JK kapotoshwa kuhusu tarehe aliyokuja Nelson Mandela mwaka 1962??

Tukiwa tunaendelea kuangalia funeral rites za Nelson Mandela, mliosikiliza hotuba ya JK ni kwamba kaeleza umati kwamba Mandela alifika Tanganyika kwa mara ya kwanza January 1962. Kwamba safari hiyo alikuja kisiri akipitia Mbeya na kuingia Tanganyika. Kisha akapewa passport ya Tanzania kusafiria.

Hapa ndipo tunaposema viongoziwetu hawapekui vitabu au documents au hata kukumbuka tu. Ukweli ni kwamba histroia haisemi hivyo. Historia inasema kwamba January 1962 ulikuwa ni mweiz mmoja tu tangu Tangayika ijitawale ikiwa na Prime Minister Nyerere. Tukio kuu la kihistoria ni kwamba Huo mwezi karibi wiki mbili zilitawaliwa na NEC ya TANU ambayo ilipomalizika Nyerere akajiuzulu u-Prime Minister na akamuachia Rashid Kawawa.

Gavana-General Richard Turnbull asingeweza kutoa passport Nelson Mandela kirahisi.

Ukweli kuhusu ujio wa Mandela ni kwamba alikuja hapa December 1962, yaani mwaka huohuo, na akawepo kushuhudia Tanganyika ikipata status ya Republic. Hapo ndipo angeweza kupata passport ya Tanganyika na ndicho kilichotokea.

Sikuweza kuamini JK alipokuwa anasoma zile tarehe mbele ya dunia nzima, kwa sababu mtu aliyechimubka historia ya Mandela kokote ilikoandikwa anajua wazi kwamba Mandela alikuja hapa December 1962.

Na hata Mandela kwenye kitabu chake alichoandika kiitwacho A LONG WALK TO FREEDOM, ISBN: 9780349106533, pg. 345: {..we arrived in Dar Es Salaam the next day and I met Julius Nyerere, the newly independent country's firss President..}

Hivyo, wakati ule asingemkuta Nyerere akiwa President, na wakati pekee alipokuwa President ni kuanzia December 09, 1962.

Tuwe tunasoma kabla ya kwenda public.

Ngoja waje wale wa Lumumba bubu 7 uone watakavyotoa mapovu kumtetea 'zao' la chama chao!

Timu nzima imejaa walaghai, watapata wapi muda wa kusoma kuelewa ilhali wanafunzi wakifeli wanalegezewa madaraja ili wafaulu?

Hapo yenyewe kwa blunder hiyo wanatamani historia ibadilishwe,alichotamka JK leo ndio kiwe historia
 
Ila hili tatizo la kufoji document kwa kweli litaendelea kututafuna maana wale wale immigration baada ya kumpa Mandela passport wameona kila kitu kinawezekana sasa wanawapa Wanigeria na Wahindi.
Mkuu,
Ilikua ni kwa nia nzuri lakini naona sasa imekuwa ni ugonjwa....lol
 
Tukiwa tunaendelea kuangalia funeral rites za Nelson Mandela, mliosikiliza hotuba ya JK ni kwamba kaeleza umati kwamba Mandela alifika Tanganyika kwa mara ya kwanza January 1962. Kwamba safari hiyo alikuja kisiri akipitia Mbeya na kuingia Tanganyika. Kisha akapewa passport ya Tanzania kusafiria.

Hapa ndipo tunaposema viongoziwetu hawapekui vitabu au documents au hata kukumbuka tu. Ukweli ni kwamba histroia haisemi hivyo. Historia inasema kwamba January 1962 ulikuwa ni mweiz mmoja tu tangu Tangayika ijitawale ikiwa na Prime Minister Nyerere. Tukio kuu la kihistoria ni kwamba Huo mwezi karibi wiki mbili zilitawaliwa na NEC ya TANU ambayo ilipomalizika Nyerere akajiuzulu u-Prime Minister na akamuachia Rashid Kawawa.

Gavana-General Richard Turnbull asingeweza kutoa passport Nelson Mandela kirahisi.

Ukweli kuhusu ujio wa Mandela ni kwamba alikuja hapa December 1962, yaani mwaka huohuo, na akawepo kushuhudia Tanganyika ikipata status ya Republic. Hapo ndipo angeweza kupata passport ya Tanganyika na ndicho kilichotokea.

Sikuweza kuamini JK alipokuwa anasoma zile tarehe mbele ya dunia nzima, kwa sababu mtu aliyechimubka historia ya Mandela kokote ilikoandikwa anajua wazi kwamba Mandela alikuja hapa December 1962.

Na hata Mandela kwenye kitabu chake alichoandika kiitwacho A LONG WALK TO FREEDOM, ISBN: 9780349106533, pg. 345: {..we arrived in Dar Es Salaam the next day and I met Julius Nyerere, the newly independent country's firss President..}

Hivyo, wakati ule asingemkuta Nyerere akiwa President, na wakati pekee alipokuwa President ni kuanzia December 09, 1962.

Tuwe tunasoma kabla ya kwenda public.

Mkuu umekurupuka vibaya sana, your theory is based on assumptions and you were too lazy not to check the whereabouts of Mandela in December 1962.
To add to what all have said hapo juu kuwa mandela was on his way to Ethiopia for a meeting in February. You base your argument sababu Mandela used the word "president", unakuwa kama wale mashabiki wa timu fulani na mambo yao ya "premier league" na "first division".
Back to the point... Using not the most reliable source(Wikipedia), this will tell you a bit the whereabouts of Mandela in December 1962

"On 5 August 1962, police captured Mandela along with Cecil Williams near Howick.[SUP][117][/SUP] A large number of groups have been accused of having tipped off the police about Mandela's whereabouts including Mandela's host in Durban GR Naidoo, white members of the South African Communist Party, and the CIA, but Mandela himself considers none of these connections to be credible and instead attributes his arrest to his own carelessness in concealing his movements.[SUP][118][/SUP] Of the CIA link in particular, Mandela's official biographer Anthony Sampson believes that "the claim cannot be substantiated."[SUP][119][/SUP] Jailed in Johannesburg's Marshall Square prison, he was charged with inciting workers' strikes and leaving the country without permission. Representing himself with Slovo as legal advisor, Mandela intended to use the trial to showcase "the ANC's moral opposition to racism" while supporters demonstrated outside the court.[SUP][120][/SUP] Moved to Pretoria, where Winnie could visit him, in his cell he began correspondence studies for a Bachelor of Laws (LLB) degree from the University of London.[SUP][121][/SUP] His hearing began on 15 October, but he disrupted proceedings by wearing a traditional kaross, refusing to call any witnesses, and turning his plea of mitigation into a political speech. Found guilty, he was sentenced to five years' imprisonment; as he left the courtroom, supporters sang Nkosi Sikelel iAfrika.[SUP][122]"[/SUP]

Kama utaendeleza uvivu wako hautasoma the rest and utabaki na ubishi wako wa "president", get your facts straight....

Last but not least tembelea website yenye archive ya Nelson Mandela kama nelsonmandela.org. To quote a few:
"..Ruth Mompati goes into exile and becomes secretary and head of Women's section of the ANC in Tanzania.
January 1962
Nelson Mandela secretly leaves South Africa to attend a Pan African Freedom Movement conference in Addis Ababa. He travels to other countries to receive military training and then comes back into the country to continue operating underground...."

Ili kuondoa uvivu wako wakutotafuta hoja before posting soma the rest of the archive ya 1962, link hii -> 1962 - The O'Malley Archives
 
Nikupateje

Tatizo lako ni kudhani kuwa mtu kupata passport ya Tanzania ni mpaka Rais ajue.

