JK kapotoshwa kuhusu tarehe aliyokuja Nelson Mandela mwaka 1962??

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,325
1,250
Akisoma hotuba kuhusu maisha ya ndani kabisa ya Mandela wakati wa harakati zake za kupambana dhidi ya utawala wa kidhalimu wa Makaburu nchini Afrika Kusini,Rais Kikwete alisema kwamba Mandela alifika kwa mara ya kwanza nchini Tanganyika mnamo January,1962.Katika kitabu chake cha 'A LONG WALK TO FREEDOM' Mandela alisema kwamba alikuja Tanganyika kwa mara ya kwanza mwaka 1962 wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.Kumbukumbu za kihistoria zinaonyesha kuwa mwezi January,1962 Mwalimu Nyerere hakuwa Rais wa Tanganyika bado,Je ni kweli Mandela alikuja Tanganyika mwezi January,1962 kama alivyodai Rais Kikwete katika hotuba yake au Mkuu aliteleza?
Mkuu,

Kumbe na wewe umeanzisha thread ingawa imeunganishwa na ya kwangu kwa suala lilelile kuhusu uhalisi wa kilichotokea mwaka 1962.

Wachangiaji humu wanaishia kukurupuka bila kupekua vizuri yaliyoyotokea 1962 na hasa hiyo January inayosemwa kwamba Mandela alikuja hapa kisiri.

Ukweli ni kwamba ukifungua ukurasa wa 345 wa kitabu chake ile version ya ISBN 9780349106533, anaeleza kwamba alimkuta President mpya.

Lakini hiyo January watu wanasahau kwamba hapa Tanganyika kulikuwa hakukaliki kwa sababu kuanzia January 16, Kamati kuu ya TANU ilikutana na kukawa na mjadala moto nchini. Joto la mjadala lilikuwa ni kufikiri Tanganyika iwe rpublic na wazungu waondolewe vyeo ili kuwe na Africanazition kamili.

Mjadala ulikuwa mto kiasi kwamba ilibidi mwisho wa NEC Julius Nyerere ali-resign u-Prime Minister na kumuachia Rashid Kawawa.

Hivyo, kuanzia January 16 hadi 22, yaani siku Kawawa anapewa u-Prime Minister kulikuwa na mkutano, na wiki kadhaa kabla kulikuwa na ajenda motomoto kwa ajili ya kiko hiki, tena kukiwa na tetesi kwamba Nyerere hawezi kuisimamia vizuri Africanisatio na hivyo ang'oke madarakani yashikwe na mtu anaywezea kuwaondoa wazungu vyeo.

Haya ni moja ya mazingira yanayotatiza sana kuamini hii January kama Mandela alifika hapa siku hizo.

Sitaki kumsingizia Mandela kwamba alifika hapa hajui kwamba Head of State alikuwa Governor-General Richard Turnbull au kama hakujua kwamba Kawawa alikwau Prime Minister au Nyerere kama ni kweli alikuja hapa hii January.

Kuna jamaa humu anasema kwamba Mandela aliondoka South Africa January 11, 1962. Hizo ni siku tano tu kabla NEC ya TANU haijaanza kikao kilichosababisha Nyerere aondoke madarakani.

Kama alitumia siku kadhaa kwa njia ya kutoroka basi alikuta NEC ya TANU imepamba moto na mjadala ule basi ni wazi alifika hapa akikuta Rashid Kawawa akiwa mkuu wa serikali na wala si Nyerere.

Tutafakari kabla ya kupost na na kuishia kulaumu. Ukiogopa kusema JK ni kapotoshwa basi uogope pia kusema Mandela aliopotoka kuhusu alichoandika kwenye page 345 ya ISBN
9780349106533.
 
Kidzude

JF-Expert Member
Jul 14, 2011
4,431
2,000
Ukweli kwenu ni udini, au siyo? niambie katika niliyoyaandika kipi si ukweli.
Nabii isa ana uhusiano gani na mada, katokea wapi. We ungetoa fact bila kumtuhumu mtoa mada kwa kuhisia kuwa motive yake ni dini?. Sio vizuri aisee just be fair to your heart na Mungu wako.
 
Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,325
1,250
Dada Faizafoxy mimi naendelea kusisitiza si JK wala wasaidizi wake aliyekosea tarehe, kama kuna aliyekosea hapa basi ni huyu jamaa aliyeleta mada, au labda niseme tunatofautiana katika kuelewa kiingereza! Dada Faiza kama unaweza, ingia google download "Long Walk to Freedom: The Autobibliography of Nelson Mandela kimechapishwa na Little, Brown and Company ya USA, fungua Part SIX ya kitabu ina title BLACKPIMPERNEL (ukurasa 158) nenda sehemu ya 46 (ukurasa wa 176) utaupata ukweli wa hii safari na kama JK alikosea au la!
Moderator,

Naomba uweke kwenye post ya juu kabisa hii scan page 345 ya kitabu nilichotumia cha Mandela kuandikia post hii.

Ubishi.JPG

Front cover ya kitabu ni hii nayo nimeamua kuiweka ili

Ubishi_02.JPG
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,314
2,000
Nabii isa ana uhusiano gani na mada, katokea wapi. We ungetoa fact bila kumtuhumu mtoa mada kwa kuhisia kuwa motive yake ni dini?. Sio vizuri aisee just be fair to your heart na Mungu wako.
Huoni kuwa anabambikiwa tarehe ya kuzaliwa? tarehe ya sherehe za kipagani "mtoto" wa Mungu kabambikiwa na hamuoni kuwa mwao? na mada hapo ni tarehe.
 
Kidzude

JF-Expert Member
Jul 14, 2011
4,431
2,000
Huoni kuwa anabambikiwa tarehe ya kuzaliwa? tarehe ya sherehe za kipagani "mtoto" wa Mungu kabambikiwa na hamuoni kuwa mwao? na mada hapo ni tarehe.
For sure you are SICK. Hujui upo nje ya topic kabisa. Just continue with Blassfo
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,314
2,000
For sure you are SICK. Hujui upo nje ya topic kabisa. Just continue with Blassfo
Tarehe tarehe tarehe ndio mada. Kama Kikwete kakosea tarehe kwanini iwe mwao wakati nyinyi mnadanganywa miaka na vikaka kusherehekea tarehe ya sherehe za kipagani mkiaminishwa na wazungu kuwa hiyo ndio tarehe ya kuzaliwa Yesu na nyinyi mpo burdaan wa sharaba. Hivi huoni kuwa ni ujinga huo?
 
kalukamise

JF-Expert Member
May 4, 2011
686
225
mm nimesikia akisema ilikuwa ziara ya siri, je mleta mada hiyo uliyosema ni ziara ya wazi au ilikuwaje? km ilikuwa ya siri basi waliojua ni TANU pekee, lkn sipingani na Maelezo yako bali ufafanuzi unahitajika iwapo ziara uliyoisema nayo ilikuwa siri
hapo usiri ni kwamba, alindoka Afrika ya Kusini kwa siri kwenda Ethiopia kuhudhuria mkutano. Otherwise angekamatwa ndio sababu ya kutafuta passport Tanganyika
 
Bijou

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,193
1,500
Huoni kuwa anabambikiwa tarehe ya kuzaliwa? tarehe ya sherehe za kipagani "mtoto" wa Mungu kabambikiwa na hamuoni kuwa mwao? na mada hapo ni tarehe.
Hivi imani isiyokuhusu, wewe inakusumbua nini? Subiri mabikira kumi ahra
 
KISHOMBO

Senior Member
Jul 19, 2012
198
170
Kwani kitabu kiliandikwa lini? Kwa sababu ujio wa Mandela ulikuwa wa siri inawezekana kabisa kuna mambo mengi ya siri alifanya hatuyajui, kitabu pekee hakitoshi kuibua yote aliyoyafanya. Bravo JK
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,314
2,000
Hivi imani isiyokuhusu, wewe inakusumbua nini? Subiri mabikira kumi ahra
Imani isiyonihusu ni hiyo ya kusherehekea sherehe za kipagani, mnambambikia Mtume wangu Yesu (as) tarehe ya kuzaliwa ambayo haimuhusu ndee wala sikio. Mtume wangu Yesu mtukufu unasema hainihusu? Wewe kweli punguani.

