Wadau
Sio kila kitu wadau ni uchawi mengine ni mila na desturiu zetu waafrika,tusiwe na huo mnaoita ustaarabu wa kizungu mpaka tukapitiliza.Nachojua hata wazungu wana mila na desturi zao.Waamerika weusi wanadestuuri zao japo walichukuliwa utumwani lakini hawakuacha na walianzisha SOUL FOOD.
Tukipitilza tunakuwa WATUMWA wa UTAMADUNI,asiyefuata ASILI ni MTUMWA.Mwalimu na usomi wake na kuongoza Taifa hili alijua kuwa kuna MUNGU WA WATYAMA pale BUTIAMA.Wazee wa Dar e Salaam pia walimuombea kwenye matambiko yao wakachinja MBUZI wakamwambia TAMBUKA [Maana yake luka au vuka] wakamwambia nenda sasa gavana TWAIN amekwisha HAKUWEZI TENA.
Tusifike mbali tukawa Watumwa mpaka kusahau kwetu,ndio JK anamatatizo ya utawala wake, lakini hata kwa hili tusifikie kuwa na dhiaki mpaka kwenye JADI tutakuwa watumwa kupitiliza.Ni kweli tu Watumwa KIUCHUMI lakini tukishadadia na hili hata hicho kidogo kinachotupa picha ya kuwa tu wa Watanzania kitapotea na tutakuwa tu wanyama tusiojua tunakotaka au tunakwenda.
Wachaga wanachinja mbuzi wakienda vijini kwao [Migombani] wakurya wanachinja mbuzi wakienda kwa kijijini [Itongo] wasukuma na wanyamwezi wanachinja mbuzi wakienda vijiji mwao [Mwiitongo].
Tujadiliane jinsi gani tunafanikisha kuludisha uchumi wa Mtanzania uliopokwa na kuuludisha mikononi mwa vijana kizazi cha Taifa hili.Haya ya kuchinja mbuzi na kunywa toga ua mbege mimi na UDOTCOM wangu nimeyakuta kwenye familia yangu nanitaendeleza kama jadi ya jamii yangu kama walivyoendeleza waamerika weusi kwenye SOUL FOOD [Soul food is used to refer to the kind of food, for example corn bread, ham, and greens, that was popular with black Americans in the southern United States and is considered typical of them.].
Wadau yakitanzania yaendelee kuwa ya kitanzania.tuzungumze tulivyopokwa uchumi wetu na maliasili yetu na ni jinsi gani tutalejesha tulivyopokwa. Tumuache yeye na wanamsoga wenzie waeendeleze na kuenzi jadi ya utanzania wao kwa mila zao kama Nyerere alivyoishi na Watyama wa kwao Butiama.Tukiyachokoza haya tutakuwa kama Mazuzu vile.