa picha ni nani anajipanga vipi kwa 2015, na siyo suala la nini au nani alifanya 2005 au 2010.
Masha amekuwa kwenye siasa za ki-Taifa kwa muda wa kama miaka 5 tu, toka kupanda hadi kuporomoka. Hana mizizi iliyokomaa ya ki-siasa ndani ya CCM, Mwanza au mahali popote. Kwa kiasi fulani, utaona kuwa huo si mtaji mzuri kwa Kikwete.
Ikiwa Kikwete ameweza 'kumtosa' Karume na kumkumbatia hasimu wake Billal, pia kawatosa Malecela, Chegeni na Msekela, basi upepo kwa Masha hausharii mema kulinganisha na watu kama akina Marmo, Makamba, Mongela, Karamagi, Kamala, Batilda au hata Mbega, Mwakipesile au Abdulaziz.
Lakini kila mtu na nyota yake, bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.