Uchambuzi huru: Katika hili, Rais Samia kajitahidi kuliko wote

m2mixh

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2017
Posts
662
Reaction score
429
Naingia moja kwa moja.

Kila awamu ina mazuri na madhaifu yake. Leo ntaeleza kwa kifupi mazuri machache ya Kila awamu na madhaifu angalau moja.

*JK I – Amefanikiwa sana kutuweka pamoja Watanzania. Kama kuna mtanzania anazungumzia udini, ukabila au ukanda, atashambuliwa kutoka Kila kona, hata kutoka kwa watu wa imani yake. Ni jambo la kujivunia saanaaa. Udhaifu ni pale ambapo alitambua katiba hii haiko sawa na kuiacha ingawa alikuwa na fursa ya kuirekebisha.

*A.H. MWINYI – Aliikuta nchi ina hali ngumu sana. Watu walikuwa wakipanga foleni kununua sukari kwenye maduka ya ushirika, yeye akaruhusu bidhaa za nje ziingie. Hilo lilisaidia saaanaa. Udhaifu ni pale aliporuhusu wafanyabiashara kuingiza bidhaa nje, wengine wakatumia fursa hiyo kujinufaisha binafsi na kuiumiza serikali (Hili alilisema mwenyewe kwenye kitabu chake).

*BEN MKAPA – Kiukweli nchi ilianzia kwake. Alianzisha organs nyingi za serikali ambazo hata sasa ndizo mihimili ya nchi. Udhaifu ni pale ambapo alihadaiwa na wakuu wake wa ulinzi, machafuko yakatokea kule Zanzibar (Ameliongea kwenye kitabu chake).

*JK II – Huyu Mimi namwita Father of democracy wa Tanzania. Ingawa Tanzania tuna tatizo la democrasia na utawala bora, lakini katika maraisi wote hadi Leo (sijui mbeleni ktk awamu hii), hakuna kama Kikwete katika uwajibikaji, democrasia, uhuru wa kujieleza, kuheshimu mihimili ya dola, ujenzi wa barabara. Hakuna raisi aliyejenga barabara kama Kikwete. Huyu ni role model wangu katika uvumilivu.

Mengi yanayotokea ambayo yanalalamikiwa sana kama utekaji, kubambikiwa kesi, n.k, ni uhalisia kuwa moyo wa JK wa pili sio wangu au wako. Uvumilivu ni karama kutoka mbinguni. Lazima tumpe maua yake kabla hajafa.

Mimi ni mwalimu, mwanafunzi aniambie “mwalimu wewe ni mpuuzi sana” tena mbele ya wenzake, sijui itakuwaje kwa kweli. Lkn Kikwete aisee!! JK wa pili alikuwa anasikiliza sana wananchi wanataka nini. Wakisema waziri huyu hatumtaki kwa tuhuma hii na hii, anamtoa.

Anayo mengi sana mazuri huyu mtu kama utamtazama kwa jicho huru. Najua wenye chuki watasema huyu jamaa ni fisadi, hilo siwezi kulizungumzia maana napata ukakasi. Kama ni kweli alikuwa fisadi basi ana akili sana.

Kwa nini nasema hivi! Mfano; mimi ni mwizi, nawezaje kumtafuta mtu achunguze wizi wangu halafu aumwage hadharani? Je, wewe unaweza?

Kila mtu anamkumbuka CAG wa muda wote, CAG MUSSA ASAD. Yule mzee ni mkweli sana yule. Alikuwa anaweka hadharani Kila uovu katika serikali ya JK wa pili. Waandishi walipomhoji kwa nini anaidhalilisha serikali, yeye akajibu; “aliyeniteua ndiye anayeniambia nifanye hivi”.

Aliyemteua ni nani? Ni JK wa pili. Huyu CAG alipokuja JPM aliamua kuendelea nae. JPM alijipambanua kwa wananchi kama raisi anayechukia rushwa, ufisadi, uonevu, na ni mkweli. Mussa Asad akaona yes, kumbe niendelee, maana huyu naye kumbe yupo kama mimi, ni mkweli.

Alipotoa ripoti yake ya kwanza tu, tirioni 1.5 zimepigwa! JPM akaona huyu hapana, akamtoa. Sasa hapo wenye D mbili wameshaelewa kutofautisha maneno na vitendo. Ukisema wewe ni mkweli, lazima ukubali kufanya kazi na mkweli.

Udhaifu wa JK wa pili ni huu; Aliweka washikaji zake kwenye maeneo mengi kiasi kwamba wakati Mwingine alikosa maamuzi ya moja kwa moja. Na hilo la ushikaji mimi siwezi kumlaumu. Hata kama ningekuwa mimi kwa kweli ningefanya hivyo. Hilo lipo kwa kila mtu, labda kama yupo aliyezaliwa, kukua, kusoma bila kuwa na washikaji.