Ni kama vile kusema Kikwete hakuhusu wakati huyo ni Rais wako na hata wakubwa zako wa chama wakiwa na matatizo yao wana mfata Ikulu kuwatatulia. Sasa ukisema hakuhusu si unakuwa punguani.
 
Mtume wako wa kuigilizia? Dini gani ilianza? Punguani ni wewe usiyejua Muumba alianzisha dini gani ya kwanza duniani
 
mondinho

Member
Aug 16, 2010
11
0
Ha ha ha ahahaa.......but the basic thing is that the late Madiba didnt specify the exact date, but said he met with first president of Tanganyika, na ndio fact ambayondugu yetu amesimamia. mpaka hapo my brother u have no solid fact. ukweli ni kwamba JK was right na wewe upo chaka
 
Kilembwe

JF-Expert Member
Aug 19, 2009
1,208
1,500
VItabu vina unique code iitwayo ISBN. Nilidhani ubishi ungeisha kwenye post yangu ya kwanza na ndiyo maana niliweka ISBN nikijua na-argue na watu wanaoelewa nini maana ya ISBN.

Nikufundishe kitu kimoja, kama ukitaja ukurasa wa kitabu chochote basi lazima utaje ISBN yake maana inawezekana unazungumza edition ya zamani ambayo lazima ISBN ni tofauti.
ISBN number ya kitabu nilichosoma kwenye mtandao ni 0-316-54585-6 kimechapishwa na Little, Brown and Company ya USA!
 
asagulaga

Member
Feb 8, 2010
86
95
Katika kesi yake iliyofanyika mwezi july 1962, Mandela alishatembelea tayari Tanzania. Kama unahitaji kujua na kuelewa fact hiyo basi pitia link hii: Nelson Mandela's First Court Statement - 1962 - The O'Malley Archives
Sehemu mojwapo anaeleza alikutana na Kawawa akiwa prime minister wa Tanganyika, alikutana na Nyerere ambaye hajataja wadhifa wake wakati huo. Vile vile alikutana na viongozi wengine wa Afrika wakati huo. Si vizuri sana kumshushia hadhi rais wa nchi yetu mbele ya watu wengine wanaosoma mtandao huu inaonyesha kuwa sisi siyo great thinkers kama tunavyowaza.
Huyo ndiyo rais wetu anayewakilisha watanzania wote. Ni alama mojwapo kuu ya taifa kwa wakati huu. tusifanye mambo kama watu wahuni.
 
Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,325
1,250
VItabu vina unique code iitwayo ISBN. Nilidhani ubishi ungeisha kwenye post yangu ya kwanza na ndiyo maana niliweka ISBN nikijua na-argue na watu wanaoelewa nini maana ya ISBN.

Nikufundishe kitu kimoja, kama ukitaja ukurasa wa kitabu chochote basi lazima utaje ISBN yake maana inawezekana unazungumza edition ya zamani ambayo lazima ISBN ni tofauti.
ISBN number ya kitabu nilichosoma kwenye mtandao ni 0-316-54585-6 kimechapishwa na Little, Brown and Company ya USA!

Edition unayotumia kwa hiyo ISBN 0-316-54585-6 ni ile first edition iliyotoka 1994 (Click here), hivyo ISBN yangu (9780349106533) ni the latest kwani ni edition of 1996 (Click here), yaani miaka miwili baada ya edition unayotumia. Kumbuka succedding editions hutoka baada ya kurekebisha virgin editions!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom