JK kapotoshwa kuhusu tarehe aliyokuja Nelson Mandela mwaka 1962??

Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
12,709
2,000
Nimeiprnda hii. Rais anatatizo la kutokujiridhisha kabla ya kusaini vitu au kuhutubia. Aliwahi kusaini mswada uliochomekwa vifungu ambavyo havikustahili kuwemo. Aliwahi pia kusema gazeti (MWANAHALISI) limefungiwa kwasababu ya kuchochea vyombo vya dola kuasi wakati silo lililokuwa limeandika habari hizo. Tatizo ni kukosekana kwa ungwana ambapo baada ya kukosea hajui kuomba radhi. Kama hali ndio hivi kwa rais wa nchi tuna haja gani ya kumshangaa Mulugo anayesema Tanzania ni zao la muungano wa visiwa vya Zimbzbwe na Tanganyika mwaka 11964??!!
 
ITEGAMATWI

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
4,739
2,000
Hivi hotuba zake zinaandikwa na MICHUZI eenh?
 
N

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,325
1,250
Penye red hapo,,naona na wewe mtoa mada unabahatisha tu,,huna uhakika.
Kama unajua zaidi ya hili mbona husemi kinachotakiwa kujulikana na wote. Kuhusu passport ya Tanganyika, by January 1962, our citizenship was subject to Queen Elizabeth of Tanganyika!!!!!
 
major mwendwa

major mwendwa

JF-Expert Member
Dec 26, 2011
2,273
2,000
Sijui kwanini tu wepesi sana kutafuta mabaya na mapungufu ya wenzetu...hata pale wanapopatia tunalazimisha kuonekane na mapungufu.
Ndugu hata mimi hili huwa linanitesa sana lakini roho hizi za kutafuta ubaya na kuushupalia siyo roho zenye nia njema hata kidogo
 
Uledi

Uledi

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
583
500
What do you expect from an empty head?
 
sikajiji

sikajiji

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
586
195
Jk ni mvivu kusoma ...
Baba Gaude sina hakika kama JK ni mvivu wa kusoma kwa sababu sina uthibitisho wa kuweza kulisema hili. Ila uhakika nilionao JK si mvivu wa kufikiri lakini kutoka na ulichoandika wewe Baba Gaude nina hakika utakuwa ni mvivu wa kufikiri (a sluggish disposition)
 
Balantanda

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,411
2,000
What do you expect from an empty head?
Akili za kuambiwa , changanya na za kwako.....

Hapa wewe ndio unaonekana empty headed zaidi kutokana na kuchangia kitu usichokijua....
 
Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
10,960
2,000
Mkuu Nikupateje,
Ukikosea jambo unasema nimekosea na ndio uungwana.

Mandela alikuwa anaenda kwenye mkutano wa Pan-African Freedom Movement for East, Central and Southern Africa (PAFMECSA) ambao ulikuwa unafanyika Addis Ababa, Ethiopia mwezi wa pili, 1962. Hiyo disemba yako mzee Madiba alisharudi SA.

Argument yako ina make sense logically lakini haiko sahihi. Mandela alipewa passport ya TZ mwezi January 1962.

In fact Mandela alikamatwa SA tarehe 5 August 1962. kwahiyo hiyo Disemba unayoisema, mzee Madiba alikuwa ndani.
Sidhani kama Mandela aliwahi kupewa Passport ya Tanzania (TZ), bali the then Tanganyika.
 
F

Fitinamwiko

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
4,807
1,500
Tukiwa tunaendelea kuangalia funeral rites za Nelson Mandela, mliosikiliza hotuba ya JK ni kwamba kaeleza umati kwamba Mandela alifika Tanganyika kwa mara ya kwanza January 1962. Kwamba safari hiyo alikuja kisiri akipitia Mbeya na kuingia Tanganyika. Kisha akapewa passport ya Tanzania kusafiria.

Hapa ndipo tunaposema viongoziwetu hawapekui vitabu au documents au hata kukumbuka tu. Ukweli ni kwamba histroia haisemi hivyo. Historia inasema kwamba January 1962 ulikuwa ni mweiz mmoja tu tangu Tangayika ijitawale ikiwa na Prime Minister Nyerere. Tukio kuu la kihistoria ni kwamba Huo mwezi karibi wiki mbili zilitawaliwa na NEC ya TANU ambayo ilipomalizika Nyerere akajiuzulu u-Prime Minister na akamuachia Rashid Kawawa.

Gavana-General Richard Turnbull asingeweza kutoa passport Nelson Mandela kirahisi.

Ukweli kuhusu ujio wa Mandela ni kwamba alikuja hapa December 1962, yaani mwaka huohuo, na akawepo kushuhudia Tanganyika ikipata status ya Republic. Hapo ndipo angeweza kupata passport ya Tanganyika na ndicho kilichotokea.

Sikuweza kuamini JK alipokuwa anasoma zile tarehe mbele ya dunia nzima, kwa sababu mtu aliyechimubka historia ya Mandela kokote ilikoandikwa anajua wazi kwamba Mandela alikuja hapa December 1962.

Na hata Mandela kwenye kitabu chake alichoandika kiitwacho A LONG WALK TO FREEDOM, ISBN: 9780349106533, pg. 345: {..we arrived in Dar Es Salaam the next day and I met Julius Nyerere, the newly independent country's firss President..}

Hivyo, wakati ule asingemkuta Nyerere akiwa President, na wakati pekee alipokuwa President ni kuanzia December 09, 1962.

Tuwe tunasoma kabla ya kwenda public.
Hayo ndio matatizo ya kupeana vyeo kwa kigezo cha fadhila, Nape, Makamba, Malima, Mwinyi, Nchimbi, Mulugo you name. Hawana sifa na watazidi kumuaibisha over and over
 
kyanaKyoMuhaya

kyanaKyoMuhaya

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
1,953
1,225
Yote ni yote kaja 1962, so what? Tunaendelea kuomboleza kwani mnakumbuka alichozungumza Kaunda? Acheni hizo!!
 
Bantugbro

Bantugbro

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
3,913
2,000
Ukweli kuhusu ujio wa Mandela ni kwamba alikuja hapa December 1962, yaani mwaka huohuo, na akawepo kushuhudia Tanganyika ikipata status ya Republic. Hapo ndipo angeweza kupata passport ya Tanganyika na ndicho kilichotokea.
Mkuu,
Nelson alikua anakwenda kwenye Mkutano wa Pan Africanists huko Adis Ababa, mkutano huo ulikua ni February 1962. Alipita Tanganyika mnamo January ya mwaka huo.

Kuhusu paspoti, kumbuka hakupewa kwa jina lake halisi bali alipewa kwa jina la bandia kama Mtangayika.
 
sikajiji

sikajiji

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
586
195
Tetea vyovyote uwezavyo. Lakini hapa mwongo ama ni JK au Nelson Mandela, na wala si mleta mada ambaye ni mimi.
Tuletee sources otherwise we count this information as "Fabricated History"
 
Matola

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,099
2,000
Akili za kuambiwa , changanya na za kwako.....

Hapa wewe ndio unaonekana empty headed zaidi kutokana na kuchangia kitu usichokijua....
Mkuu big up kama umerudi jukwaa hili maana limeoza kabisa, nitafurahi siku nikiona na ujio wa Waberoya.

Jukwaa limejaa mazuzu kibao yani ile radha yake kwisha kabisa.
 
Last edited by a moderator:
N

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,325
1,250
Tuletee sources otherwise we count this information as "Fabricated History"
Inawezekana macho yako hayasomi ninapokuambia kwamba source ni hii: {Nelson Mandela, Long Walk To Freedom, ISBN: 9780349106533, pg. 345}

Kabishane nayo halafu uje hapa useme Mandela alikuwa mwongo au fabricator katika hili.
 
Matola

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,099
2,000
Mkuu,
Nelson alikua anakwenda kwenye Mkutano wa Pan Africanists huko Adis Ababa, mkutano huo ulikua ni February 1962. Alipita Tanganyika mnamo January ya mwaka huo.

Kuhusu paspoti, kumbuka hakupewa kwa jina lake halisi bali alipewa kwa jina la bandia kama Mtangayika.
Ila hili tatizo la kufoji document kwa kweli litaendelea kututafuna maana wale wale immigration baada ya kumpa Mandela passport wameona kila kitu kinawezekana sasa wanawapa Wanigeria na Wahindi.
 
log10

log10

JF-Expert Member
Jul 30, 2013
365
250
Vitu vingine vinatufanya tuonekane mazuzu, kwani rais huwa haipitii kwanza hotuba kabla ya kuisoma hadharani? Sasa washauri wake kazi zao ni nini?
inawezakana kapitia..pengine alifahamu hilo
 
sikajiji

sikajiji

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
586
195
Sa wewe unataka kutueleza nini? Mleta mada amekupa facts za kumfanya Mandela apate Pass ya Tanganyika na ukweli ni kwamba hasingeweza kuipata January 1962 kama alivyosoma JK. PERIOD
Soma nilichoandika. "hasingeweza" na wewe ulikusudia nini? Au kiswahili lugha ya tatu
 
t blj

t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
1,440
2,000
Tukiwa tunaendelea kuangalia funeral rites za Nelson Mandela, mliosikiliza hotuba ya JK ni kwamba kaeleza umati kwamba Mandela alifika Tanganyika kwa mara ya kwanza January 1962. Kwamba safari hiyo alikuja kisiri akipitia Mbeya na kuingia Tanganyika. Kisha akapewa passport ya Tanzania kusafiria.

Hapa ndipo tunaposema viongoziwetu hawapekui vitabu au documents au hata kukumbuka tu. Ukweli ni kwamba histroia haisemi hivyo. Historia inasema kwamba January 1962 ulikuwa ni mweiz mmoja tu tangu Tangayika ijitawale ikiwa na Prime Minister Nyerere. Tukio kuu la kihistoria ni kwamba Huo mwezi karibi wiki mbili zilitawaliwa na NEC ya TANU ambayo ilipomalizika Nyerere akajiuzulu u-Prime Minister na akamuachia Rashid Kawawa.

Gavana-General Richard Turnbull asingeweza kutoa passport Nelson Mandela kirahisi.

Ukweli kuhusu ujio wa Mandela ni kwamba alikuja hapa December 1962, yaani mwaka huohuo, na akawepo kushuhudia Tanganyika ikipata status ya Republic. Hapo ndipo angeweza kupata passport ya Tanganyika na ndicho kilichotokea.

Sikuweza kuamini JK alipokuwa anasoma zile tarehe mbele ya dunia nzima, kwa sababu mtu aliyechimubka historia ya Mandela kokote ilikoandikwa anajua wazi kwamba Mandela alikuja hapa December 1962.

Na hata Mandela kwenye kitabu chake alichoandika kiitwacho A LONG WALK TO FREEDOM, ISBN: 9780349106533, pg. 345: {..we arrived in Dar Es Salaam the next day and I met Julius Nyerere, the newly independent country's firss President..}

Hivyo, wakati ule asingemkuta Nyerere akiwa President, na wakati pekee alipokuwa President ni kuanzia December 09, 1962.

Tuwe tunasoma kabla ya kwenda public.
Nimeipenda sana hii ! Bahati mbaya post zenye kuchambua na kuelimisha kama hizi zinazidi kuadimika JF.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom