Haya madawa ya kienyeji ya kutakatisha nyota huwa yana expire kwa hiyo lazima kuya boost mara kwa mara kwa kutoa sadaka ya kuchinja either mnyama au binadamu.
Kweli jamaa kakalia kuti kavu hata urais anauona mchungu - maana mambo yake hayaendi vizuri
a) Mawasiliano ya Ikulu kuhusu Dowans yana walakini mkubwa, Mkurungenzi badala ya kujibu hoja yeye anakuja na vijembe
b) Bei ya umeme juu wakati umeme wenyewe haupo
c) Huko Arusha nako usiseme, huyo Chitanda, Makamba, Mwema na Nahodha wanaonekana mizigo ndani ya Chama na Serikali
d) Soo la Kuilipa Dowans nalo halimpi usingizi
e) Maaskofu na Wakuu wa dini wameikalia koo Serikali kwa utendaji mbovu kusababisha mauaji yasiyo ya lazima Arusha
f) Suala la Katiba nao halimpi usingizi, Werema naye kupingana na Baadhi ya Mawaziri na Rais kuhusu tamko la Katiba mpya.
f) Maisha ya Mtanzania yanazidi kuwa magumu mno - hasira zao zinamwangukia yeye na CCM yake.
Kuyatolea ufumbuzi masuala haya yote kabla na nusu ya mwaka huu unahitaji kuwa na serikali makini chini ya Rais mchapakazi na mwadilifu, na sina uhakika washauri wake wanafanya kazi aliyowapa maana mambo si swari ki ujumla.
Hizi dawa za kusafisha nyota kuna wakati huwa haziwezi kufanya kazi yake endapo utakuwa umesababisha umwagaji wa damu hasa ya watu - hili la Arusha halisafishiki wa Kafara - hili linahitaji kuomba radhi live kwa watanzania wote wakusamehe.