Kwa vyovyote vile JK ni Rais wa nchi yetu na tupende tusipende kama waungwana tunawajibika kumpa heshima yake. Bila shaka watu wa nchi zingine wanatushangaa kusoma jinsi tunavyoweza kutumia lugha chafu na za kejeli kwa Rais wa nchi yetu. JK pamoja na mapungufu yote tunayoweza kuyaona, yeye bado atakuwa ni Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuwe wastaarabu kidogo hata kama tunadhani ameshindwa kazi!
Kama Watanzania waungwana tuliolelewa katika misingi ya utu, upendo na mshikamano, tumuombee arejee salama nyumbani.