Unajua kuna wanaijeria wangapi leo hii wana passport za Tanzania? Je, Rais anawajua wanaijeria hao?

Taarifa za siri nyingine huzijui. Kuwa tayari kujifunza.
 
Mkuu wangu, Akili za kuambiwa si vibaya ukachanganya na za kwako.....

Mbona ukweli uko dhahiri kwamba Nelson Mandela aliingia Tanzania January, 1962 kupitia Mbeya akitokea Lusaka....Na lengo la safari yake lilikuwa ni kwenda Ethiopia kuhudhuria mkutano uliofanyika Februari, 1962....
Hapa unakosa maana kwa kupotosha kama alivyo fanya raisi wa magamba.
Mandela alikuja TANZANIA au TANGANYIKA ?
Pamoja na kuelezea yote hayo bado unajikuta unarudi kulekule kwenye upotoshaji jipange kabla haujaanza kuandika.
 
Hongera kwa kungeza idadi ya post mkuu wangu....

Hivi kulikua na haja ya kuquote hili?

Is this the best you can do?.
 
Nilisikiliza hotuba ya jk ila sikugundua hilo kosa kama lilikwepo. Hata hivyo hotuba ilikua nzuri sana hasa alipotumia nafasi hiyo kueleza mchango mkuu wa tanzania na mwalimu nyerere katika vita vya ukombozi kusini mwa bara la afrika. Pia ilipendeza kumpatia kikongwe wa vita vya ukombozi kaunda heshima ya kutoa hotuba kwenye hadhara hiyo.
 
Utasemaje kwamba Mandela hasingepata passport mwaka 1962 January kwa sababu tu Turnbull hasingetoa hiyo pass. Hii ni ajabu kama si upotoshaji, kwanini passport isitoke na nimemsikia Rais anasema wengi walikuwa wanatumia majina ya Tanganyika akiwemo Mbeki. Nyerere alikuwa akienda UN pass alipewa na nani. Acheni ushabiki wa kitoto. Mandela alikuja January nchini kwa njia za panya on his way to Adiss na asingeweza kufika Adis bila passport
 
Ila hili tatizo la kufoji document kwa kweli litaendelea kututafuna maana wale wale immigration baada ya kumpa Mandela passport wameona kila kitu kinawezekana sasa wanawapa Wanigeria na Wahindi.
Kwa mtazamo wangu, katika hili la forgey rais alipaswa kuminya bila ya kuliongelea.
Maana ilikuwa ni forgery na rais anapoliongelea with prdides lina raise eyebrows, hata kama ni tukio lililopita.
 
Hongera kwa kungeza idadi ya post mkuu wangu....

Hivi kulikua na haja ya kuquote hili?

Is this the best you can do?.
Wewe ulichokiandika unaona kiko sahihi?
Hapa swala sio kuongeza post unapokosea la zima tukuweke sawa, na usigeuze ukweli kuwa uadui.
Siko tayari kukuona ukienda kwenye mlolongo wa wale wanao soma hotuba bila kuipitia.
 
Kwa mtazamo wangu, katika hili la forgey rais alipaswa kuminya bila ya kuliongelea.
Maana ilikuwa ni forgery na rais anapoliongelea with prdides lina raise eyebrows, hata kama ni tukio lililopita.

Huyu jamaa yetu huwa anapitiwa sana, Mandela alikuwa kwenye orodha ya magaidi ya CIA, kwa tafsiri rahisi Tanzania ilikuwa ndio base ya magaidi kama ilivyokuwa Afighanstan ya Muller Omar na Taliban yake.
 
Mleta mada na wachangiaji wengi humu ndani ni kielelezo cha kizazi cha wasomi wa kitanzania wenye sifa kuu ya ukosefu wa adabu kwa kujidhania kuwa wanajua kuliko wengine na pia hawajui kuwa nchi, dunia vilikuwepo kabla yao.
 