*JPM – Maraisi wote hadi huyu mama ni wazalendo, ila mwamba JPM ni noma. Kiukweli nchi za magharibi zikiongozwa na USA ni maharamia, majambazi au waporaji wa rasilimali zetu waafrica. Na ukiwatunishia misuli unaumia kweli. Ila mwamba JPM alithubutu kuwachana hadharani, na kuvunja mikataba Yao ya kidhalimu. Hilo anahitaji pongezi za hali ya JUU sana.

Lingine huyu mwamba alikuwa mchapa kazi sana. Alitamani kwa muda wake wa miaka 10 bongo iwe kama ulaya. Alikuwa vzr sana. Udhaifu – Alikuwa na moyo wa plastiki (hana ustahimilivu ktk kukosolewa). Ukimkosoa tu umepotea. Hakupenda democrasia kabisa yan, muasisi wa utekaji na mauaji.

*SAMIA – Amefanikiwa sana kukomesha rushwa. Wengi watalikataa lkn haiondoi ukweli. Watumishi wa umma pekee ndo watanielewa hapa. Waulize TRA na matrafic watakuambia.

Malipo yote ya serikali kwa sasa yanalipwa kwa control number. Hakuna malipo ya mkononi, na katika malipo ya mkononi ndo kunakopigwa hela huko. Cheti cha kuzaliwa unaambiwa 50, cheti kinaandikwa 22000! Sasa hv ni 10000 tu, tena unalipa online. Wapigaji wamekosa madili hapa.

Watu wengi hawajui, wanamlalamikia huyu mama eti rushwa imezidi katika utawala huu! Imezidi wapi? Katika maraisi wote, huyu mama amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuzuia mianya ya upotevu wa pesa za serikali. Ukibisha we bisha tu kwa kuwa una mihemko yako.

Pia amejitahidi kukamilisha miradi yote aliyoianzisha jpm kasoro train ya umeme tu ambayo imebaki kumalizia tu. Katika mambo yanayonifurahisha sana ni ujenzi wa vituo vya afya kila tarafa na kukamilika kwa mradi wa bwawa la Mwl Nyerere.

Umeme kwa sasa ni 24/7. ukikatika ni dk 5 au 10. Hongera zake nyingi saaaaanaaaaa.

Udhaifu ni ule muendelezo wa mabaya ya JPM. Anapaswa kuendeleza mazuri ya jpm, jk wa pili na wa kwanza, mwinyi na mkapa na kuachana kabisa na mabaya Yao. Mfano ishu ya kuteka watu badala ya kukamata ni tatizo kubwa.

Ila nashukuru kwa waziri wa mambo ya ndani ametoa maelekezo. Kama yatafuatwa vzr itakuwa poa sana. La pili ni uchaguzi huru na haki. Sijaona utofauti wa jpm na awamu hii katika uchaguzi. Akirekebisha haya mawili, tuna bonge la kiongozi.

Naruhusu kukosolewa kwa namna yoyote ile.
 
Yan mtu hakishiriki hata uchaguzi, lakini ndo anakua bora. Basi ile sera yake ya NRNE ilikubalika. CDM kina nguvu saaana
IMG-20251216-WA0021.jpg
 
Samuya atabaki kuwa the worst president ever in our beloved Tanganyika!.
Hata kitendo cha wananchi wengi KUTOKUJITOKEZA kwenda kupiga kura ile tarehe 29 oct maana yake ilikuwa wananchi walinusa mengi ya hovyo baada ya kuona uongozi wake kipindi cha urais wa kurithi!.
Funga kazi ni mauaji ya watz aliyoyaamuru (alikiri mwenyewe akizungumza na wazee wa mchongo) tarehe 29 oct na siku zilizofuata!!.
 
Hiyo control number inatibu rushwa kweli? Imekwaje basi huduma za kijamii hazikui ilivyotarajiwa badala yake miradi ya watu binafsi mitaani tunaona inaota kama uyoga km shell majumba,magari nk mengi yakifanywa na watumishi wa umma.Kuna siri gani hapo?
 
