Ujengelele
JF-Expert Member
- Jan 14, 2008
- 1,253
- 22
Kazidi uzururaji katika nchi za watu, hii hali ikiendelea kwa miezi kadhaa labda itabidi Sitta aingie Ikulu.
Mi naona azamie kimoja huko huko. Hana faida yeyote. Angekwama Obama, J. Zuma, Jonathan etc ungesikia CNN. Lakini hako kajamaa bure tupu.
Kulia au kutolia inategema unalilia nini na kwa sababu gani si kila mtu akifa lazima nilie, inategemea mtu huyo ameyagusa maisha yangu kwa kiasi gani kama kila mtu akifa lazima ulie mbona watu wanakufa kila siku basi kila siku tungekuwa tunalia yalipotokea ya Poland binafsi sikulia ila nilisikitika binadamu mwenzangu kapotea.wabongo bana,yakitokea ya poland nyie ndio mtakua wakwanza kuja lia lia hapa,acheni hizo huyo ndio prezidaa wenu mliomchagua mnaye mpaka 2015,mlie tu.
Halafu bado kuna watu wazima na akili zao wanapendekeza jina lake lipite bila kupingwa october mwaka huu. Kama si wehu ni nini?vitu vidogo vidogo vinamsumbua tu,
ziara hazina tija kwa taifa hili, anazurura tu
halafu mkewe ndo anasomewa taarifa za maendelleo( niliumia sana na kuchukia sana)
ndio maana akirudi huku anakurupuka kusaini sheria za kishenzi shenzi
na kudanganywa ovyo.
natamanan kumzaba vi.......................o!
Kwa vyovyote vile JK ni Rais wa nchi yetu na tupende tusipende kama waungwana tunawajibika kumpa heshima yake. Bila shaka watu wa nchi zingine wanatushangaa kusoma jinsi tunavyoweza kutumia lugha chafu na za kejeli kwa Rais wa nchi yetu. JK pamoja na mapungufu yote tunayoweza kuyaona, yeye bado atakuwa ni Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuwe wastaarabu kidogo hata kama tunadhani ameshindwa kazi! Kama Watanzania waungwana tuliolelewa katika misingi ya utu, upendo na mshikamano, tumuombee arejee salama nyumbani.
Cheusi,
Sidhani kama nimesema kuwa hiyo kazi haifanywi na watu. Nilichoaamisha na ninachopinga ni matumizi ya lugha yanayolenga kumdhalilisha mtu. Naamini Nyange alitaka kumshushia hadhi JK, kitu ambacho siyo ustaarabu hata kidogo!
Kwa vyovyote vile JK ni Rais wa nchi yetu na tupende tusipende kama waungwana tunawajibika kumpa heshima yake. Bila shaka watu wa nchi zingine wanatushangaa kusoma jinsi tunavyoweza kutumia lugha chafu na za kejeli kwa Rais wa nchi yetu. JK pamoja na mapungufu yote tunayoweza kuyaona, yeye bado atakuwa ni Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuwe wastaarabu kidogo hata kama tunadhani ameshindwa kazi!
Kama Watanzania waungwana tuliolelewa katika misingi ya utu, upendo na mshikamano, tumuombee arejee salama nyumbani.
Lakini si yeye mwenyewe JK anajishushia hadhi kufanya afanyayo, tofauti na marais wengine? Marekani kila apatapo kasababu, huku nchi iko katika trajectory isiyo? Aliyesema anashindwa hata kuteua DG wa Tanesco for over 8 mths now huku kuna crisis kubwa ya umeme si kasema kweli kuhusu huyu mjamaa? Hana uchungu wa nchi, ingawa atachaguliwa this year tu kwa sababu anatagemea kura za masikini wengi waliojifunika mablanketi ambao hata hawajui umasikini wao unakuja vipi.
This is nonsense ans should not even be in this forum.. wekeni kwenye porojo..