Tetea vyovyote uwezavyo. Lakini hapa mwongo ama ni JK au Nelson Mandela, na wala si mleta mada ambaye ni mimi.

Mleta mada angeonekana ana busara kama asingeweka mada yake kwa kujipna anajua zaidi, mbayakwa sababu ya chuki yake na Kikwete alijikita ktk kumdharirisha zaidi kuliko kutaka kujua, na bado kasimama ktk lengo lake, akumbukuke 1962 nchi hii tayari ilikuwa huru. Cheo cha Waziri Mkuu kilikuwa ch muda mfupi sana kuliko cheo cha Urais ktk nchi yetu. Raisi wa Kwanza ni Nyerere hivyo Mandera kuandika kuwa aripokelewa na Rais miaka kadhaa baadaye ni kiyu cha kawaida.
 
Mkuu big up kama umerudi jukwaa hili maana limeoza kabisa, nitafurahi siku nikiona na ujio wa Waberoya.

Jukwaa limejaa mazuzu kibao yani ile radha yake kwisha kabisa.

sio radha,ni ladha.
 
Last edited by a moderator:
Mleta mada angeonekana ana busara kama asingeweka mada yake kwa kujipna anajua zaidi, mbayakwa sababu ya chuki yake na Kikwete alijikita ktk kumdharirisha zaidi kuliko kutaka kujua, na bado kasimama ktk lengo lake, akumbukuke 1962 nchi hii tayari ilikuwa huru. Cheo cha Waziri Mkuu kilikuwa ch muda mfupi sana kuliko cheo cha Urais ktk nchi yetu. Raisi wa Kwanza ni Nyerere hivyo Mandera kuandika kuwa aripokelewa na Rais miaka kadhaa baadaye ni kiyu cha kawaida.

sio kumdharirisha,ni kumdhalilisha.
sio mandera ni mandela.
sio aripokelewa ni alipokelewa.
 
Na ndio maana aljazeera na cnn walimtoa kwenye runinga. Pole mkulu
 
Tukubali tu kwamba JK kanena vizuri suala la kukosea tarehe ni kitu kidogo kulingana na ujumbe alio ufikisha kwa dunia na SA.
Nadhani angesema pumba Wabaya wangefurahia sanaa. hongera jk kwa Kunadi TZ.
 
Naungana na wale wote waliosema ndugu Nitakupataje amekosea, ziara ya Mandela ambayo ki ukweli ilikuwa ziara yake ya kwanza kabisa nje ya SA ilikuwa ni kwenda kuhudhuria mkutano wa PAFMECA uliokuwa ufanyike Addis Ababa Ethiopia mwezi wa February 1962, ANC walipewa mualiko baada ya kuwa kuna chama kimoja cha upinzani (cha weusi wa SA) kilikuwa kimeanza kusambaza propaganda dhidi ya ANC, so ilionekana na lazima Mandela ahuhudhirie ili kusafisha lile wingu jeusi, na kweli ziara ilikuwa ya siri maana Mzee Mandela pia alikuwa anasafiri ili akapate mawazo na mbinu za kuanzisha Umkotho We Sizwe, na plan ya safari ilikuwa aondoke na ndege kutoka Basutuland(Botswana ya sasa) kwenda Dar (Tanaganyika) kupitia Mbeya, plan ilifanikiwa na alipokelewa na ndugu Mwakangale (mjumbe wa TANU pale Mbeya) hiyo ilikuwa ni January 1962 maana aliudhuria mkutano wa PAFMECA February 1962, na wala Mwalimu Nyerere hakumpa passport ila document (kwa maneno yake mwenyewe amesema" because I did not have a passport, I carried with me a rudimentary document from Tanganyika that merey said "This is Nelson Mandela, the citizen of South Africa....(Long walk to freedom page 176). so my President JK yuko sawa!
 
Back
Top Bottom