Ndugu yangu, mimi sipo hapa kubishana.Ndiyo maana nimesema ukiondoa mihemko utanielewa.Hv Mimi mtumishi wa serikali nazuiliwa kuanzisha biashara yangu?Hujui kama mabank yanatoa mikopo kwa watumishi kwa dhamana ya mshahara?Na kiwango kinategemea na TGTS yako.Kama mtu mwenye cheo cha afisa elimu anaweza kupewa hadi milioni 200,wabunge hadi milioni 500,mawaziri je hawawezi kukopeshwa bilioni moja?Sasa bilioni moja anashindwa kujenga ghorofa?kama ukiwa na mtaji wa milioni 50 unaweza kujenga na kuanzisha Petro station,bilioni moja inajenga sheli ngapi?
*Hili la miradi ya serikali kisimama nadhani labda wewe unaishi Kenya.Mimi huku nilipo miradi ya serikali mingi imekamilika.Shule,vituo vya afya na zahanati vyote sasa Hivi vinafanya kazi na watu tunatibiwa kwa gharama nafuu kuliko hapo awali,maana tulikuwa tukitumia private hospital.Kitaifa leo tatizo la umeme ni historia,daraja la jpm tunapita bila tatizo kwenda kigoma,relief ya mwendokasi Bado kidogo tu kipande cha kwanza kikamilike na watu wapo kazini(Mimi mwenyewe nashuhudia hapa nilipo).Sasa wewe hiyo miradi unayosema imesinama inapatikana wilaya gani!!Kuwa mkweli mkuu.Ndiyo maana mimi Sipendi kuwa mwanasiasa.Uanasiasa ni uongozi na fitna tupu!Wanaharakati karibu wote ni wanasiasa,kama si wa ccm basi wa upinzani.Kuweni kama mzee warioba.Yeye anasimama katika ukweli hata kama utamgharimu kiasi gani.Nimeanza kumfuatilia tangu akiwa mwenyekiti wa tume ya katiba mpya.Hajawahi kuyumbishwa hadi sasa.Lkn wengine ni uchawa,chuki,fitna.
 
Control number alianzisha JPM...usimshuhudie huyu bibi uongo!

Samia alichofanya cha kipekee kabisa ni uporaji wa madaraka mchana peupe.
Usiwe mwenye mihemko ya umagu mzee.Wanazi wa magu mna shida sana.Kila jema ni la magu na Kila baya ni la kikwete na Samia!Hatuendi hvyo mzee.Waulize wafanya biashara,au watumishi wa umma watakuambia.Najua wewe unaongea tu kwa mihemko au kusikia lkn pengine hata hujawahi kufanya malipo kwa control number.
 
Sawa, huo ni mtizamo wako siwezi kukuondoa huko.

Ila kwenye suala la malipo ya serikali kwa kielektronik (GePG = Government Electronic Payment Gateway) ilianza rasmi 24 November 2017.
Taasisi ya kwanza ya serikali kuanza kutumia huu mfumo ilikuwa ni RITA.
Kwenye hili Ninazungumzia uzoefu sio siasa na ubishi wenu usiokuwa na tija.

Kama mwaka huo Samia alikuwa madarakani, basi ni sawa alianzisha yeye.
 
Marekani njoo utwange magaidi ccm yametuua Zaid ya elf Tena mikoa ya wakristo wengine Songwe,mbeya, Arusha, amelenga mikoa ya wakristo. Mikoa ya waislam hajaua kama Pemba,unguja,Tanga,pwani,
 
Ndugu yangu, mimi sipo hapa kubishana.Ndiyo maana nimesema ukiondoa mihemko utanielewa.Hv Mimi mtumishi wa serikali nazuiliwa kuanzisha biashara yangu?Hujui kama mabank yanatoa mikopo kwa watumishi kwa dhamana ya mshahara?Na kiwango kinategemea na TGTS yako.Kama mtu mwenye cheo cha afisa elimu anaweza kupewa hadi milioni 200,wabunge hadi milioni 500,mawaziri je hawawezi kukopeshwa bilioni moja?Sasa bilioni moja anashindwa kujenga ghorofa?kama ukiwa na mtaji wa milioni 50 unaweza kujenga na kuanzisha Petro station,bilioni moja inajenga sheli ngapi?
*Hili la miradi ya serikali kisimama nadhani labda wewe unaishi Kenya.Mimi huku nilipo miradi ya serikali mingi imekamilika.Shule,vituo vya afya na zahanati vyote sasa Hivi vinafanya kazi na watu tunatibiwa kwa gharama nafuu kuliko hapo awali,maana tulikuwa tukitumia private hospital.Kitaifa leo tatizo la umeme ni historia,daraja la jpm tunapita bila tatizo kwenda kigoma,relief ya mwendokasi Bado kidogo tu kipande cha kwanza kikamilike na watu wapo kazini(Mimi mwenyewe nashuhudia hapa nilipo).Sasa wewe hiyo miradi unayosema imesinama inapatikana wilaya gani!!Kuwa mkweli mkuu.Ndiyo maana mimi Sipendi kuwa mwanasiasa.Uanasiasa ni uongozi na fitna tupu!Wanaharakati karibu wote ni wanasiasa,kama si wa ccm basi wa upinzani.Kuweni kama mzee warioba.Yeye anasimama katika ukweli hata kama utamgharimu kiasi gani.Nimeanza kumfuatilia tangu akiwa mwenyekiti wa tume ya katiba mpya.Hajawahi kuyumbishwa hadi sasa.Lkn wengine ni uchawa,chuki,fitna.
Hoja zinazotolewa na CAG bila hatua madhubuti kuchukuliwa zinaonyesha unatetea ufisadi
 
Back
Top Bottom